DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mzee Edwin Isaac Mbiliewi Mtei, kilichotokea usiku wa tarehe 19 Januari, 2026, jijini Arusha.
Kupitia ujumbe wake wa rambirambi, Rais Dkt. Samia amesema kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa niaba yake binafsi, anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
Rais Samia amemkumbuka marehemu Mzee Mtei kama mmoja wa watumishi na viongozi waliotoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa, hususan katika sekta ya fedha, mipango na uchumi. Amesema Mzee Mtei aliwahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali muhimu ikiwemo kuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanzia mwaka 1966 hadi 1974, akishiriki kuweka misingi imara ya uendeshaji wa benki hiyo na uthabiti wa mfumo wa fedha nchini.
Aidha, Rais Samia amesema marehemu ataendelea kukumbukwa katika historia ya siasa za vyama vingi nchini, kama mmoja wa waasisi wa demokrasia ya ushindani wa vyama, akitajwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Rais ameongeza kuwa mchango wa Mzee Mtei utaendelea kuenziwa na vizazi vya sasa na vijavyo, hususan kupitia maandiko yake binafsi (autobiography) yanayoelezea safari ya maisha yake, utumishi wa umma na mchango wake katika ujenzi wa Taifa.
Katika hitimisho la salamu zake, Rais Dkt. Samia amewaombea faraja, nguvu na amani familia, ndugu na wafiwa wote, huku akimuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Pia Soma: TANZIA - Mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei afariki Dunia