Rais Samia amuaga rais wa Romania

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,532
Reaction score
3,192
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemuaga Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini leo tarehe 19 Novemba 2023 Ikulu jijini Dar es salaam.

Pamoja na Rais Samia viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali wameshiriki kumuaga kiongozi huyo ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.).

Viongozi wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.


 
Ila waafrika wabaya jmn hebu money Chalamila na Jirani yake walivyo na muonekano wa hovyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…