Rais Samia anaidekeza safu yake ya uongozi

Rais Samia anaidekeza safu yake ya uongozi

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
765
Reaction score
490
Hivi ni kweli mpaka leo umekosekana ufumbuzi wa suala la umeme, nchi nzima na kiza kimetanda, au mama hajui au anaongopewa? Mpaka imejidhihirisha uwanjani mechi za kimataifa haoni? Hizi kelele mitandaoni hazioni?

Mama usitegemee kua kuna siku utasikia taarifa mbaya ya safu yako kwenye vyombo vya habari sababu Nape anafanya kazi nzuri ya kuziba midomo yao.

Kiongozi wa kweli na mwenye kusimamia haki kwa uadilifu hua ana watu wake wa siri wa kumletea matatizo ya wananchi wake, usiamini chawa na kama sasa hivi unao basi wanakuongopea.

Mtaani kila siku matangazo watu wanapotea hawajulikani walipo na hawarudi wapo wapi?

Mtaani watumia madawa wa kulevya wameongezeka, ngada zinauzwa nje nje na baadi ya vitengo vyako vya usalama kua mawakala wakuu.

Matapeli wamejazana wanalindwa na vyombo vya dola wanafanya yao kwa uhuru na kujiamini, yani kama wewe ni tapeli ujisamishe tu kwao uwe unapeleka hesabu.

Wamama wanaojiuza wameongezeka hali ni mbaya huku pesa unazotoa kusaidia maendeleo ya kinama kuliwa na wajanja wachache wanaojiita wanaharakati wa maendeleo ya wanawake.

Sisemi hayapo mazuri ambayo unafanya ila mabaya yanaonekana zaidi. Mama jitafakari mungu amekupa wadhifa wa kusimamia maisha ya watanzania, kusema kwetu sio kwamba tuna gubu ila nadhani huyajui ya mtaani maisha magumu mno, sio mfanyakazi, mfanyabiashara wala mkulima hali tete.
 
Nenda kinondoni Sasa hivi.

Wahuni wote wamerudi Tena kwa kasi ya ajabu.
 
Back
Top Bottom