Rais Samia ameutendea haki Urais

Mimi siandiki hapa jukwaani kwa ajili ya kutafuta uteuzi ndugu yangu
Unaweka namba ya simu kwa tafsiri gani nyingine? Nani humu JF atakupigia simu kwa sababu ya posts za aina hii?

Watanzania wanahitaji umeme na maji vipatikane wakati wote majumbani na maeneo ya kazi. Havipatikani hivyo hakuna lugha ambayo mtu wa kawaida anaweza kuvutiwa nayo
 
Kwani wapi huko uliko ambako hakuna umeme na maji?
 
Samia hana wa kumlinganisha kwenye swala la Uongozi na delivery
 
Pruning the bushes...
Utafika tu, lakini usinisahau
Mimi nahitaji koneksheni ya ukandarasi wa ofisi za chama, tupige pesa ndefu....
 
Umesifia wee mpaka sasa unaandika tanzia kabla ya wakati.

Kuwa na kiasi mkuu.
 
Uwe na adabu kwa kaka yako.mimi sitegemei kununuliwa bando bali napata hela ya bando kwa jasho langu kwa kufanya kazi kwa nguvu na kujituma.
Ili uwe na kipato cha uhakika kilicho halali ni lazima uwe na akili timamu. Kupata hela halali kunahitaji akili.

Wewe kukosa kipato cha uhakika na halali ni sahihi sana. Maana kwa hii akili uliyo nayo, huwezi kuwa na kipato cha uhakika. Labda hela ya kununulia chumvi, mchele na siku nyingine, kitimoto. Lakini lazima utaendelea kutunzwa na baba yako au jirani au ndugu, kwa jitihada zako huwezi kupata hata hela ya kujengea banda la uani kwa kipato halali kitokanacho na mapato halali ya jasho na akili yako.

Ndiyo maana kwa sasa unahangaika kumtapeli Rais Samia kwa uwingi wa sifa za kinafiki ili abebe mzigo wa kukutunza. Pathetic!

Na watu kama ninyi, ikitokea kwa sababu yoyote ile Rais Samia awe nje ya madaraka, hamtapenda hata kulisikia jina lake, mtahamishia utapeli wenu wa sifa kwa yule aliyepo madarakani hata kama huyo mtu atakuwa ni adui mkubwa wa Rais Samia. Kwa baadhi ya nchi zilizofanya mapinduzi, tena ya kumwaga damu, kwa kuondoa uhai wa kiongozi aliyepo madarakani, walitumika watu wanafiki kama ninyi, waliofanikiwa kuwahadaa watawala kuwa wanawapenda sana, kumbe kinachopendwa ni yale madaraka yao yanayoweza kusaidia wao kupata maisha.

Fikiria Samuel Doe aliyejifanya kuwa rafiki mkubwa wa familia ya Rais, kwa kila siku kuisifia familia kwa sifa kedekede za kinafiki, ndiye aliyetumika kumwua Rais William Tolbert kule Liberia. Ogopa sana watu wanaojipendekeza kwako kwa kukusifia kupindukia. Kuna wanachokitafuta.

Watu wanafiki kama Mwashambwa, ni watu wanaotakiwa kuogopwa sana na watawala, maana hawa huwa wapo tayari kufanya chochote alimradi aweze kula na kupata pesa. Hawa ni watu waliojiapiza nafsini mwao kuwa wapo tayari kufanya lolote, baya au zuri, haramu au linalokubalika alimradi tu wapate maisha. Ndiyo maana kiongozi yeyote mwerevu huwaaogopa sana na kupuuza kabisa hizo sifa zao bandia wanazozitoa ili kukupofusha unayesifiwa.
 
wewe nawe mjinga sana
 
Asante kwa mchango wako .nimesoma kila neno uliloandika kuanzia mwanzo hadi mwisho .ambapo umejikita kuelezea kuwa ninaandika na kufanya kazi ya uandishi humu jukwaani kwa lengo la kujipendekeza na kutafuta fursa ya kupata chochote au fadhila au kitu chochote kile kutoka kwa mh Rais.na ikaenda mbali zaidi kwa kutoa mifano ya akina Samuel Doe . Nashukuru kwa mchango wako na mawazo yako na mtizamo wako ambao ni sehemu ya demokrasia na afya ya maendeleo ya kifikra.ambapo inatoa nafasi kwa kila mtu kuwaza awazavyo.

Hata hivyo mimi naandika siku zote humu kwa kumaanisha na siyo kwa ajili ya kusaka uteuzi au fadhila au chochote kile.

Lakini pia hujasema nawe huwa unaandika kwa lengo gani na kumfurahisha nani au kumuhadaa nani ambapo kila siku wewe ni kupinga pinga tu kila kitu utafikiri wewe ni kipofu wa akili na macho ambapo huoni mema na mazuri na makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na mh Rais wetu,yaliyogusa maisha ya mamilioni ya watanzania na kuleta matokeo chanya.
 
Ila wewe Mwashamba nawe siangine bana!

Kama unazidisha Maji badała ya unga!

Hebu jifunze kuchutama Basi badała ya kuanika nyevu nje.

Huoni unajichoresha?
 
Ukweli ni kwamba utawala mbovu na dhaifu kupata kutokea ndani ya Tanganyika wa kwanza ni awamu ya 4 ya JK kisha ikafuata hii ya Mama!.
Hata upambe namna gani ila huo ndo ukweli hata wao wanajua hivyo tena wanakushangaa.



Mtu asipokuwa makini rahisi akajisahau na kufanya hadi ukomo wa kiłę anachosema Mentor wake tu copy and paste?!

Lakini ingekuwa Kheri kufanya zaidi ya kile mentor anachokuelekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…