Rais Ruto: Sitoomba msamaha Kwa kujenga Kanisa Ikulu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Rais wa Kenya, William Ruto amesema hatomuomba msamaha yoyote kwa kitendo cha yeye kujenga Kanisa Ikulu ambapo amewashangaa wanaoanza kuleta manenomaneno kwasababu amejenga Kanisa hilo huku akisisitiza kwamba hajaanzisha Kanisa jipya bali anajenga Kanisa bora zaidi na la kisasa baada ya kukuta Kanisa la mabati ambalo haliendani na hadhi ya Ikulu.

Akiongea leo July 04,2025, Ruto amesema ““Mimi nina muamini Mungu, sitoomba msamaha kwa kujenga Kanisa, tutajenga Kanisa la Mungu, shetani akasirike afanye anavyotaka, naambiwa hata kwa magazeti eti leo Mtu anasema najenga Kanisa Ikulu, ni kweli najenga Kanisa”

“Hapa Ikulu nilikuja nikakuta Kanisa la mabati, Kanisa la mabati linaendana na Ikulu?, hata kwa maoni yenu?, na sijengi na pesa ya Serikali, Mimi najenga na pesa yangu, Mimi sijaanzisha Kanisa Ikulu nilikuta Kanisa likiwepo shida tu lilikuwa la mabati, sasa nimeamua tujenge Kanisa linaloendana na hadhi ya Ikulu na haitogharimu Serikali ya Kenya nitajenga na pesa zangu kwasababu Kanisa la Mungu ni mahali ambapo panatoshana na heshima”

View attachment 3394128

View attachment 3394140
huyu jamaa ni mpumbavu! Ile ni ofisi ya serikali isiyo na Dini!
 
Back
Top Bottom