PreGE2025 Rais Samia atoa magari saba kwa jeshi la polisi Pwani

PreGE2025 Rais Samia atoa magari saba kwa jeshi la polisi Pwani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,770
Reaction score
2,886
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limepokea magari saba ikiwemo matatu aina ya Toyota Land cruiser mpya (Zero kilomita ) hatua inayolenga kuongeza kasi na ufanisi wa Jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu , kuhakikisha usalama wa raia na mali zao pamoja na kuimarisha utendaji kazi kwenye Wilaya za mkoani hapa

Magari mengine manne yaliyokabidhiwa ni aina ya GWM Single Cabin, yakiwa yamekusudiwa kwa ajili ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).na kwamba magari hayo yote ni sehemu ya msaada uliotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Jeshi la Polisi nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salim Morcase amekabidhi rasmi magari hayo Mei 13 ambapo matatu ni ajili ya Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD'S ) wa Kisarawe, Kibaha, na Bagamoyo ambao ndio waliowawakilisha wenzao wa wilaya zingine kupokea zana hizo za kazi.

Magari mengine manne yaliyokabidhiwa ni aina ya GWM Single Cabin, yakiwa yamekusudiwa kwa ajili ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).na kwamba magari hayo yote ni sehemu ya msaada uliotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Jeshi la Polisi nchini.

Katika hafla hiyo, Kamanda Morcase amesisitiza umuhimu wa kuwa na vitendea kazi kama magari ili kuimarisha ufanisi wa jeshi katika kukabiliana na uhalifu, kuimarisha usalama, na kufikia maeneo mbalimbali kwa urahisi na haraka.

Aidha Subira Tossi ni mkuu wa Polisi Wilaya ya Kisarawe ( OCD) wakieleza namna ambavyo kupatikana Kwa magari hayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao hususani kukabiliana na Uhalifu wameishukuru Serikali kuwawezesha na kwamba msaada huu utaongeza nguvu kazi na kuwezesha Polisi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi katika kulinda raia na mali zao.
 
Kachukulia kwa wajomba au kwa bajeti na kodi za watanzania?
 
Magari mazuri sasa mbona hawaletewagi yale ya kukaa ndani😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Mvua ikianza wanapigwa kama bodaboda😂😂😂😂😂😂
 
Msaada?
Kwa jeshi la polisi?
Kutoka kwa rais..?
 
"kwamba magari hayo yote ni sehemu ya msaada uliotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Jeshi la Polisi nchini."

W@#$&t@#$&f
Mashkolo mageni haya. Tunapewa misaada Kwa Kodi zetu na mtu tuliyemwajiri atuongoze?!!!! Africa yangu. Tanzania wake up my people.
 
Alete hata 100 ila asijisahaulishe no reforms no election
 
Back
Top Bottom