Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,351
- 23,758
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa Hakika Rais Samia Ni Kiongozi Mwenye Maono, ni kiongozi anayeishi mbele ya Wakati ,ni kiongozi ambaye anawaza miaka Elfu moja ijayo,ni kiongozi Mwenye akili kubwa na uwezo mkubwa sana wa kuona mbele.
Ni kiongozi ambaye anafikiria kesho njema ya Taifa letu, ni kiongozi ambaye amebarikiwa na kujaliwa uwezo na maarifa ya kujenga Taifa litakalokuwa na uwezo wa kujitegemea na lenye uchumi imara ,jumuishi na wenye Kugusa Maisha ya watanzania.
Awali wakati Rais wetu Mpendwa anakuja na maamuzi ya kutafuta wawekezaji na kuboresha bandari ya Dar kwa ajili ya kuongeza ufanisi Bandarini. Kuna watu walipiga sana makelele yasiyo na msingi wala kichwa . Makelele yaliyojaa maneno matupu ya uongo ,uzushi na uchonganishi tu. Maneno ambayo yalijaa chuki binafsi tu.
Ambapo watu wakawa wanataka kuleta uchonganishi na kumchafua Rais wetu kwa watanzania kwamba Ameuza Bandari zetu. Jambo ambalo lilikuwa ni la uongo na uzushi tu. Lakini kutokana na ujasiri ,uimara , ushupavu na umadhubuti wa kiuongozi Rais wetu Mpendwa aliendelea kusonga mbele na adhimu na dhamira yake njema ya kufanya maboresho ya Bandari yetu pamoja na kuweka mwekezaji.
Hatua ambayo iliongeza ufanisi pale bandarini na kila mmoja akashuhudia ufanisi ukiongezeka ,muda wa kukaa mizigo bandarini ukapungua na hivyo kupungua kwa gharama. Jambo ambalo limevutia wafanyabiashara wengi sana kutoka Nchi mbalimbali hususani zile za kutoka SADC yaani kusini Kwa Afrika kupitishia mizigo yao kwetu.hali iliyoongeza mapato.
Sasa habari njema ni kuwa Bandari yetu imeweka Rekodi ya Mwaka kwa kupokea Meli kubwa kabisa kutoka shirika kubwa kabisa la Meli Dunia. Kwa kupokea Meli Kubwa kwelikweli ambayo ina uwezo wa kubeba Magari takribani Elfu 9 kwa mpigo yaani 9000. Kiwango ambayo ni kikubwa Sanaaaa kuwahi kushuhudiwa meli ya hiyo kuwahi kutia nanga kwenye Bandari yetu.
Sasa mtu unaweza kujiuliza kwanini hili limewezekana? Jibu ni kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa na Rais Samia yamejenga imani ya Makampuni na wafanyabishara mbalimbali kutoka Duniani Kwote. Pili Kukua kwa uchumi wetu ambako kumepelekea kukua kwa biashara ikiwemo hii ya magari. Kuongezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja. Lakini pia ufanisi na ubora wa huduma unaotolewa Bandarini kwetu.
Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Ni chaguo la Mungu. Anastahili kupewa kura za ndio za kishindo ili aendelee na kazi njema ya kulijenga Taifa letu katika nyanja zote. Baada ya Miaka mitano Tanzania itakuwa ndio Dubai ya Afrika mahali au sehemu ambayo kila mmoja atataka kuja kutembelea na kupita au kufanya biashara au kuwekeza Mtaji wake.
(Soma hapa pia👉Bandari ya Dar es Salaam imeandika historia mpya baada ya kupokea Meli mpya ya kisasa ya kubeba magari, MV Grande Shanghai, iliyowasili kwa mara ya kwanza ikitokea China katika safari yake ya kwanza.
Meli hiyo iliyokamilika kujengwa Julai 2025 nchini China, ina uwezo wa kubeba Magari 9,000, ikiwa na urefu wa mita 220 na upana wa mita 38, ambapo katika safari yake ya kwanza imeshusha Magari 1,624 yakiwemo Malori, mabasi na magari madogo.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Meli hiyo tarehe 21 Septemba 2025, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania( TPA) Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed, amesema ujio wa Meli kama hii ni matokeo ya maboresho makubwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na ushirikishwaji wa sekta binafsi.)
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.