Rais Samia ameua ndoto ya Urais kwa wanawake wengine nchini!

Rais Samia ameua ndoto ya Urais kwa wanawake wengine nchini!

Una hoja though sidhani kama wanawake wote wana kariba au uwezo sawa, so kwa hoja yako kama SSH ameharibu haimaanishi basi na wengine will do the same.

Mkuu, nadhani umesoma bandiko langu lakini hujaelewa msingi/mantiki yake!
 
Hii habari ya jinsia itatuchelewesha sana. Sisi tuangalie AKILI ya mgombea tusiangalie jinsia yake

Mkuu, nadhani ulichokiandika ni nadharia!

Naomba utambue kuwa katika dunia hii masuala ya jinsia ni mapambano katika jamii.
 
Aisee asije akatokea tena Rais jinsia Ke kilichotokea kinatosha.Hata aliyetaka kufanya alichokifanya SSH alisubira Rais ajaye akifanye,aliyekuja alikitupilia mbali na kusema kisifanyike kwa maslahi ya nchi,Alipoingia mwanamke alishawishiwa kidogo tu akafanya jambo ambalo hamna aliyedhubutu.Mungu atuepushie mbali na viongozi wanawake nafasi za juu serikalini wabakie hukohuko chini majority ya wanawake ni dhaifu!
 
Katika dunia hii kila kitu kina mwanzo na mwisho.

Mwanzo wa suala lolote hujenga msingi ambao unakuwa ni rejeo kwa kizazi na kizazi bila kujali kama ni mzuri au mbaya.

Historia yetu inabainisha wakoloni walikuwa na dhana ya kuwa Watanzania hatuna uwezo wa kujiongoza/kujitawala. Hii dhana ilitumika vizuri kwa muda mrefu ili kuhakikisha hatupati uhuru wetu na kujitawala.

Kwa nchini mwetu, uongozi wa Rais Nyerere ulifuta dhana hiyo na kuweka msingi na rejeo ambalo mpaka sasa linatumika katika kupima uongozi na uzalendo wa Rais nchini.

Kutokana na mfumo dume kutamalaki nchini, dhana ya wanawake kushika uongozi wa juu imekuwa ikipingwa sana na waumini wa mfumo dume nchini lakini dhana hii ilipata mtihani baada ya Rais Samia kushika nafasi ya juu ya uongozi wa kurithi nchini.

Urais wa Rais Samia ulikuwa na fursa ya kuifuta hii dhana ya mfumo dume lakini kutokana na hulka za uongozi za Rais Samia ambazo zimeonyesha wazi kuwa hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi unafanya wanaopigia chapuo dhana ya mfumo dume nchini wanaonekana wako sahihi na kwa msingi huo ameua ndoto za wasichana na wanawake wengine nchini wanaofikiria kushika uongozi wa juu kabisa serikalini kwa sababu hawataaminiwa tena nchini.

Kwa sasa itachukua miongo mingi kwa wanawake nchini kuja kuaminiwa na umma kushika tena nafasi ya Urais nchini kwa sababu ya rejea ya uongozi mbovu wa Rais Samia.

Nimesikia baadhi ya wanawake wameanza kuwalaumu wanaume kuwa ndio chanzo cha kushindwa kwa uongozi wa Rais Samia. Mmojawapo aliyetia lawama hizo kwa wanaume ni Mama Gertrude Mongella.
Angalia video;

View attachment 2765193

Kuna baadhi pia wanasema eti anashauliwa vibaya au eti kuna “genge” la washauri linataka asifanikiwe. Ukijiuliza, kwani hilo “genge” au kundi aliyeliweka katika nafasi za kumshauri ni nani? Kwa mantiki hii tukubali kuwa Rais Samia hajui anachokifanya au ni kama “remote control” na kuna mtu/watu wengine wanaitumia!

Yaani Rais Samia anavurunda halafu lawama wanabebeshwa wanaume.

Kuendelea kuwabebesha lawama wanaume au viongozi wengine haimsafishi Rais Samia bali inazidi kuonyesha kuwa hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi. Hii pia inaonyesha ni Rais kivuli!

Katiba yetu katika Ibara ya 33 na Ibara ya 36 imempa Rais madaraka makubwa na uwezo wa kuajiri na kufukuza mtumishi yeyote wa serikali bila kuhojiwa au kuwajibika kwa mtu/taasisi yoyote nchini. Hii ina maana kuwa lolote linalofanyika serikalini linakuwa na baraka/limekubaliwa na Rais kama hajakanusha.

Kwa miongo mingi ijayo wanawake nchini watakuwa wanapimwa kwa kutumia kigezo cha uongozi mbovu wa Rais Samia.

Wanawake ni vema kwa sasa watambue “mchawi” wao katika kuaminiwa na jamii kubwa kuanzia sasa ni Rais Samia na sio wapenda mfumo dume!
Wivu 😁😁😁

Samia kawapa confidence kabisa kwamba kumbe inawezekana kuongoza wanaume na wakaufyata.

Mwanaume yupi Kwa waliopita anaweza kumfikia Samia?
 
Na spika pia ni sehemu ya waliosababisha wanawake wasiaminike kabisa. Hovyo kabisa!
 
Yani hao wanawake wachache unaokutana nao ndio wakufanye ufikie hitimisho kwamba tumekubali hatupaswi kupewa nafasi za juu?

Angela Merkel ni mwanaume? Tena nafasi ya juu kwa nchi kubwa kama Germany na aliongoza kwa ufanisi mkubwa. Vipi Rais wa Croatia?
Watu mnakutana na wanamama vilabu vya mataputapu huko mnasikiliza mawazo yao ndio mnayatumia kama reference, sio sawa.
Wewe unaweza kumlinganisha kiuwezo Samia na Merkel kiuongozi?
Samia hana uwezo wa kuongoza!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nalia na umeme. Hapa tangia asubuhi hakuna umeme, nani atatusaidia?. Wenyewe baadala ya kuja na emergency strategy wanapenda miezi sita. Very stupid.
Mkuu, Pole sana
 
Attachments

  • IMG_4723.jpeg
    IMG_4723.jpeg
    67.2 KB · Views: 3
Kwa ufupi ni kuwa Rais samia Amewasafishia njia wanawake kuja kushika na kuendeleaa kuaminiwa kushika nafasi za juu za uongozi wa Taifaetu hasa Urais wa Nchi. Hii ni kutokana na kazi kubwa na aliyoifanya na uchapa kazi wake uliotukuka uliyogusa maisha ya wengi na kuleta maendeleo katika Taifa letu.

Wananchi watakumbuka kuwa ni uongozi wa mama wa shoka mama samia ndipi Elimu ilianza kutolewa bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita,huku mikopo kwa Elimu ya juu ikitolewa kwa wanafunzi wote wenye sifa.lakini pia ni wakati wake ambapo fedha ya kujikimu ilipanda na kufikia elfu kumi kwa siku .

Atakumbukwa kama rejea kuwa ni wakati wake ambapo watu hasa wafanyabishara walianza kutunza pesa zao benki bila hofu ya aina yoyote ya kuchotewa pesa zao kinyume na sheria za nchi na kibenki, wafanyabishara watamkumbuka Rais samia na kuhitaji mwanamke mwingine kuongoza Taifa letu kwa kuwa watakumbuka kuwa ni wakati wake pekee ambapo walifanya biashara kwa uhuru huku maafisa wa TRA wakiwa kwaajili ya kutoa Elimu kwao na siyo kuwafungia biashara zao na kuwapa makadirio makubwa ya kodi yasiyoendana na uhalisia wa biashara zao.

Watumishi wa umma watakumbuka kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo walianza kupandishwa madaraja,kulipwa malimbikizo yao ya madeni,kupewa nyongeza ya kila mwaka pamoja na kuboreshewa mazingira ya kazini kwao.

Vijana kwa maelfu watakumbuka kuwa ni wakati wa Rais samia walianza kushuhudia serikali yao chini ya Rais samia ikitoa maelfu ya ajira mitaani ,huku miradi nayo ikimwaga maelfu kwa maelfu ya ajira pasipo ubaguzi.

Vyama vya siasa na wadau wa demokrasia watakumbuka kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo walianza kuzungumza kwa uhuru,kukosoa,kufanya mikutano ya ndani na hadhara kwa ajili ya kutangaza sera zao pamoja na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya nchi na kukaa meza moja na serikali yao.

Wakulima watakumbuka kuwa ni wakati wa mwanamke mzalendo mama samia ambapo walianza kunufaika na kilimo chao ,baada ya serikali yao kuwapatia mbolea za Ruzuku,kuwatafutia na kuwawekea mazingira mazuri ya masoko kwa mazao yao, kuhakikisha kuwa pembejeo hasa mbolea zinapatikana kwa wakati pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha kulifikia soko.wakulima watakumbuka kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo walianza kuinuka kiuchumi.

Watanzania pia watakumbuka kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo kama Taifa lilianza kupokea mafuriko ya watalii na wawekezaji kutokana na kuwa na sera nzuri za kiuwekezaji pamoja na mazingira mazuri ya utalii yaliyochagizwa pia na uimarishaji wa diplomasia yetu kazi iliyofanywa na mama Samia mwenyewe.

Wananchi watakumbuka kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo uchumi wetu ulikua kwa kasi kupita nchi zote za jumuiya ya Afrika mashariki,huku uchumi ukiwa unakuwa katika mifuko ya watu na kugusa maisha yao, kutokana na serikali ya Rais samia kuwekeza mabillioni ya pesa katika shughuli zinazogusa maisha ya mamilioni ya watanzania.

Hayo na mengine mengi yatawafanya wananchi kuendelea kuwaamini wanawake ,kuhitaji CCM impitishe mwanamke Mwingine kama vile mh Dr Tulia Acksoni mwansasu au mh Ummu mwalimu kugombea urais na kuwapatia kura za kishindo.
 
Back
Top Bottom