Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 308
- 424
Hakika mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Anachokifanya Rais Samia Suluhu Hassan kwa watumishi wa umma na wengine, hakiwezi kupita bila kuungwa mkono.
Rais Samia amefanya mambo makubwa sana kwa watumishi katika namna tatu.
Hivi karibuni Serikali ilitangaza ongezeko la kima cha chini cha mishahara kwa asimilia 23.3, kikokotoo cha mafao kupanda haki asilimia 33 kutoka asilimia 25 na posho ya safari kutoka Sh. 12,000 kwa mwezi hadi 250,000.
Hiyo ni kwa kiwango cha juu, lakini pia kutoka Sh. 80,000 hadi Sh. 100,000 kwa mwezi kwa watumishi wa kiwango cha chini na kusaidia kupunguza ukali wa maisha kwa watumishi nchini Tanzania.
Bila shaka, hatua alizochukua Rais Samia zinatokana na mabadiliko ya muda na mazingira hasa ukizingatia kwamba watumishi nchini Tanzania katika kipindi cha miaka sita hawajawahi kupanda ongezeko lolote katika mishahara yao.
Imani yetu kwa sasa sisi Watanzania ni kuona kwamba jambo kama hili linakwenda kutokea katika sekta binafsi pia. Ni ukweli usiopingika kwamba katika sekta binafsi ndiko kuna watu wanaolipwa mishahara mikubwa sana lakini pia ndio hukohuko wapo wanaolipwa mishahara midogo sana. Serikali tulivu ya Rais Samia, tunaamini kwamba muda hautokuwa mrefu sana hadi kusikia viwango vipya ya mishahara katika sekta binafsi.
Hatujaumbwa kuja kukosea tu, na watu tuliowapa dhamana kutongoza sio malaika, hivyo tuaamini kwamba wanakosea, na hapo tunawajibu wa kuwarekebisha. Kama tuna haki ya kuwarekebisha, basi tuwe waungwana pia kumwaga sifa pale wanapofanya vyema kulingana na matarajio yetu. Hiyo inawapa motisha wa kufanya kazi na kuujenga uzalendo zaidi mioyoni mwao.