Rais Samia Aridhia Hekta 18,000 za Ranchi Wapewe Wananchi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,475
2,927
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kumegwa kwa eneo la Ranchi ya Kagoma wilayani Muleba na Karagwe katika Mkoa wa Kagera yenye ukubwa wa hekta 18,031.26 kwenda kwa wananchi waendeleze shughuli za kibinadamu yakiwemo makazi.

Hayo yalibainishwa juzi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula katika Kijji cha Rutoro, wilayani Muleba wakati wa kutoa mrejesho wa uamuzi wa baraza la mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwa wananchi wa Rutoro.

Kutokana na kumegwa kwa eneo hilo, wananchi wa Rutoro watapata asilimia 44.44 kutoka asilimia 100 ya Ranchi ya Kagoma huku asilimia 55.56 ikibaki katika ranchi hiyo.

Waziri Mabula alisema kinachowatenganisha wawekezaji na wananchi baada ya uamuzi huo ni mipaka mipya itakayowekwa. Kwa mujibu wa Dk. Mabula, vijiji ambavyo wananchi wake _watanufaika na uamuzi huo ni Rutoro, Kyobuheke, Mishambya na Byengeregere.

"Serikali haijafanya makosa kufanya uamuzi huo bali ni utaratibu unaolenga kuwapunguzia adha waliyokuwa nayo wawekezaji kwa kugombana na wananchi na mheshimiwa Rais hapendi hayo madhara yanayotokea kwa pande zote, ndiyo maana uamuzi umechukuliwa kuwatenganisha," alisema.

Alisema utaratibu uliotumika kutoa maeneo kwa wananchi katika Kata ya Rutoro utasaidia kumaliza tatizo la Mwisa lI kwa kuzingatia mapendekezo ya mkoa wa Kagera.

Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage, mbali na kupongeza uamuzi huo wa serikali alionya wananchi wa Rutoro kuepuka kukaribisha watu baada ya uamuzi huo na kuwataka kutulia kuisubiri serikali iwapatie vitu walivyovikosa.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo naUvuvi Abdallah Ulega, aliwataka wananchi kutovamia maeneo ya watu wengine baada ya uamuzi huo na kueleza kuwa, kufanya hivyo ni kuingia katika hatia na serikali itachukua hatua kwa watakaofanya hivyo.

"Msivamie eneo la mtu yeyote hadi utaratibu utakapokuwa umekamilika na yaliyotangazwa hapa hayamfanyi mmoja kati yetu atoke aende kujimilikisha, atakayefanya vitendo visivyokuwa va kiungwana kwa kuvamia eneo hatakuwa na mtetezi kutoka upande wowote," alisema.
Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais (Mazingira) Khamis Hamza Chilo aliwataka wananchi wa Rutoro kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo wanayokwenda kuishi kutunza mazingira na kuondokana na athari ya tabianchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Nazir Karamagi, alisema amefurahishwa na ziara ya mawaziri wa kisekta katika mkoa wake na kueleza kuwa ujumbe huo umekwenda na mamlaka kamili na kufanya uamuzi waliokubaliana kuhusiana na utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, alieleza kuwa anaamini baada ya mango wa matumizi bora ya ardhi kuwekwa katika eneo walilopatiwa wananchi na hatimaye wakulima kupangwa vizuri utaratibu
wa miradi ya 'umwagiliaji utapelekwa na wakulima watanufaika na miradi hiyo.
Kamati ya mawaziri wa wizara za kisekta ilivohusisha nawaziri kutoka
Wizara ya

Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mifugo ha Uvuvi, Kilimo, Maliasili na Utalii, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) pamoja na makatibu wakuu wa wizara hizo na wale wa Maji, TAMISEMI na Ulinzi lihitimisha ziara yake ya siku moja mkoani Kagera ukiwa mendelezo wa juhudi za kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
 
Serikali ipime kabla ya kuwapa ipime viwanja vya makazi, shule, makanisa etc
 
Kwenye mipango ya ardhi hatuna serikali. Tuna genge la wahuni na wala rushwa limejiweka na kujiundia mfumo wa kihalifu ili kusababisha migogoro isiyoisha. Kwa bahati mbaya sana kila Rais anayekuja anachekacheka tu na kujitafutia sifa bandia za kujitangaza msuluhisha migogoro ya ardhi.

Tuendelee kukataa uporaji wa bandari za Tanganyika.
 
Maeneo serikali iwe inapima kwanza kabla ya kuyagawa kwa watu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom