Rais Samia anajenga barabara ya Same - Kisiwani - Mkomazi km 97

Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kazi inaendelea kwa kasi katika kila kona ya nchi,Kaskazini baada ya kusahauliwa kwa muda leo mama anawafungua kwa kasi.

Ona hii barabara ya Same – Kisiwani-Mkomazi kujengwa lami,​

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same – Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46).
Screenshot_20211122-114713.png

Akikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo Eng. Kasekenya amesema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itahusisha KM 11.9 ambapo ujenzi utaanzia sehemu ya Mroyo – Ndungu hadi Kihurio.
Screenshot_20211122-114742.png

Barabara hiyo ambayo inapita pembezoni mwa hifadhi ya taifa ya Mkomazi itachochea na kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi, kilimo, utalii na biashara kwa wakazi wa tarafa za Gonja, Ndungu, Kihurio, Bendera na Mkomazi wilayani Same na hivyo kukuza uchumi wa wakazi hao.

“Tumejipanga kuijenga barabara hii kwa lami na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa”, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.
Screenshot_20211122-114727.png

Aidha amekagua ujenzi wa madaraja ya Mamba na Yongoma ambayo ujenzi wake umekamilika katika barabara ya Mwembe-Myamba-Ndungu na kuzungumzia umuhimu wa wananchi kulinda miundombinu hiyo ili itumike wakati wote wa mwaka.
Screenshot_20211122-114511.png

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando amesema ujenzi wa madaraja na makalvati katika barabara ya Mwembe hadi Ndungu ni zoezi endelevu hivyo kuwataka wananchi kuepuka kulima karibu na hifadhi ya barabara ili kuepuka mmomonyoko wa udongo.

Naye Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malechela amesema ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi (KM 96.46), na Mwembe-Myamba-Ndungu (KM 90.19), ukikamilika utafungua uchumi wa wakazi wa wilaya ya Same ambao kwa kiasi kikubwa unategemea shughuli za kilimo cha mazao ya tangawizi na ndizi na kuhuisha utalii katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi.
Heko Mama
 
Tuendelee kuchapa kazi
 
Haya mnaosema Rais Samia hafanyi kitu njoo mtazame hii. Narudia tena,Tanzania tunaye Rais wa kujivuna na kujivunia.
Mnapata taabu sana sana kwenye huu mradi wenu wa kumdanganya rais.

Mnachompendea ni pesa mnayopewa kueneza propaganda iliyoshindwa.

Hali ni mbaya mno. Watu hawwna mafumaini ya hata ya huo mlo mmoja kwa siku. Maji, umeme, afya vyote ni mtihani

Pia huyo rais anatoa wapi hela hadi mseme YEYE ndo anajenga? Hana mawaziri?
 
Back
Top Bottom