GE2025 Rais Samia aahidi Bima ya Afya kwa wote ndani ya Siku 100 za kwanza

GE2025 Rais Samia aahidi Bima ya Afya kwa wote ndani ya Siku 100 za kwanza

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mtama Mkoani Lindi kujiandaa na ujio wa Bima ya afya kwa wote, ambayo amesema ndani ya siku mia moja za uongozi wake ikiwa atapewa ridhaa na watanzania, zoezi hilo la bima litaanza kwa majaribio ili kupima ufanisi wake.

Rais Samia amebainisha hayo leo Septemba 24, 2025 wakati akizungumza kwenye Uwanja wa Mtama, Wilayani Mtama Mkoani Mtama kwenye Mkutano wake wa kampeni, akiwataka wananchi kuhifadhi sehemu ya fedha watakayoipata wakati wa mavuno ya korosho ili kuweza kugharamia Bima hizo za afya zitakazosimamiwa na serikali ijayo ikiwa wananchi watakichagua Chama Cha Mapinduzi.

 
@Admns em fanyeni kitu basi.
Tujue kumbe JF ni unkwepable...

Maana kama maCCM yameizima JF then yanakuja hapa kwa VPN...

NINI SASA...
HAYA MANYOOKOO YAPIGENI LIFE BLOCK
 
Huu utapeli wa wanasiasa haupaswi kuchekewa tukatae aise toto afya yenyewe kizungumkuti ndio ije bima ya afya kwa wote kilichoshindikana kitu gani kama sio mauzauza ya uchaguzi ni nini ? Kataa matapeli na wahuni ahadi zisizo tekelezeka mtalia na kusaga meno kwa miaka mingine 5 na bima itakuwa kiini macho
 
Mimi si muumini wa bima yyte ile naona bima ni wizi tu
 
Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mtama Mkoani Lindi kujiandaa na ujio wa Bima ya afya kwa wote, ambayo amesema ndani ya siku mia moja za uongozi wake ikiwa atapewa ridhaa na watanzania, zoezi hilo la bima litaanza kwa majaribio ili kupima ufanisi wake.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Septemba 24, 2025 wakati akizungumza kwenye Uwanja wa Mtama, Wilayani Mtama Mkoani Mtama kwenye Mkutano wake wa kampeni, akiwataka wananchi kuhifadhi sehemu ya fedha watakayoipata wakati wa mavuno ya korosho ili kuweza kugharamia Bima hizo za afya zitakazosimamiwa na serikali ijayo ikiwa wananchi watakichagua Chama Cha Mapinduzi.

View attachment 3478462
Mwambieni Kuna vitu awe anaoongea sio kuropoka.
 
Back
Top Bottom