Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 16,818
- 62,030
Katika nchi yetu, ukiona umepoteza ushwishi kanda ya ziwa ujue una hali ngumu sana ya kisiasa. Kwa sasa dalili zote za kisiasa zinaonyesha kuwa Samia amepoteza uungwaji mkono wa kanda ya ziwa.
1. Press conference ya Gwajima imeizimua kanda ya ziwa.
Katika mitandao ya kijamii nimefuatilia watu ambao wanajitambulisha kama wasukuma au kutoka kanda ya ziwa, wengi wao wanaonyesha kumuunga mkono Gwajima kwa press yake, na kwa kuwa wengi wa hawa ni influencers ni dhahiri moto wa kisiasa dhidi ya Samia huko kanda ya ziwa unawaka.
2. Wananchi wengi waliokuwa mashabiki wa Magufuli wanamuunga mkono Lissu.
Katika angalia yangu ya maudhui katika mitandao ya kijamii na maongezi, wengi wa wanaomkubali Magufuli wanamkubali zaidi Lissu kuliko Samia. Hii inaonyesha kuwa kama watu wa chini, ambao kimsingi wanamkubali sana Magufuli sasa wanamkubali Lissu zaidi basi ni dhahiri Samia ana hali ngumu sana kisiasa. Kwa kulitambua hili mbunge kutoka kanda ya Ziwa Luhaga Mpina amewahi kutweet kuonyesha kuwa hali ya kisiasa ya CCM chini ya Samia ina hali ngumu sana kanda ya ziwa.
3. Umakamu Mwenyekiti wa Heche umeongeza uungwaji mkono wa CHADEMA kanda ya Ziwa.
Kiasili, kanda ya ziwa imekuwa ni kanda ya upinzani, kilichosababisha kabda hiyo kurudi CCM ni urais wa Magufuli. Leo hii kanda hiyo imerejea katika default settings zake za kussurport upinzani. Hii imechangiwa na makamu mwenyekiti kutoka kanda hiyo, na pia kuonekana ni mtu aliyenyooka, mwenye misimamo isiyoyumba na kipawa kikubwa cha ushawishi na sauti yenye mamlaka.
4. Mfumo dume haujamuacha Samia salama huko kanda ya ziwa.
Ukanda wa kanda ya ziwa bado haujaamini mwanamke kuwa kiongozi wa kaya. Haujamwamini bado mwanamke kuwa Jemedari wa kuongoza mapambano. Kwa hiyo it seems Samia bado hajawashawishi watu wa ukanda huo kuwa atosha.
MWISHO.
Ipo kazi kubwa sana ambayo Samia anayo ili kuweza kuwin hearts and minds za Wakazi wa kanda ya ziwa. Hii maana yake ni kuwa kama kanda ya ziwa itaitikia mwito wa no reforms no election basi Samia atakuwa rais atakayekosa legitimacy kubwa sana 2025-2030. Hii haitakuwa afya kwa urais wake na Taifa kiujumla.