Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi wateule leo tarehe 15 Februari, 2023 Ikulu jijini Dares Salaam.
Viongozi walioapishwa ni pamoja na:
- Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, huku Balozi Dkt. Pindi Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akihamia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
- Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas Said, amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Dkt. Hassan Abbas aliyechukua nafasi ya Prof. Eliamani M. Sedoyeka.
- Mwingine ni Said Othman Yakub aliyeapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas
PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS
Kocha yoyote yule huwa anatazama timu yake inavyocheza. Na baada ya pale, anafikiria ili nipate ushindi basi nitabadilisha namba hii iende defense au iende ikafunge magoli. Tunakupongeza Mheshimiwa Rais.
Niwapongeze na ninyi mlioaminiwa. Bahati nzuri Mh. Mchengerwa, Mh. Pindi Chana, mmekuwepo mnajua maadili ya kiserikali. Natumai jambo mtakalolifanya ni kukaa pamoja nakuona namna gani mnabadilishana hizo namba.
Katim ya wizara ambazo zimekuwa na mawaziri wengi ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii. Ambayo ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu. Ni sekta ambayo mchango wake katika fedha za kigeni, katika ajira ni kubwa sana. Kwahiyo umepewa dhamana ya kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua na kuchangia zaidi katika maendeleo ya nchi yetu.
Lakini vilevile sekta hiyo bahati mbaya sana ina vishawishi vingi. Nina uhakika Dkt. Pindi Chana atakudokeza mengi aliyoona katika kipindi chake. Nadhani mjiepushe na vishawishi hivyo – kama ni kwenye vital una mengineyo.
Lakini katika upande wa sekta ya utamaduni, kwenye takwimu ndiyo sekta ambayo inakuwa hivi sasa kuliko sekta nyingine zote. Na ndiyo sekta ambayo inaajiri vijana wengi – tegemeo la taifa letu kesho. Kwahiyo, ukaitendee haki. Mh. Pindi Chana, uende ukaitendee haki. Vijana wetu wanaitegemea sana hiyo sekta.