Rais Samia aipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

Rais Samia aipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa juhudi inazofanya za kuimarisha michezo nchini akieleza kuwa ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake Tanzania imepata mafanikio makubwa,

Amesema maendeleo yaliyopatikana nchini katika kipindi cha miaka miwili ni pamoja na kuimarika kwa Michezo, Utamaduni na Sanaa.

“Nataka niseme ndani ya miaka miwili hii tumeweza kunyanyua michezo kwa kiasi kikubwa na hii ni kutokana na umuhimu ambao Serikali imetoa kwenye shughuli za vijana, michezo, wasanii, mila zetu na tamaduni zetu. Nawapongeza Wizara na Watendaji wake.

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa timu zote za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa ziendelee kulitetea Taifa kwa kufanya vizuri zaidi huku akisisitiza kuwa ahadi yake ya kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa iko pale pale.

“ Nataka niwahakikishie Mama bado anazo wekeni mipira kwenye wavu, jengeni jina la nchi yetu ” Amesisitiza.
IMG-20230319-WA0004.jpg
 
Soka tumekuwa kiukweli na mama kaongeza chumvi
 
Back
Top Bottom