Rais Samia apokea taarifa ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari, Ngorongoro

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Rais Samia Suluhu, akipokea taarifa ya Tume za Rais alizoziunda kutathmini masuala ya mgogoro wa ardhi na utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Machi 12, 2026, Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume iliyopewa jukumu la kutathmini matumizi ya Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Regarld Ndika amesema licha ya mafanikio yaliyopo katika Hifadhi hiyo zipo changamoto nyingi zinazoathiri matumizi mseto ya Ardhi Ngorongoro na zisipotatuliwa shinikizo la matumizi ya Ardhi na migogoro haitoisha akitaja changamoto mojawapo kuwa ni ongezeko la idadi ya Watu ambao wamefikia 100,793 mwaka 2022.

Akiwasilisha ripoti ya Tume hiyo mbele ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino, Dodoma leo March 12, 2026, Dkt. Ndika amesema "Pamoja na mafanikio zipo changamoto nyingi zinazoathiri matumizi mseto ya Ardhi Ngorongoro na zisipotatuliwa shinikizo la matumizi ya ardhi ndani ya hifadhi halitokuwa himilivu, changamoto hizo ni pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya maendeleo ya Jamii ndani ya Hifadhi kutokana na ongezeko la idadi ya Watu ambayo imeongezeka kutoka Watu 8,000 mwaka 1959 hadi Watu 100,793 mwaka 2022"

“Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu za mwaka 2022 idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia Watu 276,651 mwaka 2050 katika wastani wa ukuaji wa 3.6% kwa mwaka"

"Ongezeko hili la idadi ya Watu linaenda sambamba na ongezeko la mahitaji ya matumizi ya ardhi na kuongeza ushindani wa matumizi ya ardhi kwa ajili ya ufugaji, utalii na maendeleo ya Jamii"

Mapendekezo ya Tume kuhusu Ngorongoro, yamo ya sheria

"Kwa kuzingatia upungufu na changamoto za matumizi ya ardhi zilizobainika, ni dhahiri kuwa mfumo wa matumizi mseto ya ardhi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro siyo endelevu. Hivyo tunapendekeza sheria ya Hifadhi ya Ngorongoro, Sura ya 284, ifanyiwe mapitio na marekebisho kwa kuwashirikisha wadau wote muhimu ili iendane na wakati na mahitaji ya sasa."

Mhandisi Musa Iyombe Mwenyekiti wa Tume ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro

"Tume imepokea malalamiko ambayo yamegawanyika katika makundi matatu, wale waliobaki ndani ya hifadhi…malalamiko kutoka kwa wananchi waliobaki ndani ya hifadhi ni pamoja na kuzuia huduma za kijamii, kuhamishwa kwa fedha za maendele, kuwekewa zuio la ajira kwa wenyeji katika hoteli"

"Tathimini ya Tume kuhusu suala la ushirikishwaji wa wananchi katika zoezi la uhamaji kwa hiari wa wakazi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, halikuwa shirikishi katika kuandaa na kutekeleza mpango wa uhamaji, Tume imebaini kuwa zoezi kwa upande wa wananchi liliendeshwa kwa binu ya ushawishi wa kuhama badala ya ushirikishwaji"

Rais Samia Suluhu Hassan

"Ngorongoro ni urithi wa Dunia sio tu wa Tanzania lakini ni urithi wa dunia na upo kwenye vitabu vya dunia chini ya Shirika la UNESCO, ni lazima sisi ambao tumeshushiwa Ngorongoro na Mwenyezi Mungu tulinde urithi huu wa Dunia"

"Sote tutakubaliana kwamba huu ni mfumo muhimu na wa kipekee kwa ajili ya uhifadhi endelevu wa maeneo haya kwa manufaa ya taifa lakini pia dunia kwa ujumla nasi tumezisikia changamoto tumesikia kwamba serikali tulifanya zoezi kwa nia njema lakini tulikosea baadhi ya maeneo"

"Tumesikia kwamba Serikali tulifanya zoezi [uhamaji wa hiari Ngorongoro] kwa nia njema lakini tulikosea baadhi ya maeneo. Na hayo ndiyo maeneo kukaa, kutafakari na kurekebisha. Kwahiyo tutaendelea na hilo zoezi lakini baada ya kurekebisha."

"Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kupata suluhu za kudumu kwa changamoto mbalimbali zinazotokea ndani ya nchi yetu. Tunafanya hivyo ili tuweze kulinda uhuru wetu, tamaduni na mila zetu na heshima yetu kama nchi."


 
Mbona kumekuwa busy ghafla shitholeni, hatupoi na matukio ya mamaduro wiki hizi, si ajabu atasema tume imeshauri tusitishe na mara moja nawamuru wamasai wabaki walipo

Cheza na the Hague
 
Apokee na hii,mdogo wangu hajaonekana tangu October 29
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…