Rais Samia anaweza kuwa Mama wa Taifa kwelikweli

Fukua

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
546
479
Salaam.

Mwl J.K NYERERE ndiye baba wa taifa kwelikweli, yaani mwasisi wa taifa letu, ameasisi Mambo mengi ambayo mpaka Sasa yanalifanya taifa kudumu katika amani na utulivu, siwezi kuyaeleza ni mengi Sana na wengi tunafahamu.

Bila kuwasahau marais wengine wastaafu michango yao ni mingi na muhimu Sana kwa taifa letu Kila mmoja kadri Mungu alivyomjalia kuitumikia nchi yetu.

Rais Samia ndiye mwenye usukani Sasa na rais wa Kwanza mwanamke Tanzania, ameingia madarakani katika kipindi ambacho nchi inauhitaji mkubwa Sana wa maridhiano ya kitaifa pia uhitaji wa katiba mpya.

Binafsi Mambo haya mawili ni muhimu sana hata Kama wapo wengine wanaosema katiba mpya isubiri Kwanza, vyovyote iwavyo Katiba Mpya inaweza kudumu kwa Karne nyingi Sana.

Endapo mama na Rais Samia atakubali kuanza mchakato na hatimaye awapatie watanzania katiba mpya basi atakuwa mwasisi wa taifa jipya na Bora la Tanzania yenye maridhiano, na hapo ndipo tutakapo ona maendeleo yanakuja kwa Kasi kwani maendeleo yanaletwa na watu wenye kuelewana, kushikamana na wenye siasa Safi.

Tukubali tukatae Tanzania yetu inahitaji katiba mpya na inawezekana wote CCM na vyama rafiki tukikubaliana kwa dhati.

Niwatakie Serikali na vyama rafiki mazungumzo mema yatakayoleta muafaka mzuri wa taifa letu.

NINATAMANI KUIONA TANZANIA MPYA CHINI YA MWASISI MAMA YETU WA TAIFA MH. RAISI SAMIA SULUHU HASANI
 
emoji1241.png

Matumaini yako yote umeyaweka kwa huyo mtu mmoja? Hapo ndipo hoja yako ilipoishia matopeni!

Huyo mtu mmoja asipokuwepo haiwezekani kwa "Tanzania Mpya" kuwepo?
 
Akitupatia katiba mpya watanzania atakuwa ameweka historia kubwa Kama nilivyoeleza lkn si kwamba nimeweka matumaini yangu yote kwake
 
Yeye hana uwezo wa "kutupatia" au "kutunyima" chochote.

Huo ni uamzi wa waTanzania wenyewe. Kinachokosekana tu, sasa hivi ni uongozi wa kuwatangulia wananchi katika kufikia lengo la kuwa na Katiba Mpya.
 
Anaweza kuamua kuwa kiongozi wa kuwaongoza wananchi kupata katiba mpya
 
Akitupatia katiba mpya watanzania atakuwa ameweka historia kubwa Kama nilivyoeleza lkn si kwamba nimeweka matumaini yangu yote kwake
Binadamu haridhiki hata siku moja. Akitupatia katiba mpya tutadai pia kingine kama kuhakikisha kila mtu ana ajira
 
Salaam.

Mwl J.K NYERERE ndiye baba wa taifa kwelikweli, yaani mwasisi wa taifa letu, ameasisi Mambo mengi ambayo mpaka Sasa yanalifanya taifa kudumu katika amani na utulivu, siwezi kuyaeleza ni mengi Sana na wengi tunafahamu.

Bila kuwasahau marais wengine wastaafu michango yao ni mingi na muhimu Sana kwa taifa letu Kila mmoja kadri Mungu alivyomjalia kuitumikia nchi yetu.

Rais Samia ndiye mwenye usukani Sasa na rais wa Kwanza mwanamke Tanzania, ameingia madarakani katika kipindi ambacho nchi inauhitaji mkubwa Sana wa maridhiano ya kitaifa pia uhitaji wa katiba mpya.

Binafsi Mambo haya mawili ni muhimu sana hata Kama wapo wengine wanaosema katiba mpya isubiri Kwanza, vyovyote iwavyo Katiba Mpya inaweza kudumu kwa Karne nyingi Sana.

Endapo mama na Rais Samia atakubali kuanza mchakato na hatimaye awapatie watanzania katiba mpya basi atakuwa mwasisi wa taifa jipya na Bora la Tanzania yenye maridhiano, na hapo ndipo tutakapo ona maendeleo yanakuja kwa Kasi kwani maendeleo yanaletwa na watu wenye kuelewana, kushikamana na wenye siasa Safi.

Tukubali tukatae Tanzania yetu inahitaji katiba mpya na inawezekana wote CCM na vyama rafiki tukikubaliana kwa dhati.

Niwatakie Serikali na vyama rafiki mazungumzo mema yatakayoleta muafaka mzuri wa taifa letu.

NINATAMANI KUIONA TANZANIA MPYA CHINI YA MWASISI MAMA YETU WA TAIFA MH. RAISI SAMIA SULUHU HASANI
Sukuma gang wanasemaje huko?
 
Back
Top Bottom