Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Rais salamu.
Rais wangu kama ni kweli jeshi la Polis mkoani Dodoma limezuia shughuli ya CHASO DODOMA iliyopangwa kufanywa ndani ya UKUMBI, basi itakuwa shughuli ya pili ya kisiasa iliyopangwa kufanywa ndani ya ukumbi kuzuiwa na JESHI LETU LA POLIS kwa kisingizio cha WANDAAJI HAWANA KIBALI.
Rais wangu, tangu mfumo wa vyama vingi uanze mikusanyiko yote ya ndani ya kisiasa haikuwahi kuombewa kibali cha Polis, na mara zote imefanyika kwa amani bila matatizo.
Tangu wewe rais Magufuli uwe rais wetu ndio tunaanza kuona haya mauzauza ya kuirudisha nchi enzi za ujima, enzi za dunia ya KIZA.
* Tulishuhudia mapema mwaka huu TBC ikisitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge kwa kisingizio cha bajeti, lakini baada ya wadau kujitokeza kuiwezesha TBC ili iweze kurusha matangazo hayo, serikali ikaibuka na kisingizio cha watu wafanye kazi badala ya kupoteza muda kuangalia bunge.
Kumbe tatizo haikuwa bajeti???
Serikali hii iliyo izuia TBC wasirushe matangazo ya bunge moja kwa moja ili watu wafanye kazi, imeshindwa kutuambia hadi leo vipindi vinavyo fuata baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni watazamaji wake wakina nani, na je hao watazamaji hawana kazi ya kufanya? Rais wangu, baada TBC kusitisha matangazo ya asubuhi bungeni ili watu wafanye kazi, vipindi vinavyo fuata mtazamaji wake nani ambaye anapingana na kauli mbiu ya HAPA NI KAZI TU?
Rais wangu unajua kuwa nchi yetu sasa imejaliwa kuwa na vutuo vingi vya television na redio, pia serikali imeshindwa kutumbia, watu wanao fuatilia vipindi vinavyo rushwa na TV na Redio hizo hawana kazi za kufanya? Kama wanazo, kwanini sasa isiamuliwe tu vituo vyote vya redio na TV visitishe matangazo yao kila siku kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili usiku ili watu wote wapige KAZI? Hapa utagundua rais wangu hoja hii kutumika kuzuia bunge kurushwa mojakwamoja ilikuwa hoja ya kuokotezwa tu yenye lengo la kuficha dhamira halisi ya serikali.
Rais hauna hadhi wala sifa ya kuitwa dikteta, ila kitendo chako cha kuibariki wizara inayoongozwa na Nape kuzuia bunge kurushwa kama ilivyo kuwa linarushwa awali tena kwa sababu zisizo za msingi, hakika unapo elekea utaitwa jina hilo, sababu madikteta wengi hawakuanza kuwa madikteta bali walianza kuwa maadui wa haki ya wanachi ya kupata habari.
Rais wangu, kutokana na mtiririko huu wa matukio, hata kama wazo la bunge kuwa na studio zake lilikuwa wazo la mhimili huo, tunashawishika kuamini kuwa wazo hilo limetoka katika mhimili wa serikali na hasa ukizingatia utekelezaji wake umewabana vituo binafsi vya TV na baadhi ya matukio au michango ya wabunge huhaririwa kabla ya kurushwa.
* Rais wangu, mikutano na maandamano wakati mwingine kuzuiwa kwa kisingizio cha taarifa za kiitelejensia kuwa na uvunjifu wa amani ni kitu cha kawaida, na tumekuwa tukizoea pamoja na kwamba mara zote tumekuwa tukilikumbusha jeshi la Polis kuwa wajibu wao ni kulinda mikutano na maandamano ya aina yoyote, na kazi yao si kuzuia.
Ila hii ya mikutano ya ndani ya kuombewa kibali cha Polis kwetu ni mpya na kwa vyovyote vile imekuja pamoja na amiri jeshi mkuu mpya wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Nasema hili umekuja nalo Rais Magufuli sababu kabla yako halikiwako, hivyo nafikiri wewe ndio mtu pekee mwenye uwezo wa kuliondosha.
Rais wetu, wewe ni rais wa hapa kazi tu, matumaini yangu hiyo kauli mbiu ya hapa kazi tu, pia itumike katika kukuza na kutanua demokrasia, na kudumisha na kuheshimu uhuru wa kujieleza na wa kukusanyika.
Naomba rais wangu ulitake jeshi polisi liachane na utaratibu wao huu mpya wa kutaka vikao na makongamano yanayo fanyika ndani ya ukumbi kuombewa kibali, usipofanya hivyo utatulazimisha tuamini kuwa hili jambo Jeshi letu si lao bali lako wewe rais wangu, hasahasa tukizingatia waathirika wa utaratibu huu ni wapinzani wako kisiasa.
* Rais wangu vurugu na machafuko husababishwa zaidi na kitendo cha watu kuzuiwa kusema ya moyoni, ukilinganisha na kitendo cha kuwaruhusu. Waache watu wakutane, waseme sanaaa, jioni kila mtu aenda kwake kulala.
Waachwe waseme, Ili mradi tu maneno yao yasiwe yale kuhamasisha vurugu, migomo, au kufanya uasi dhidi ya serikali yetu ikiyochaguliwa kihalali. Naomba ulifanyie kazi hili ili tupate kuamini ile kauli yako kuwa
"mimi nitakuwa rais wa watu wote, CCM wangu, CHADEMA wangu, ACT wangu, TLP wangu, ..." ULIITOLEA MOYONI NA SI MDOMONI.
Rais wangu naomba niishie hapa.
Kalamu naomba koma, sinitie gerezani,
Karatasi soma zama, hizi sio za zamani,
Ewe wino fanya hima, wangojea kitu gani?
Hapa sasa kaditama, penye kosa samahani,
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
whatspp/call 0622845394 Morogoro.