God'sBeliever
JF-Expert Member
- Sep 1, 2015
- 5,788
- 3,067
- Thread starter
- #41
mkuu wewe ndie unaejua uchungu na nchi yako na mlikotoka achana nan hawa watanzania waoga yani wako kigeugeu kila siku. wanavyosema ni mtu hatari ndio ni kweli lakin hawaoni mazuri yake? wapuuzi sana watanzania, nasema tena Paul Kagame ni jembe leo hii Rwanda inaishi kwa amani sababu ya ushujaa wake jamaa katoka mbali sana fikiria kule Uganda alikoishi kama mkimbizi na akapgana hadi museven akaingia madarakani akaamua kurudi nyumbani kwake kutafuta amani ya nchi yake. sasa hawa watanzania hata sio wanyarwanda ina wauma nini. tumpe heshima yake bana.Wakuu, mimi mnyarwanda. Nimeona comments kibao badhi mnamponda Kagame, wengine wanamsifia. Nyote nawapeni big up, kwa sababu kila mmoja ana lake analolijua. Ila napenda tu niwwaeleze kitu kimoja.Hamna kiongozi mkamilifu;kwa sababu lazima kila siku kutakuwa na pande mbili, wanaomuunga mkono na wapinzani. Hivyo, unategemea mpinzani atamuelewaje! Kwa upande wa Rwanda, jameni, acheni, nyie hizi ni habari mnazozisikia, na muombe yasiwakute. Na kwa kifupi asingekuwepo hadi leo hii Rwabda damu ingekuwa inamwagika dakika hadi dakika.Mauaji yalikuwepo toka miaka ya 1959, ili waliwowaita watutsi waangamie na kila mtoto atakaezaliwa alitakiwa awe anaulizia hilo kabila lilikuwa la aina gani! Na isitoshe, waliokuwa wakishiliki mauaji hayo, hata wao walikuwa wanakumbwa na mkasa huo. Sasa unataka kuniambia ni nani alifaidi katika mauaji hayo wakati aliyekuwa anaua na yeye alikuwa alikuliwa? Kazi kubwa aliyoyifanya sasa, unadhani leo hii umoja wa wanyarwanda umetoka mbinguni? Unajua aliyeua na aliyeuliwa leo hii waepatana mpaka watoto wao wanaoana! Hilo jambo kwenu haliwezekani, ila Rwanda limewezekana! Halafu, hajaja kama kiongozi ambaye ana hamu sana na mali ya uma, bali amejitahidi kuuonyesha ulimwengu kwamba utu ndo mhimu zaidi ya utajili.Utapinga sawa, lakini ukiongea na walengwa ndo watakwambia faida yake. Hivyo basi, kama dicteta sawa, sababu ukitaka uongoze vichwa zaidi ya milioni kumi kwa matakwa ya kila mmoja utafika wapi!? Lazima mmoja aonewe ili angalau 100 wasalimike. Na nyie kumbuka wewe unayechat hapa, kuna zaidi ya milioni hata simu hawajaigusa! Jamani, na wao binadamu na wana haki sawa na wewe.Hivyo basi, kubalini ushauli wake, muuchambue muone kipi kina faida kwenu.Mkiona kuna jambo la kuwasaidia, fuateni ushauli wake.Japo mi najua kwa mwendo wa Rais wenu baada ya miaka 5 mtaona faida ya udikteta wake.
pia unakumbuka Libya walimsaliti gaddafi sasa ona matunda wanayovuna.