Rais niombe radhi

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,286
1464896985464.jpg


Rais niombe radhi, tena iwe hadharani,
Kauli yako yakuudhi, imekera si utani,
Leo nakupa waadhi, uandike ukutani,
Nasi tuna yetu hadhi, tulo feli darasani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Nimeketi nimewaza, mkono uko kichwani,
Baba wanita kilaza, mwana atanita nani?
Nini hasa uliwaza? Hebu nitoe gizani,
Hakika umenikwaza, moyoni sina amani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Makosa yalotokea, ni sawa kusawazisha,
Kwa hilo hujakosea, tena nakupa motisha,
Ila ulikoendea, fahamu kwasikitisha,
Yaepuke mazoea, yasije kukutingisha,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Neno likiwa na meno, halifai asilani,
Lisiwe kama ndoano, likatunase vinywani
Ama liwe msumeno, kukata yetu amani,
Lataka liwe mfano, kutoka kwa Sulemani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Kalamu naomba koma, sinitie gerezani,
Karatasi soma zama, hizi sio za zamani,
Ewe wino fanya hima, wangojea kitu gani?
Hapa sasa kaditama, penye kosa samahani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
whatspp/call 0622845394 Morogoro.
 
Wewe kama ulikuwa na four ni kilaza hata unge tunga beti za aina gani lakini haibadilishi kuwa mtihani ulikushinda!

Jiunge na kikundi cha watunga mashairi...
 
Kuna watu hawajui kutofautisha kati ya Tusi na sifa. Kilaza katika lugha isiyo rasmi vyuoni ni mtu alieshindwa kufanya vizuri kwny mitihani. Mlitaka vilaza wa Udom waitwe vipanga?
 
View attachment 353096

Rais niombe radhi, tena iwe hadharani,
Kauli yako yakuudhi, imekera si utani,
Leo nakupa waadhi, uandike ukutani,
Nasi tuna yetu hadhi, tulo feli darasani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Nimeketi nimewaza, mkono uko kichwani,
Baba wanita kilaza, mwana atanita nani?
Nini hasa uliwaza? Hebu nitoe gizani,
Hakika umenikwaza, moyoni sina amani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Makosa yalotokea, ni sawa kusawazisha,
Kwa hilo hujakosea, tena nakupa motisha,
Ila ulikoendea, fahamu kwasikitisha,
Yaepuke mazoea, yasije kukutingisha,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Neno likiwa na meno, halifai asilani,
Lisiwe kama ndoano, likatunase vinywani
Ama liwe msumeno, kukata yetu amani,
Lataka liwe mfano, kutoka kwa Sulemani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Kalamu naomba koma, sinitie gerezani,
Karatasi soma zama, hizi sio za zamani,
Ewe wino fanya hima, wangojea kitu gani?
Hapa sasa kaditama, penye kosa samahani,
Mimi kunita kilaza, rais niombe radhi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
whatspp/call 0622845394 Morogoro.
Umeshauriwa utafute chuo cha saizi yako!! Hapo waachie vipanga. Shida iko wapi, huo ndo ukweli, japo unauma!!!
 
Neno " kilaza" ni la myaka ya 1983 wakati huo kulisikika misamiati mingine kama ",nguini -kusoma arts, "uhanga au UH ikiwa na maana ya kukaukiwa mademu", "odesa", Mzee punch. n.k. Nina imani kuna siku mkuu atayakumbuka.
 
Wewe kama ulikuwa na four ni kilaza hata unge tunga beti za aina gani lakini haibadilishi kuwa mtihani ulikushinda!

Jiunge na kikundi cha watunga mashairi...
kilaza kama anauwezo wa ktunga mashairi hv,bora fani zote zngekuws na vilaza tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom