Rais Samia anatumia reki sio fagio

Rais Samia anatumia reki sio fagio

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,180
Kwa kutumia fagio hata lingekuwa la chuma kuna watu wangekuwa salama nionavyo anatumia reki la chuma na linapapatua kikweli kweli, japo wananchi wanaitazama hii movie ya Samialism baada ya Magufulism kusimamishwa na alie mbinguni ambayo ilikuwa inaelekea katika uchumi wa juu.

Tunaona baada ya Mheshimiwa Samia kunogewa na kazi ya uteuzi sasa ameshika kasi kubadilisha na kuondoa magome yaliyopevuka katika sehemu mbalimbali za nchi hii, kisemwacho kuwa walikuwa ni mirija ya magufulism. Hatutosikia kutuhumiwa kwa watu wanaoondolewa lakini wabobezi wa mambo ya ndani huwaga wanamwaga mtama.

Tufahamu kuwa Mheshimiwa Rais Samia sio chaguo ni mrithi, kama mambo yake yatakuwa supa katika kuinyanyua Tanzania na watu wake basi anaweza kuwepo madarakani kwa miaka 14, sijui katiba ikoje, ila kama akigombea rasmi 2025 ndio itakuwa ni Rais wa Kuchaguliwa.

Wacha amalize kuseti volume ya Serikali yake tuone kipya atakachokifanya, hadi sasa bado hajatulia na utamu wa uteuzi, lini atamaliza ni kitendawili, ila akitulia na baada ya siku mia, kipimo cha ufanisi wa uongozi wake ndio, utakaowapa dira Watanzania hapo 2025.

Hili reki lipite kwenye tume ya uchaguzi.
 
Muhimu tu asijaribu kabisa kuiga ule uonevu, umungu mtu, ukabila, ubaguzi, ukaidi na ubinafsi wa mtangulizi wake. Akijiepusha na hayo madhaifu, atafanikiwa sana.
 
Kikatiba Samia ana muhula mmoja pekee wa kugombea urais baada ya sasa.
 
Madam tunamsubiri May Mosi.

Wafanyakazi tuna imani madam atatuelewa kama sio ameshatuelewa kuwa tumekanyagwa sana kwakuwa tunatishana sana tumedhurumika sana.

Sasa kuna maneno akisema Utumishi wa Umma Tanzania utapona.

Nadhani anayajua na Najua analijua yeye ambae Katiba (URT) inamtaja kama 'Chief of Comforter'

Asante
 
Tunabadili katiba, vipi hiyo?
Hapana kuhusu hilo liachwe ila yapo ya kubadilisha tuachane na tabia ya kutukuza marais yeye aongoze muhula wake awaachie wengine tanzania ina watu Mil.60+ambapo ndani yake wenye umri wa miaka 45+ si chini ya 10mil, hivyo ni ujinga kuamini kwamba katika idadi hiyo ya watanzania nitu mmoja pekee ndiye mwenye uwezo wa kuongoza.
 
Rais Samia ni rais anayetokana na CCM na anatekeleza ilani ya CCM.

UFIPA NA ZITO wamesahau kujenga vyama vyao wako bize kusifia wana CCM.
 
Mama bado mapema sana kumzungumzia..

Tujipe muda..

Hii nchi inaweza kukushangaza muda wowote.
 
Sasa reki na fagio ni kipi kinachobakiza!?

Tukiachana na hayo... katiba inamtambua Samia kama raisi tena wa awamu iliyokamilika kabisa maana amepokea kijiti na kama atamaliza basi itakuwa miaka inayozidi mitatu hivyo atabakiza awamu moja tu ya miaka mi5 basi

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom