Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewagusa watoto katika vito vya kulea watoto wenye mahitaji maalum na wanaoishi katika Mazingira magumu Mkoani Kigoma kwa kugawa Sadaka ya vyakula ikiwemo mbuzi, mchele, mafuta ya kupikia, unga, sabuni za kuogea na kufulia pamoja na vinywaji vikiwa na thamani ya Shilingi Mil. 10.
Akizungumza mara baada ya kugawa Sadaka hiyo katika vituo vya kulea watoto Sanganigwa B na Brothers of Charity Bangwe vilivyopo Mabispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amesema jamii inapaswa kuiga mfano huo mzuri kwa kuwajali watu wenye uhitaji kwa kuwa wananafasi ya kuishi kama binadamu wengine.
"Ni Muhimu Kujali wahitaji kuliko kuwawekea vikwazo hasa kuwaficha ndani bila kuwapa msaada, hali hiyo inawafanya kukosa matumaini ya kuishi hivyo kuwajali ni kuwapa tumaini na amani katika maisha yao" amesema Andengenye.
Amesema Mhe. Rais Dkt. Samia ataendelea kuwajali watanzania huku akiwatakia kheri kuelekea Sikuku ya Eid El Fitri.
Ameendelea kusema kuwa, ni vizuri watanzania wakasherehekea huku wakiwakumbuka wahitaji na kuwapa faraja, jambo litakalowapa baraka za Mwenyezi Mungu kwani wamekuwa wakisahaulika na jamii bila kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula na mavazi.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma Petro Mbwanji, amesema serikali imekuwa ikishirikiana na wadau kuwalea watoto katika vituo hivyo na kusisitiza jamii kuzidi kuguswa kwa kutoa michango mbalimbali ya kuwawezesha kupata mahitaji ya kibinadamu.
Amesema serikali imekuwa ikitoa uangalizi wa karibu kuhakikisha wanaondokana na ukatili pamoja na kunyanyaswa kwa kupewa mahitaji ya kijamii na Elimu ili waweze kuwa na furaha na amani wawapo vituoni humo.
Wakati huo huo wanaotekeleza jukumu la malezi kwa watoto hao katika vituo hivyo, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kufanikisha misaada hiyo na kwamba itawezesha kusherehekea sikuku ya Eid El Fitri kwa furaha na amani.
Sadaka hiyo imetolewa kwa vituo nane (8) vya malezi