Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, sio lazima apendwe na kila mtu — hiyo ni kawaida katika uongozi. Lakini ni LAZIMA aheshimiwe na kila raia bila kujali tofauti za kisiasa, kiimani au mitazamo ya kijamii.
Kuongezeka kwa lugha za matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya viongozi mitandaoni siyo tu kwamba ni ukiukwaji wa maadili bali pia ni kuvunja misingi ya nidhamu na ustaarabu wa kitaifa.
Tujifunze:
- Kukosoa kwa hoja, si kwa matusi.
- Kutoa mapendekezo, si kubeza kila jambo.
- Kuelimisha, si kuchochea.
Tanzania ni yetu sote. Ustaarabu, maadili na heshima kwa viongozi wetu ni tunu ambazo lazima tuzilinde.
Tuijenge nchi kwa hoja zenye tija — si matusi mitandaoni.
✳️
Tanzania kwanza, tofauti baadaye.
Matusi yalianzia Pwani .
Zamani ilikua ni jambo la ajabu sana kumkuta mtu wa Bara akitukana au kusema matusi ya nguoni .Hayo mambo tuliyakuta kwa Waswahili hasa Wazanzibari na Wataramo .
Kwa hiyo matusi ni kibwagizo kwa waswahili na Wazanzibari.
Usiogope mtawala kutukanwa kinachotakiwa ni kutenda haki tu.
Unajua hata mwanaume au mwanamke akianza kutembea na watoto wadogo atadharaulika na kupoteza heshima yake mbele ya watu wa umri wote .
Sasa ukiona rais anatukana anachukiwa anasemwa vibaya usiangalie taasisi nzima bali anza kuangalia tabia yake katika kuongoza ,uadilifu wake , utu wake kwa wengine , upendo wake ,upendeleo ,dharau aliyo nayo ,kujikweza , kujiona yuko sawa na Mungu , kutaka kuheshimika yeye tu bila kuwaheshimu wengne ,kutaka kuhuurumiwa yeye tu bila kuwahurumia wengine .Mfano anaona fahari sana kuona jinsi Tundu Lisu anavyoteseka gerezani bila kosa wakati ni mgonjwa . Kumbe angesema tu tena hadaharani kuwa DPP anagalia huyo mtu ni mgonjwa mtoe utafute ushahidi mwingine . Angaheshimika sana kama mwanzoni alivyoheshimika na kupokelewa kwa shangwe kubwa sana na wapenda haki wote duniani pale alipoanza vizuri na kuwa na nia ya kubadli katiba na reforms nyingne ili nchi iwe na haki . Aliwahi kuwambia polisi wanabambikia watu kesi na wanakamata watu wasio na hatia akijitokea mfano yeye mwenyewe.
Cha ajabu alipoambiwa kuwa hawa Polisi ndio wanaotusaidia kushinda kwa nguvu akabadilika sana . Hapo hakujua kuwa kwa alivyoanza kama angefanikiwa kuleta mabadiliko angajijengea heshima kubwa sana na angepata ushindi mkubwa sana maana wapinzani wangekosa agenda na Kanisa pamoja na wapigania haki za binadama wasingekua na jambo la kukosoa kuhusu mauaji ,utekaji na dhulma .
Urais ni taasisi lakini Rais ni Mtu mmoja kwa nafsi yake na maono na matamanio yake .
Ndio maana Urais unagombewa lakini Rais hagombewi .
Tanganika kwanza kama ilivyo Zanzbar kwanza