Rais Paul Kagame aahidi kuwasweka gerezani mahujaji wa Kikatoliki wanaotukuza ufukara

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Hii imekuja baada ya kushutumu watu wanaotembea maelfu ya km kwenda mojawapo ya Kijiji Nchini humo kufanya hija Kwa maelezo kwamba mwaka 1981 Bikira Mariam mama wa Yesu aliwatokea mabinti 2 eneo Hilo.

Kagame amechukizwa na Hali hiyo ambayo Kanisa la Katoliki Rwanda linabariki na kufanya sehemu ya ibada.

My Take: Hili Kanisa Lina vioja sana, nimewahi hoji kwa nini Masista na Makatekista wanafanywa mafukara na kutendewa kama watumwa huku wakila kiapo Cha kutumikia Ufukara?

=============

Kagame promises to imprison Catholic pilgrims who 'worship poverty'​

Rwandan President Paul Kagame has threatened to round up Catholic faithful who visit a global pilgrimage site in his country, accusing them of "worshipping poverty".

Every year thousands of people, many travelling for several days on foot, visit Kibeho, a town in southern Rwanda where the Virgin Mary is said to have appeared to three schoolgirls four decades ago.

But Kagame lashed out at the pilgrims after more than 20,000 attended a Catholic mass in the hillside town on Assumption Day, August 15.

Catholic pilgrims gather for celebrations in Kibeho in southern Rwanda on November 28, 2016 to mark the anniversary of the reported apparition of the Virgin Mary in 1981 in the hope of receiving miracles and being healed from illnesses and disabilities. PHOTO/AFP

In an address to a youth conference on Wednesday, he described the pilgrimage to Kibeho, where the three teenagers said the mother of Christ appeared to them in November 1981, as "horrible".

“I thought that when you pray, you are praying for what can help improve your lives, praying to get rich and get out of poverty," he said.

"No one must worship poverty. Do not ever do that again... If I ever hear about this again, that people travelled to go and worship poverty, I will bring trucks and round them up and imprison them, and only release them when the poverty mentality has left them," said Kagame, himself a Catholic.

It is not clear what prompted the outburst by Rwanda's iron-fisted ruler and the Catholic Church in the country has not yet made any public comment.

The 1981 event was authenticated by the Vatican in 2001 and the site has become a popular destination for Catholic pilgrims from all over the world, many hoping for miracles or cures for illness.

Local media reported earlier this month that the Catholic Church is seeking funding of 3.5 billion Rwandan francs (about $3 million) to expand Kibeho.

Almost all Rwandans are Christians, with Catholics making up roughly half the population.

Chanzo: Monitor
 
My Take
Hili Kanisa Lina vioja sana,nimewahi hoji Kwa nini Masista na Makatekista wanafanywa mafukara na kutendewa kama watumwa huku wakila kiapo Cha kutumikia Ufukara?
To each their own...;

Bora wao wanaosema ukiwa fukara sio mwisho wa maisha (there is more to life that material things) Kuliko hawa walamba asali ambao tunawalipa ili watuondoe kwenye Ufukara lakini badala ya kufanya hivyo wanaendelea kutudumbukiza kwenye lindi la umasikini kwa matozo (kutuingiza kwenye madeni kwa mikopo) bila kuona value for money...

Hawa ndio wakuwafutilia mbali...., By the way masikini ni nani ? Yule aliyeridhika kwa kidogo alichonacho au yule mwenye vingi lakini bado anatembeza bakuli kina kona ?
 
Mimi Kiranga ChaNgeda ni mtu nisiyeamini katika uwepo wa Mungu. Ni atheist.

Siamini Mungu, siamini Shetani, siamini uchawi, siamini malaika, siamini vibwengo, siamini supernatural powers zozote.

Naweka hilo wazi kwanza kabisa, ili maneno yangu yanayofuata yawe na uzito mkubwa kwa kuangalia muktadha huo.

Sasa basi, licha ya mimi kuwa atheist, napenda kupinga vikali sana azimio la rais Kagame.

Licha ya kuwa atheist, mimi ni mtu ninayependa sana uhuru wa watu, ukiwamo uhuru wa kuabudu.

Napenda sana watu wajiamulie wenyewe jinsi ya buabudu, au kutoabudu, bila ya kuingiliwa na wengine, au serikali.

Anachofanya rais Kagame, ni kuingilia uhuru wa watu wa kuabudu, kitu ambacho, kama hakijavunja katiba ya Rwanda, basi kwa hakika kitakuwa kimevunja haki za binadamu.

Raia wa Rwanda wana haki ya kibinadamu ya kwenda kuhiji kokote, kwa sababu yoyote, iwe nzuri au mbaya, almuradi tu hawajamuingilia mtu mwingine uhuru wake.

Sasa leo Kagame kaamua kuwakataza Wanyarwanda wasiende kuhiji Rwanda, kesho akipiga marufuku hija za Mecca itakuwaje?

Nasema hivi, mimi ni atheist, na labda kuna watu wangetegemea kama atheist nifurahie habari hii, lakini kwa kweli imenichukiza. Kwa sababu, rais hatakiwi kuwa na uwezo wa kuingilia haki za kibinadamu za raia wanapoamua kuabudu, vyovyote vile, ilimradi hawaingilii uhuru wa mtu mwingine.

Huu ni utawala wa kidikteta.Maendeleo hayaletwi kwa kulazimisha watu. Waelimisheni watu wajue ujinga ni nini, wataacha hija za ujinga wenyewe.

Ukiwalazimisha watu waache ujinga kidikteta kwenye mambo ya dini, utatengeneza wafia dini usiweze kumaliza ujinga wala kuleta maendeleo.
 
Sayansi, Theologia, Utamaduni na Saikolojia wanayotumia wakatoliki kuimpact imaini Yao kwa wa amini wao ni siri iliyojificha mno mithili ya mitego au mapose ya chatu mawindoni au kwenye purukushani.

Wanamuziki Fulani waliwahi kuimba
Usimchezee Chatu Utaukosa Ushindi
Hawa ni hawawezekani na hawabishanagi
 
Mimi Kiranga ChaNgeda ni mtu nisiyeamini katika uwepo wa Mungu. Ni atheist.

Siamini Mungu, siamini Shetani, siamini uchawi, siamini malaika, siamini vibwengo, siamini supernatural powers zozote.

Naweka hilo wazi kwanza kabisa, ili maneno yangu yanayofuata yawe na uzito mkubwa kwa kuangalia muktadha huo.

Sasa basi, licha ya mimi kuwa atheist, napenda kupinga vikali sana azimio la rais Kagame.

Licha ya kuwa atheist, mimi ni mtu ninayependa sana uhuru wa watu, ukiwamo uhuru wa kuabudu.

Napenda sana watu wajiamulie wenyewe jinsi ya buabudu, au kutoabudu, bila ya kuingiliwa na wengine, au serikali.

Anachofanya rais Kagame, ni kuingilia uhuru wa watu wa kuabudu, kitu ambacho, kama hakijavunja katiba ya Rwanda, basi kwa hakika kitakuwa kimevunja haki za binadamu.

Raia wa Rwanda wana haki ya kibinadamu ya kwenda kuhiji kokote, kwa sababu yoyote, iwe nzuri au mbaya, almuradi tu hawajamuingilia mtu mwingine uhuru wake.

Sasa leo Kagame kaamua kuwakataza Wanyarwanda wasiende kuhiji Rwanda, kesho akipiga marufuku hija za Mecca itakuwaje?

Nasema hivi, mimi ni atheist, na labda kuna watu wangetegemea kama atheist nifurahie habari hii, lakini kwa kweli imenichukiza. Kwa sababu, rais hatakiwi kuwa na uwezo wa kuingilia haki za kibinadamu za raia wanapoamua kuabudu, vyovyote vile, ilimradi hawaingilii uhuru wa mtu mwingine.

Huu ni utawala wa kidikteta.Maendeleo hayaletwi kwa kulazimisha watu. Waelemisheni watu wajue ujinga ni nini, wataacha hija za ujinga wenyewe.

Ukiwalazimisha watu waache ujinga kidikteta kwenye mambo ya dini, utatengeneza wafia dini usiweze kumaliza ujinga wala kuleta maendeleo.
🤭
 
Back
Top Bottom