- Source #1
- View Source #1
Kuna maneno yanazunguka mitandaoni yakimnukuu Rais Samia akitoa ya moyoni juu ya Gwajima kuwa anatumia kanisa kutakatisha fedha, je maneno haya ni kweli kayasema ? Na kayasemea wapi?
- Tunachokijua
- Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha taarifa iliyoambatana na nukuu inayodaiwa kuwa imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimtaka Askofu Josephat Gwajima kutafuta chama kingine cha siasa na kumtuhumu kuwa kanisa lake linatakatisha pesa. Nukuu hiyo inasomeka;
“Wewe Gwajima, acha kunijaribu! Unikome kabisa! Wale wanaokutumia urudi kwao uwaambie serikali ya Samia iko imara. Kanisa lako linatumika kufanya money laundering -tutalifunga! Usijaribu kwenda kuchukua fomu CCM kwa sababu wewe ni muasi! Tafuta chama chako.”
Uhalisia wa nukuu hiyo
JamiiCheck imefuatilia inayoonekana kuwa ni nukuu ya Rais Samia kwenye grafiki yenye utambulisho wa Channel 7 News na kubaini kuwa si ya kweli na maneno hayo hayajatamkwa wala kuchapishwa na Rais.
Grafiki hiyo inaeleza kuwa maneno (nukuu) hayo ni ya Juni 05, 2025 lakini ufuatiliaji umebainisha kuwa Juni 05, 2025 hakuna uthibitisho kuwa Rais Samia aliyasema maneno hayo ama kuyachapisha kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Juni 5, 2025 Rais Samia alihudhuria kwenye harambee iliyoandaliwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) chini ya Askofu Dkt. Alex Malasusa yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum.
Akiwa hapo Rais alitoa hotuba yake akigusia masuala mbalimbali ikiwemo kutamka mchango wake kwenye harambee hiyo na hakusema chochote kinachofanania na nukuu hiyo inayosambazwa.
Miongoni mwa maneno aliyoyatamka Rais Samia ni “Huu ndiyo utumishi wa dini, na kazi hii mnayoifanya inapeleka ujumbe kwa wale waliojionyesha kama watumishi wa dini lakini kwa kweli ni watumishi wa ushetani au mambo mengine” akiashiria kulipongeza kanisa KKKT kwa walichokifanya