Rais Samia ana bahati, ni Mungu alimpangia au vyote viwili?

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Nimekua nafuatilia sanaa na sayansi ya majina kwa ukaribu japo sio kwa sana.

Na leo pia nimeamua kutafiti kwenye mtandao maana ya jina Samia. Nimekutana na tafsiri nyingi ila kwa sasa naomba nikushirikishine hii moja. Samia as a girl's name is of Arabic origin, and the meaning of Samia is "exalted"

Hii imenipa kukumbuka wakati Malaika Gabriel anamtokea Yusuf, alimwambia mtamwita Yesu ikiwa na maana "ni yeye atakaewaokoa wanadamu na dhambi zao".

Wakati nabii Isaya apewa jina la Emmanuel kama masihi ajae, alimbiwa tasfiri ni Mungu anakaeishi katikati ya wanadamu/Mungi pamoja na wanadamu.

Kwa wale tunaozaa bado, kumbe kuna haja ya kuzingatia jina gani mtoto apewe. Inasemekana names have power, names have purpose and names have destiny.

Ukisoma historia ya Goodluck Jonathan kwa namna alivyopanda mpaka kufikia kuwa rais wa Nigeria unapata kuona nguvu iliyomsukuma toka maisha ya kawaida ya kushika chaki chuoni mpaka kufikia cheo cha makamu wa Rais na baadae kurithi madaraka kama madam President Samia hapa kwetu. Na baadae kugombea na kushinda uchaguzi.

Nihitimishe kwa kumtaka mwenye nafasi kusoma kitabu cha this child will be great. Ukipitia kurasa kwa kurasa unaweza kuona namna Ellen Johson Sirleaf alitoka kuwa mtoto wa kawaida alieolewa mapema akiwa hana shule "kiviile"; mpaka kuweza kufika US kwa bahati na kulazimisha. Ila shule aliyosoma US ikampa maarifa na turning point maishani mwake.

Ofcourse kuwa na jina zuri ni kitu kimoja na kukomaa ni jambo la pili. Angela Duckworth katika kitabu chake cha Grit: The Power of Passion and Perseverance. Angela kaweka wazi kuwa pamoja na karama au jina zuri, shauku/hamu/tamaa/njaa na uvumilivu wa kuyachumilia makubwa hasa kwenye kugusa maisha ya wengine.

Ninapozungumzia kugusa maisha ya wengine hii ni kwenye siasa, biashara, taaluma, sànaa au chochote ambacho wanadamu kapewa ili dunia iliyomzunguka ifaidike na uwepo wake.

Waingereza wanasema names have potential, names have purpose & names have destiny.

Hongera Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kufikia kwenye nafasi ya juu ya utumishi Tanzania. Maombi yetu kwa Mungu utende haki kwa kugusa maisha ya Watanzania ili wajivunie uwepo wako katika nafasi/kitu ulichoketi.

Kwa wazazi tunaoendelea kuzaa, tufikirie mara mbilimbili na kwa kina kwanini mtoto aitwe. Ila pia tuwape nafasi ya kuwajenga kimalezi na maadili. Sio wote wataenda straight juu. Wengine watakomaa sana, mama Samia amekomaa. Haikuwa easy to the throne, ila kwa uvumilivu na jitihada kaweza kufika juu kabisa kwa utumishi hususan kwenye duru za siasa.

Kuna ambao wanaweza kusema bahati ila mwenzetu ulifanya ground work ya kuingia kwenye duru za siasa kuanzia Zanzibar mpaka ukaja bunge la JMT. Basically Bunge la Katiba ambalo halikuzaa matunda ya katiba mpya ila lilitoa platform ya wewe kuonekena. Miaka 5 ya utumishi chini ya JPM utakuwa umeiva vya kutosha kulisukuma gurumu toka sasa mpaka 2025 na baada ya hapo kama utaona inafaa na una nguvu na kuwatumikia Watanzania.

Ramadhani Kareem

Fredfie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom