Rais Samia, avunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini TASAC

Huu Mkataba ulisainiwa na Raisi Samia wakati Magu (RIP) alisharudi nyumbani.

Mtamsingizia Magu mpaka lini? Usisahau Makamba keshapiga 30 million dollars USD, na Samia ni Raisi wa nchi, atakuja kukana pia.
Hata mie nashangaa
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza wizara kuichukulia hatua bodi ya mamunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa kampuni ‘hewa’.

Maamuzi ya Rais Samia leo Dis. 4 yanafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini.

Dau hili lenye thamani ya Sh bilioni 438.8 lilisainiwa mjini Mwanza Jun. 15, 2021 nakushuhudiwa na Rais Samia. Hata hivyo timu iliyohusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Askari kutoka kikosi ya wanamaji, na wataalamu kutoka MSCL ilibaini kuwa YÜTEK haikuwa na uwezo wa kifedha wala wataalamu kutekeleza mkataba huo.

“Nimeagiza Waziri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuvunja mkataba huo… hata hivyo uwezo wangu ni kuvunja bodi hivyo wenyeviti wote wawili nimewaondoa,” alisema Rais Samia wakati akizindua maboresho ya gati za Bandari ya Dar es Salaam.

Rais Samia amesema mkandarasi huyo alikuwa ameweka wakala nchini aliyekuwa anufaike kati ya Dola za Marekani milioni 1.9 hadi 2 kwa kila meli itakayo jengwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi, Mkandasi huyo hana eneo la kujenga meli (shipyard) badala yake wao ni madalali wa kutafuta kazi na kutoa kwa kampuni zingine. Pia ilibainika kwamba uwezo wa kampuni kifedha ni mdogo mno.

Wasifu na uwezo wake katika ujenzi ni wa mashaka kwani haipo hata kwenye orodha ya wajenzi wa meli inayotolewa na umoja wa wajenzi wa meli Uturuki. “Hili ndio liliotuthibitishi kwamba hawa ni madalali. hawakuwa na watu wenye sifa na vifaa vya kujenga meli. hadi sasa kampuni hiyo haijafanya lolote,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amehoji ikiwa uwezo wa kampuni hiyo ulikuwa ni kutengeneza boti ndogo.

“Tujiulize tenda hii ilitolewa na bodi husika ya wizara ama shirika. Shirika linabodi ya wakurugenzi ambao wamepitisha tenda hii lakini pia mkandarasi alifanyiwa due diligence. Sasa haya tumeyabaini hivi karibuni, huko nyuma yametokea mangapi?” alihoji nakutaka tenda bodi iliyohusika, bodi ya wakurugenzi kuwajibishwa.

Chanzo: Habari leo
 

Rais Samia anashuhudia utiaji saini mikataba 5 ya ujenzi na ukarabati wa meli Shilingi Bilioni 417. Kihoja … hadi anashughudia utiaji saini alikuwa hajastuka tu? Maza anaibiwa sana​

 
Hana lolote zaidi ya kutaka kuweka watu wake, waswahili kutoka visiwani 'Zanzibar' na ukanda wa Pwani plus team Msoga; kama alivyofanya TANESCO, wizara ya nishati na kwingineko
Kutesa kwa zamu, six years back
Kuna waliokuwa wakisema hivi hivi
Huku wakitaja kanda ya ziwa, kabila flani hivi na dini flani hivi
So no way
Tuvumilie tu
 
chief hili linchi ligumu sio rahisi kama tunavyofikiria.... bila ukatili na ubabe haliwezi kwenda kama tunavyofikiri, mijitu ni mijinga na mipumbavu huko hatari...

Wakati wananchi wanalalamikia tozo na inflation kuwa juu, kuna mijitu inaiba na kufanya ujinga huku mitaani, masemina yasiyo na maana + kulipana miposho na matumizi mengine ya hovyo matokeo yake serikali haina hela tunakwenda kukopa...

Amini leo, nchi hii inahitaji ukali na unyama mkubwa sana ili watu wakae kwenye mstari na kujitambua wao ni watumishi wa umma na wapo kutumikia mamilioni ya watanzania masikini..

Leo hii wizi kama huo unafanyika halafu unashangaa serikali haina hela yakujenga madarasa huku lijitu na wenzie kwa kushirikiana na foreigners limelipwa hela mbuzi linatanua huku mtaani na vimada na kujiona lenyewe lichapa kazi balaa...
Ninakubaliana kabisa, tena ninaunga mkono mawazo haya, mradi tu yawe si ya kuoneana na kuzushiana tu kwa sababu za pembeni, kama za kisiasa kwa upande wa wapinzani.

Rais Samia Suluhu Hassan, kama anapenda kuacha alama za uongozi wake ndani ya nchi hii katika miaka hii michache toka hii leo hadi 2025, akiamua kupambana kwa dhati kabisa na hii mijitu isiyosikia lolote, akapambana nayo kwa njia za utaratibu unaojulikana kisheria, hili peke yake litamweka juu sana na kumpa heshima.

Lakini najuwa hawezi kufanya hivyo.
 
Acha kuwaza kijijnga jinga eti katiba katiba .ndio katiba mhim lakinj usifikiri kuwa bila watu waadilifu hiyo katiba sio chochote sio lolote .Kenya wana katiba bora tu kwa mujjbu wa upinzani lakini inaongoz kwa ufisadi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahyo katiba nzuri sio ishu. Kwahyo tusubiri ikitikea bahati nzuri kupata viongozi waadilifu ndio Mambo yaende. Unategemea kweli tupate viongozi waadilifu wakati Sheria na katiba mbovu
 
Naona Bandari wameamua kumhujumu wazi Rais SSH na juhudi zake za kuinua uchumi.. Wanachelewesha kushusha mizigo bila sababu hivyo kufanya meli nyingi kukimbilia Mombasa.
Bandari ya DAR inadaiwa kuwa na urasimu na msongamano.
Kwa wiki za hivi karibuni Viwanda 7 vikubwa vinavyotumia sukari kwa wingi( kama Tani laki moja kwa mwaka) vinaendeshwa kwa kusuasua baada ya shehena zao za sukari kukwama Bandarini kwa kisingizio cha kutoa kipaumbele kwa shehena za mizigo ya miradi ya kimkakati ya Serikali..
Serikali inakosa mapato kwa ajili ya visingizio vya watendaji..
Inabidi Mkurugenzi Mkuu Eric awe makini sana na watendaji wake..
 
Kusema la haki hata uwe top hawa wanaweza kukumaliza pia hata sumu wanakuwekea

Kumaliza wizi na dhulma ni kazi sana popote pale
Yaani kuna watu wanakushangaa ukikemea wizi halafu hapo hapo walivyo wapumbavu wanalia na ugumu wa maisha

Kama hela zilizotengwa kwenye miradi inapigwa, huku wakusanyaji wa kodi wengi sio waadilfu, huku nako wanapeana tender za mabilioni huku wakikata % zote sio 10% tena

Halafu wanasema eti mpaka KATIBA utafikiri hiyo katiba ni mashine itakayowasaga wahalifu na wavunja sheria

Hiyo katiba nani ataifuata wakati hii yenyewe hakuna anaeijali
Wafuasi wa CDM wao wnaamini hata kumtia mkeo mimba unahitaji katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote tisa baada ya kuongelea ufisadi siku nzima asilimia kubwa ya maamuzi ya nidhamu kamuachia waziri na mkurugenzi wa TPA wakati Magufuli hapo watu kadhaa wangeondoka leo.
Kwenye hili yuko sawa Mamlaka ya nidhamu ndiyo inapaswa kushughulika na mtuhumiwa kadri ya taratibu.

Magufuli alikosea sana ndiyo maana wote aliowatumbua mpaka anakufa walikuwa rumande wanahangaika na kesi. Kimsingi usipofuata sheria kuwatoa kazini lazima watakushinda Mahakamani
 
Kwenye hili yuko sawa Mamlaka ya nidhamu ndiyo inapaswa kushughulika na mtuhumiwa kadri ya taratibu.

Magufuli alikosea sana ndiyo maana wote aliowatumbua mpaka anakufa walikuwa rumande wanahangaika na kesi. Kimsingi usipofuata sheria kuwatoa kazini lazima watakushinda Mahakamani
Afanye anavyotaka lakini asituchafulie shujaa wetu.

Kesho akitaka kuwapa hela tena wazee wa CCM za kumbukumbu ya marehemu mzee Kingunge, awape tu wajikusanye wakapige soga ndio kitu wanachojua lakini sio kuendesha nchi.

Wengine tushakubali matokeo, ndio hali; adapt or suffer thats part of everyday human struggle.

Lakini swala la kumtungia Magufuli uongo alikubaliki.
 
Kwenye hili yuko sawa Mamlaka ya nidhamu ndiyo inapaswa kushughulika na mtuhumiwa kadri ya taratibu.

Magufuli alikosea sana ndiyo maana wote aliowatumbua mpaka anakufa walikuwa rumande wanahangaika na kesi. Kimsingi usipofuata sheria kuwatoa kazini lazima watakushinda Mahakamani
Sababu ya sheria mbovu ndio maana wanaiba bila wasiwasi, wanajua watashinda kesi,
 
Tatizo ka Taifa hili ni sheria imekaa kisoft mno tukiweka sheria kama China Kuna mtu atagusa fedha umma kweli tujiulize Kwanza ,tutaimba umasikini mpaka kiama Cha dunia
 
Back
Top Bottom