Rais peleka muswada wa elimu ya wabunge ianzie kidato cha sita, umri mwisho miaka 60 na walipwe na halmashauri zao

pefhana

Senior Member
Mar 26, 2017
158
105
Kwanza naomba tu nikiri kwamba bunge ndio chombo pekee cha wananchi. Ndicho chombo ambacho wananchi wanawasilisha maoni, kero, matakwa, na matatizo yao kwa serikali ambaye ndo mhimili nguzo kwa taifa. Mhimili mwingine ni Mahakama. Mihimili yote mitatu ipo huru lakini utekelezaji wa majukumu ya mihimili miwili (bunge na mahakama) inategemea kuwezeshwa na serikali kwani katika mihimili yote hiyo mitatu, watendaji wake wote ni wa serikali.

Mtakubaliana nami maendeleo ya nchi yetu kiuchumi na kijamii yamekuwa yanasuasua licha ya kujitawala kwa takribani miaka 60 sasa. Licha ya umaskini huu nchi yetu bado ina rasili mali za kutosha ikiwemo ardhi na watu. Tunachokosa ni sera na uongozi bora tu. Naomba nishauri mambo kadhaa hapa chini ambayo yatatuvusha kwenda kwenye uchumi wa kati:

1. Elimu ya wabunge, wawakilishi, na madiwani ni kujua kusoma na kuandika
Katiba ya JMT inamtaka mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika agombee nafasi hizi. Kujua kusoma na kuandika sio lazima uende shule. Kwa maneno mengine hata asiyefika darasa la saba anaweza akagombea nafasi hizi ilimradi tu apewe tuisheni ya kusoma a,e,i,o,u na kuandika jina lake inatosha kuwa kiongozi. Ndugu zangu hili ndo zimwi namba moja lililotuletea umaskini miaka nenda rudi. Tunapata viongozi wasio na upeo, maono, wala mtazamo wa kuwaletea au kubuni mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo chanya. Tusitarajie viongozi maamuma watailetea tija jamii yake na taifa kwa ujumlani ndotoo. Hata aje malaika kuwa rais hawezi lolote kama baraza la madiwani ndo wamejaa watu wa namna hii ambao hata mkataba mdogo tu wa kukukusanya taka katika mtaa au kijiji chake anashindwa kuutafsiri. No way, tutalaumiana tu na tutamlaumu kila rais kumbe kansa zipo na tunazilea zituue vizuri. Tutahangaika sana.

Maoni yangu sheria iweke angalau kidato cha sita ndo agombee nafasi hizi (nasema angalau ), ila ingekuwa angalau digrii moja ingependeza sana. Jamani uongozi siyo kupyayuka tu majukwaani,uongozi ni brain!!!....Hilo ndo lilikuwa lengo hasa la Nyerere, nchi ipate wasomi wakawaongoze wananchi kujiletea maendeleo.... "Those who receive this privilege..." Ninaamini tukiwa na baraza za madiwani mahili kabisa, hii nchi haitakamatika katika Africa. Lakini tuking'ang'ania vipofu wawaongoze vipofu wenzao, mnafahamu kinachoendelea....Hii nchi tumechezewa sana na wazungu kwa kutokuwa na viongozi wanaojiamini, na kujiamini katika mikataba na wawekezaji katika halmashauri zetu hakutokani na ubausa au uwezo wa kuongea bali ni brain upstairs. Nchi hii tuna wasomi karibia kila kijiji, ukiangalia elimu ya mkt wa kijiji au mtaa,na uwezo wake kwenye issue technical, utamhurumia. Magufuli kama kuna sehemu za kuwapeleka wasomi wanotangatanga mitaani bila kazi rasmi basi ni kwenye nafasi za uongozi.

2. Umri wa mgombea ni kunzia miaka 21 hadi infinity (150??)
Hili ni janga lingine. Viongozi wanaimba kwenye majukwaa, watoto ni taifa la kesho na vijana ni taifa la leo. Katika utumishi wa umma umri wa kustaafu ni miaka 55 kwa hiari na 60-65 kwa lazima. Na ili ugombee ubunge sheria inakutaka uwe na miaka 21, urais miaka 42 (kama sikosei). Sasa maajabu; ukienda katika bunge la JMT utakutana na wastaafu ndo wanawawakilisha wananchi. Mtu ametestaafu katika taasisi ya umma au binafsi leo ndio diwani, ndio mbunge ndio rais..!!! Wazungu katika tafiti zao waliona uwezo wa mwili na akili ya binadamu ipo peak (juu sana) katika umri wa ujana, na inapungua kadili umri unavyosonga mbele, na ni zero at infinity. Sasa infinity ya Tanzania inaweza ikawa miaka 100!! au 150!!
Taasisi zilimstaafisha huyu mtumishi kwa uwezo wake wa kuzalisha ulipungua. Leo hii tunamruhusu tena kwa sheria aongoze watu wapate maendeleo!!! Kweli mganga aliyetuloga kafa..ha ha hah!! Taifa lina vijana zaidi ya asilimia 60 ni vijana, na katika hao wasomi wapo, leo hii mstaafu ndo anapewa chapuona vyama eti anafaa kugombea na kuongoza..duh... lazima tubadilike,vinginevyoo tutalaumiana milele bila mafanikio ya kiuchumi na kijamii kwa vijiji vyetu.

3. Malipo kwa wabunge,wawakilishi na madiwani
Ninafurahi madiwani, wenyeviti wa mitaa na vijiji wanalipwa na halmashauri zao. Hii inasaidia kama hakuna fedha madiwani wanajua ni kwa kuwa wamezembea katika kukusanya mapato ya hamashauri. Na hii inakuwa fimbo kwa zile halmashauri ambazo kumejaa uzembe kwenye kuainisha vyanzo,kusimamia ukuaji mapato, ukusanyaji mapato, na kudhibiti matumizi.

Ushauri wangu nikuwa malipo ya wabunge yafanywe na halmashauri zao ili wabunge wawajibike moja kwa moja kwa wananchi kupitia baraza la madiwani katika halmashauri husika. Hii itasaidia mbunge kuwajibika na kuhangaika kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ndani ya halmashauri na kusaka miradi ya maendeleo itakayosimamiwa na serikali kuu au wadau wa maendeleo. Hii itamfanya mbunge kushinda katika jimbo lake lauwakilishi kusaka kero,changamoto, nk ili kuzitafutia ufumbuzi. Itamfanya mbunge kuheshimu na kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani. Hii ndo suluhu ya wabunge kudhani ubunge ni kufanya makazi Masaki Dar na Area C Dodoma. Kwa kifupi italeta uwajibikaji wa Mbunge kwa kuwa atafahamu kabisa mapato ya halmashauri yakishuka hata mshahara... Natamani Mhe Rais afanye hivi na inawezekana kuleta maendeleo.

4. Malipo ya Pensheni .
Sheria ya pensheni inataka mtumishi atumikie utumishi kwa miaka angalau 15 ili apate pensheni au malipo ya uzeeni. Na mabadiliko ya hivi karibuni yameondoa fao kujitoa na kuingiza fao la kukosa ajira. Na mabadiliko ya hivi karibuni sana watumishi watalipwa asilimia 25 tu ya pensheni zao,na asilimia 75 watalipwa kidogo kidogo katika malipo ya mwezi kwa miaka 12.5. Ingawa mabadiliko yote haya ni mwiba kwa mtumishi sio lengo langu kujadili hilo. Mimi naangalia pensheni kwa wenyeviti mitaa/vijij, madiwani, wawkilishi,wabunge, na rais. Je, kwanza hao watu wanastahili pension? ( are they pensionable?). Kuna wabunge/madiwani walikuwa watumishi na walishastaafu na kulipwa pensheni zao!Je hawa wanalipwa pension mara mbili? Kuna wabunge/madiwani wamechangia miaka mitano tu! Je,hawa wanalipwa kwa utaratibu gani ilihali kwanza hawajakamilisha michango 180 (yaani kwa miaka 15), wengi wao hawastahili kulipwa kwani hawajatmiza miaka 55 au 60, labda wangelipwa fao la kukosa ajira baada ya miezi 6 (kama itathibitika hawana ajira baada ya bunge kuvunjwa. Pili hawastahili kulipwa asilimia 100, ilitakiwa kwa wale wanaostahili walipwe asilimia 25 kwa mkupuo na 75 kidogo kidogo kwa miaka 12.5. INAWEZEKANA WABUNGE WANASHERIA TOFAUTI YA PENSION, kama ndio hivyo kwa nini wabunge wawe na sheria tofauti ili hali nao wanachangia mifuko ile ile. NIPO TAYARI KUKOSOLEWA.

5. Mwisho,niseme tu jambo moja. Tukubali au tukatae maendeleo ya Taifa yatatokana na juhudi,maarifa,na mipango yetu sisi watanzania wenyewe. Tusitegemee mzungu ndiye atakayetuletea maendeleo. Hebu jiulize, Finland au Denmark ni nchi ndogo lakini zinachangia bajeti za nchi karibu zote za Africa. Zinachangia miradi mbalimbali ya kijamii katika nchi nyingi za Africa, Hivi tumewahi kuwaza hawa jamaa wanapata wapi uchumi wa kusaidia nchi nyingi namna hii. Ukienda katika nchi hizo wananchi wao wanateseka na kodi kuwa juu, ada za vyuo zipo juu, harafu sisi waafrika tunapewa udhamini na serikali zao katika vyuo vyao. HIVI UMEWAHI KUJIULIZA WAO WANAPATA NINI KUTUSAIDIA WAAFRIKA. JIULIZE MASWALI UTAGUNDUA KUWA HAKUNA KITU CHA BURE DUNIANI. TANZANIA ITAENDELEZWA NA WATANZANIA WENYEWE...
 
Naunga Mkono Hoja
 
Nazan utaratibu huo wa kujua kusoma na kuandikwa uliwekwa kutoka na idadi ya wasomi kwa wakat huo kwa Sasa iyo imepiywa na wakati wasomi Ni wengi tuu ingekua powa Sana kingwekwa tu kigezo Cha elimu ya mmbunge kiwe degree moja walau Basi hata Kama mtu Hana uwezo binafsi wa kuchambua mambo Basi elimu imsaidie
 
sure aisee...bunge la wanaojua kusoma na kuandika tu ni la ajabu. Sio role modes hata kwa vijana wanaoendelea kusoma. Kwaani hutakiwi kusoma sana uwe mbunge
 
Umewaza sana, tena sana
 
Hawezi kupeleka maana hawezi kuwapa miswada ya hovyo wanaojielewa wakiwa wasomi wengi Bungeni..
 
  1. Hakika mkuu unastahili pongezi kwa uwandishi wako mujarabu na pia jinsi ulivyowasilisha hii nyuzi hapa jukwaani. Tukate tukubali viongozi darasa la saba ndio kansa ktk hii inchi, mbunge ambae anajua kusoma kuandika ndio hawa ambao hufanikisha kutunga sheria kandamizi kwa wananchi bila ya kujua athari za hizo sheria kwa kizazi kijacho. Hata mie ningependekeza ili MTU awa mbunge angalau awe ametimu chuoni either awe ametunikiwa cheti cha diploma au degree, tutafanikiwa sana kama tutaondoa hawa wabunge uchwara(std 7)
 
hayo yote yapo kwenye mapendekezo ya katiba ya warioba na ndiyo maana wakaikataa kwa kuwa wengi wa wabunge wangeondolewa na hiyo katiba
Kwa hiyo tunapaswa kuidai katiba ili tuweze kuongea kuhusu maendeleo lakini kwa sasa hata tumleta Baraka Obama atakwama tu
 
Back
Top Bottom