Rais Samia, avunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini TASAC

Huu Mkataba ulisainiwa na Raisi Samia wakati Magu (RIP) alisharudi nyumbani.

Mtamsingizia Magu mpaka lini? Usisahau Makamba keshapiga 30 million dollars USD, na Samia ni Raisi wa nchi, atakuja kukana pia.
Anadai amekodi mfumo wa kuendesha Tanesco kwa 69.5 billion hio pesa unaweza ukala laki kila siku mpaka unakufa na chenchi ikabakia. Halafu kuna kenge wanampigia kifua humu eti aachwe afanye kazi😅
 
Maisha ya Ulaya zamani yalikuwa hivi hivi
Hapo nazungumzia kama Uingereza miaka ya 1500, 1600
Wafalme walikuwa wakali haswa na watu kwa kuiba walikuwa wanachomwa moto au kunyongwa au wengine kukatwa vichwa na ku display mbele ya watu ili iwe fundisho

Sio kwamba wazungu wameacha rushwa na wizi wa mali ya umma na kuogopa kukwepa kodi kwa kuelimishwa shuleni au nyumbani
Hapana
Wamechinjwa sana na kuuwawa sana mpaka wakakaa mstari mmoja

Sasa kwetu ukikemea wizi wewe ndio unapotezwa
Eeh bongo ukijifanya Muadilifu labda uwe Top layer kama Rais au Makamu ila chini ya hapo kama si risasi utaundiwa ajali tu uishe.

Nashindwa kuelewa kwanini hawa watu wawili hawa coordinate kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa?
 
Ni kama utani, lakini haya ndiyo yanayotakiwa yafanyike kufuatana na hali iliyopo hapa nchini.

Lakini usitegemee huyu kufanya kama unavyopendekeza. hawa ni waarabu wa Pemba, wanafahamiana kwa vilemba vyao.

Leo umesikia maneno hayo, subiri kesho atakavyofanya yeye au hao atakaokuwa anawatuma kumfanyia.
Sina imani hata ndogo na uwezo wa huyu mama kukabiliana na maovu yanayowaumiza wananchi. Ataishia mipasho ya hapa na pale basi, mambo yanaendelea kama kawaida.

Too bad!

chief hili linchi ligumu sio rahisi kama tunavyofikiria.... bila ukatili na ubabe haliwezi kwenda kama tunavyofikiri, mijitu ni mijinga na mipumbavu huko hatari...

Wakati wananchi wanalalamikia tozo na inflation kuwa juu, kuna mijitu inaiba na kufanya ujinga huku mitaani, masemina yasiyo na maana + kulipana miposho na matumizi mengine ya hovyo matokeo yake serikali haina hela tunakwenda kukopa...

Amini leo, nchi hii inahitaji ukali na unyama mkubwa sana ili watu wakae kwenye mstari na kujitambua wao ni watumishi wa umma na wapo kutumikia mamilioni ya watanzania masikini..

Leo hii wizi kama huo unafanyika halafu unashangaa serikali haina hela yakujenga madarasa huku lijitu na wenzie kwa kushirikiana na foreigners limelipwa hela mbuzi linatanua huku mtaani na vimada na kujiona lenyewe lichapa kazi balaa...
 
Hivi nchi hii Haina majasusi? Mbona Kila tukio ni Kama limetokana na ramli?
Tiss ifumuliwe na ijengwe upya Kwa kuajiri vijana wasomi, wenye ueledi na wazalendo Kwa nchi Yao.
Na dpp anafanya Nini hapo ofisini? Hana maagent wa kumfeed taarifa nyeti ili akamate na kushtaki? Why dpp na takukuru na tiss wasubiri amri ya Rais ndio watende? Hawamfai Madame SSH Kwa hizi loopholes na matobo ya wazi hivi huku Kila mwisho wa mwezi wanachungulia account zao Kama zimenenepeshwa!
Madame SSH, ikikupendeza wafukuze kazi hao wakuu wa idara za takukuru, tiss na dpp Kisha washtakiwe Kwa uzembe wakiwa kazini! Fanya Sasa uliokoe taifa na hizi aibu!

wako kidimbwi pale na mitaa mingine ya ushuani wanakula bata tu....nchi yao hii...kazi yao ni kudeal na petty issues za vijana wa mjini wapate kuishi vizuri...
 
Nchi yangu inasikitisha sana....

Halafu vijana wanaambiwa wapite JKT wakafundishwe UZALENDO.....

Mijitu hiyo ni misinia iliyopita KOZI zote za uzalendo....ona WAKIFANYACHO...

It's terrible 😥

#Siempre JMT

hahahaha umenichekesha sana, yaani mijitu ileile iliyopitia JKT miaka ile ndio mijizi halafu wanasumbua watoto wetu wakajifunze uzalendo JKT.....
 
Mama bila kuwa mnyama na kupeleka watu jela hutaweza kudeal na hizi pumbavu..
Mama bila kuua watu na kutesa wengine huwezi kufanikiwa kudeal na hizi pumbavu...

Mama anzisha kikosi chako maalum haraka kudeal kwa siri na haya mambo, kukufeed proper information, na kuwa well informed na kila kinachoendelea kwenye ground..

Report kutoka kwenye kikosi chako ndio zitaleta maamuzi ya kinyama dhidi ya pumbavu hizi, sio dhambi kuua pumbavu hizi zinazotia nchi hasara na kuua mamilioni ya watanzania kwa kukosa huduma mbalimbali...

Ua, nyonga, poteza wajinga hawa otherwise utakuwa kila siku unakopa na kuomba misaada huku yenyewe ikishibisha mitumbo yao kwa wizi mali za umma...
 
Hii nchi haipiti miezi miwili lazima utasikia upigaji sehemu ..
 
Hana lolote zaidi ya kutaka kuweka watu wake, waswahili kutoka visiwani 'Zanzibar' na ukanda wa Pwani plus team Msoga; kama alivyofanya TANESCO, wizara ya nishati na kwingineko
Bora tu wawe watanzania,elimu,ujuzi na uaminifu kwa nafasi husika
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza wizara kuichukulia hatua bodi ya mamunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa kampuni ‘hewa’.

Maamuzi ya Rais Samia leo Dis. 4 yanafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini.

Dau hili lenye thamani ya Sh bilioni 438.8 lilisainiwa mjini Mwanza Jun. 15, 2021 nakushuhudiwa na Rais Samia. Hata hivyo timu iliyohusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Askari kutoka kikosi ya wanamaji, na wataalamu kutoka MSCL ilibaini kuwa YÜTEK haikuwa na uwezo wa kifedha wala wataalamu kutekeleza mkataba huo.

“Nimeagiza Waziri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuvunja mkataba huo… hata hivyo uwezo wangu ni kuvunja bodi hivyo wenyeviti wote wawili nimewaondoa,” alisema Rais Samia wakati akizindua maboresho ya gati za Bandari ya Dar es Salaam.

Rais Samia amesema mkandarasi huyo alikuwa ameweka wakala nchini aliyekuwa anufaike kati ya Dola za Marekani milioni 1.9 hadi 2 kwa kila meli itakayo jengwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi, Mkandasi huyo hana eneo la kujenga meli (shipyard) badala yake wao ni madalali wa kutafuta kazi na kutoa kwa kampuni zingine. Pia ilibainika kwamba uwezo wa kampuni kifedha ni mdogo mno.

Wasifu na uwezo wake katika ujenzi ni wa mashaka kwani haipo hata kwenye orodha ya wajenzi wa meli inayotolewa na umoja wa wajenzi wa meli Uturuki. “Hili ndio liliotuthibitishi kwamba hawa ni madalali. hawakuwa na watu wenye sifa na vifaa vya kujenga meli. hadi sasa kampuni hiyo haijafanya lolote,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amehoji ikiwa uwezo wa kampuni hiyo ulikuwa ni kutengeneza boti ndogo.

“Tujiulize tenda hii ilitolewa na bodi husika ya wizara ama shirika. Shirika linabodi ya wakurugenzi ambao wamepitisha tenda hii lakini pia mkandarasi alifanyiwa due diligence. Sasa haya tumeyabaini hivi karibuni, huko nyuma yametokea mangapi?” alihoji nakutaka tenda bodi iliyohusika, bodi ya wakurugenzi kuwajibishwa.

Chanzo: Habari leo
Hayo mambo ndo PPRA huwa wanayapenda maana huwa yanakuwa na rushwa nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutalia hivihivi mpaka siku ya kiama. Tatizo mnaamini katika mtu yaan Raisi wa nchi na sio mfumo mzuri, ikiwepo katiba nzuri. Buñge liwe na nguvu kama la mzee wetu wa speed na viwango enzi hizo( tuwe na time huru ya wananchi kuchagua wanaowaamini). Sheria ya mwizi wa kuku jela miaka kumi ila aliyehujumu mabilioni jela miaka mitatu au kulipa faini ya million miatano, hapo kunakitu mnavyoona kweli
Acha kuwaza kijijnga jinga eti katiba katiba .ndio katiba mhim lakinj usifikiri kuwa bila watu waadilifu hiyo katiba sio chochote sio lolote .Kenya wana katiba bora tu kwa mujjbu wa upinzani lakini inaongoz kwa ufisadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliwatoa walioachwa na mwendazake kuwa watamuhujumu,kumbe hata ndugu wanahujumu?
Alisema yeye hatakuwa anafokafoka hovyo....sasa ndo ataelewa kwanini mwendazake alikuwa akifoka.

Wale wa wizara ya fedha hawakusimamishwa mpaka leo kulikoni?
Sijui laikin mama ananiangusha sana inavyoonyesha walikuwa na njaa kali sana ndo maan walisubiri magufuli afe waanze kugawna fedha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eeh bongo ukijifanya Muadilifu labda uwe Top layer kama Rais au Makamu ila chini ya hapo kama si risasi utaundiwa ajali tu uishe.

Nashindwa kuelewa kwanini hawa watu wawili hawa coordinate kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa?

Kusema la haki hata uwe top hawa wanaweza kukumaliza pia hata sumu wanakuwekea

Kumaliza wizi na dhulma ni kazi sana popote pale
Yaani kuna watu wanakushangaa ukikemea wizi halafu hapo hapo walivyo wapumbavu wanalia na ugumu wa maisha

Kama hela zilizotengwa kwenye miradi inapigwa, huku wakusanyaji wa kodi wengi sio waadilfu, huku nako wanapeana tender za mabilioni huku wakikata % zote sio 10% tena

Halafu wanasema eti mpaka KATIBA utafikiri hiyo katiba ni mashine itakayowasaga wahalifu na wavunja sheria

Hiyo katiba nani ataifuata wakati hii yenyewe hakuna anaeijali
 
Ndio hapo unaposhangaa yani anyway tule ugali tushibe maisha yaende
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza wizara kuichukulia hatua bodi ya mamunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa kampuni ‘hewa’.

Maamuzi ya Rais Samia leo Dis. 4 yanafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini.

Dau hili lenye thamani ya Sh bilioni 438.8 lilisainiwa mjini Mwanza Jun. 15, 2021 nakushuhudiwa na Rais Samia. Hata hivyo timu iliyohusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Askari kutoka kikosi ya wanamaji, na wataalamu kutoka MSCL ilibaini kuwa YÜTEK haikuwa na uwezo wa kifedha wala wataalamu kutekeleza mkataba huo.

“Nimeagiza Waziri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuvunja mkataba huo… hata hivyo uwezo wangu ni kuvunja bodi hivyo wenyeviti wote wawili nimewaondoa,” alisema Rais Samia wakati akizindua maboresho ya gati za Bandari ya Dar es Salaam.

Rais Samia amesema mkandarasi huyo alikuwa ameweka wakala nchini aliyekuwa anufaike kati ya Dola za Marekani milioni 1.9 hadi 2 kwa kila meli itakayo jengwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi, Mkandasi huyo hana eneo la kujenga meli (shipyard) badala yake wao ni madalali wa kutafuta kazi na kutoa kwa kampuni zingine. Pia ilibainika kwamba uwezo wa kampuni kifedha ni mdogo mno.

Wasifu na uwezo wake katika ujenzi ni wa mashaka kwani haipo hata kwenye orodha ya wajenzi wa meli inayotolewa na umoja wa wajenzi wa meli Uturuki. “Hili ndio liliotuthibitishi kwamba hawa ni madalali. hawakuwa na watu wenye sifa na vifaa vya kujenga meli. hadi sasa kampuni hiyo haijafanya lolote,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amehoji ikiwa uwezo wa kampuni hiyo ulikuwa ni kutengeneza boti ndogo.

“Tujiulize tenda hii ilitolewa na bodi husika ya wizara ama shirika. Shirika linabodi ya wakurugenzi ambao wamepitisha tenda hii lakini pia mkandarasi alifanyiwa due diligence. Sasa haya tumeyabaini hivi karibuni, huko nyuma yametokea mangapi?” alihoji nakutaka tenda bodi iliyohusika, bodi ya wakurugenzi kuwajibishwa.

Chanzo: Habari leo
Ukiona CCM wanakusifia ujue kuna sehemu. Wanapiga fedha.
 
Back
Top Bottom