Rais Mwinyi akilonga kuhusu uchinjaji

Rais Mwinyi akilonga kuhusu uchinjaji

Akh! imegoma kufunguka kwa mchina!!!
 
mwinyi kaanza vizuri lakini baadaye amechanganya kati ya public policy na private policy suala la dini ni la mtu binafsi n private policy, yeyekm mtu ambaye alikuwa kiongozi wa nchi na anakula kodi ya watu wote ilibidi aongelee public policy ambayo haisemi lolote kuhusu masuala ya kuchinja. unasema usingependa kugawa watu huku ukivuta upande mmoja. i like him at least he took a stand although he maybe wrong rather than mr.dhaifu who is afraid to take a stand.
 
mwinyi kaanza vizuri lakini baadaye amechanganya kati ya public policy na private policy suala la dini ni la mtu binafsi n private policy, yeyekm mtu ambaye alikuwa kiongozi wa nchi na anakula kodi ya watu wote ilibidi aongelee public policy ambayo haisemi lolote kuhusu masuala ya kuchinja. unasema usingependa kugawa watu huku ukivuta upande mmoja. i like him at least he took a stand although he maybe wrong rather than mr.dhaifu who is afraid to take a stand.

Wakati mwingine unapofanya analysis ya public policy lazima uzingatie factors nyinginezo ambazo jamii hiyo imezifuata au inazifuata kama vile utamaduni na dini. Vinginevyo kabla ya kuandaa policy husika ufanye "factor relaxing" kwa maana uitoe hiyo jamii katika hizo "other factors" kwanza au (you have to ignore other factors) kama ile ya ceteris paribus. Na hili ndilo tatizo kubwa la kutofanya kazi vizuri kwa public policy katika maeneo yenye hizi other factors (indigenous factors). Kwa mfano, kule nchi za Asia, wao kila kitu katika wanyama wanakula lakini hapa kwetu, mbwa paka ukilishwa hata kwa bahati mbaya utataabika kupita maelezo(hivyo iwapo unaandaa nutrition policy inayolenga kupanua wigo wa matumizi ya vyakula vunginevyo zaidi ya Wali na Ugali, bila shaka utaacha kujumuisha mbwa, nyani, paka nk. kama sehemu ya vyakula japokuwa wanyama hao ni rahisi kupatikana na matumizi yake yangelipunguza sana tatizo la chakula). Pia kwenye diversified communities kama hizi za kwetu athari hizo zinapatikana hata katika nyanja enginezo kwa mfano ukeketaji wa wanawake kwa baadhi ya makabila. Kama nilivyosema lazima utafute nyia nyingine ya kukiondoa kile kitu(kuutangazia umma kuwa ukeketaji ni kosa hivyo watu watachukuliwa hatua). Kwenye hili letu ni ngumu kuja na statement ya kuondoa tofauti za kidini (nonsectarian community). Ndiyo maana hata Mzee Ruksa amekuja kupata kigugumizi huku baadaye iweje sasa ikiwa jamii ziko hivyo. Ndipo akajikita zaidi kwenye kuvumiliana baina ya wakristo na waislamu. Mimi kwa maoni yangu nadhani suluhu yaweza kuwa katika namna 3 zifuatazo
1. Kuvumiliana kama alivyosema mzee Ruhksa
2. Machinjio yote ya umma yawe "electronically" naamini hili linawezekana kwani hata kule Saudia wakati wa hija wale kondoo hawachinjwi "individual"
3. Ipatikane tafsiri sahihi ya kuchinja ili tuone kama iko-"specific" na nini hasa. Nasema hivi kwa kuwa sidhani kama tuna tafsiri sahihi ya kuchinja hasa ni kukata kichwa, kusudio la kukata kichwa, maombi, nia au sababu za kuchinja au nni? Pindi tukipata tafsiri hii, tunaweza kuwa na wachinjaji ambao wana utaalamu wa kuchinja bila kuangalia dini zao (kwanini). Binafsi ni muislamu lakini naamini wanaojishughulisha na uchinjaji kwenye maeneo mbalimbali nchini(lets say ni waislam) wameingia huko "by chance" wala si kwa ueledi wao wa kusoma dua, au misikiti imewapeleka specially kwa ajili ya kuchinja au vyovyote(niko tayari kukosolewa hapa kama siko sahihi) kwani huenda wengine hawajui hata huko kusoma hizo dua(ila nia yao ni kuchinja watu wale na wanakula). Hivyo wataalam tunaomba maana na tafsiri ya kuchinja.
 
Huyu ameonyesha uthubutu ingawa amechanganya mambo. Suala hili bado ni gumu. Hakuna dini inayoruhusu kula vibudu, mnyama ni lazima achinjwe.
 
jamani sheria ya nchi inasemaje kuhusu kuchinja ?? sheria ya nchi haina dharura wala au dini fulani full stop. mwislamu akileta mtazamo wake kwenye suala fulani naye mkristo akatafasili kitu hicho kwa dini yake tutafika kweli ???tufuate sheria ya nchi full stop.
 
"In Zibah-e-Iztiraari, the animal may be severed (cut) anywhere on the body by being stabbed or cut by the sharp edge of the weapon causing its death. If a trained dog or hunting bird causes such injury to the animals being hunted, thus causing its death, then such an animal is Halaal. "

Kumbe hata kilichouwawa na mbwa ni halaal! Duh!
 
jamani sheria ya nchi inasemaje kuhusu kuchinja ?? sheria ya nchi haina dharura wala au dini fulani full stop. mwislamu akileta mtazamo wake kwenye suala fulani naye mkristo akatafasili kitu hicho kwa dini yake tutafika kweli ???tufuate sheria ya nchi full stop.

Exactly! Hiyo ndio njia sahihi ya kupata muafaka. Hizi tantarira za "tangu zamani walikuwa wanachinja watu fulani" ambazo hata jana niliona baadhi ya wabunge wakiziendekeza hazina nafasi tena. Sheria za nchi zifuatwe kwa ukamilifu wake - full stop.

Waislamu, wakristo, dini zote na wananchi wote kwa ujumla waambiwe kila mmoja ana haki ya kuchinja na hakuna mwenye hodhi ya hili suala. Wasitake kutafuta kura za hawa jamaa kwa ghiliba za kijinga kama hizi.
 
Huyu ameonyesha uthubutu ingawa amechanganya mambo. Suala hili bado ni gumu. Hakuna dini inayoruhusu kula vibudu, mnyama ni lazima achinjwe.

Kama alivyosema mchangiaji #5 , kuna haja ya kupata trafsiri sahihi ya neno kuchinja maana kwa tafsiri aliyoitoa Mzee Ruksa si sahihi. Huwezi kuwa kama mnyama ambaye hakujichinjwa na mwislam ni mzoga. Mnyama aliyechinjwa na mkristo siyo mzoga kwa tafsiri hasa ya neno mzoga wala hakuna mkristo anayekula mzoga.

Hili tatizo liliibuka baada ya waislam kudai kuwa kuchinja ni sehemu ya ibaada yao kufuatana na imani yao ndo maana wakristo wakasema wasingependa kushiriki hiyo ibaada ya kiislam. Kwa maana hiyo na wao inabidi wachinje wenyewe ili wasishiriki ibaada ya kiislam.

Kwa maana hiyo neno "kuchinja na mzoga" linavyotumiwa na waislam si sahihi.
 
Wakati mwingine unapofanya analysis ya public policy lazima uzingatie factors nyinginezo ambazo jamii hiyo imezifuata au inazifuata kama vile utamaduni na dini. Vinginevyo kabla ya kuandaa policy husika ufanye "factor relaxing" kwa maana uitoe hiyo jamii katika hizo "other factors" kwanza au (you have to ignore other factors) kama ile ya ceteris paribus. Binafsi ni muislamu lakini naamini wanaojishughulisha na uchinjaji kwenye maeneo mbalimbali nchini(lets say ni waislam) wameingia huko "by chance" wala si kwa ueledi wao wa kusoma dua, au misikiti imewapeleka specially kwa ajili ya kuchinja au vyovyote(niko tayari kukosolewa hapa kama siko sahihi) kwani huenda wengine hawajui hata huko kusoma hizo dua(ila nia yao ni kuchinja watu wale na wanakula). Hivyo wataalam tunaomba maana na tafsiri ya kuchinja.
Mkuu upo sahihi kabisa. Nadnani suala hili limechanganywa na wanasiasa, kwa kuwa kimsingi halina mantiki. Nijuavyo mimi, hakuna dini inayopeleka mtu kuwa mchinjaji, lakini mwenye kitoweo humwita awaye-yeyote ilmradi anajina la kiislam kuja kuchinja. Haijulikani endapo wachinjaji ni waislam safi au ni kwa ajili ya jina, ama wamesomea elimu ya uchinjaji. Bila shaka suala hili lingekuwa dogo kama wanasiasa wangewaachia viongozi wa dini, badala ya wao kutoa matamko ambayo hayatetewi na sheria zilizopo.
 
Endeleeni kujadiliana kuhusu kuchinja.sie huku twapanga jinsi ya kuanza wapatia standard 1 laptop.Mkihamia pande hii sisi tutaenda mbali zaidi.
 
Naona alikua anajisafisha baada ya kauli yake ya awali kuwachukiza waislam, huenda amehofia kupigwa vibao.
 
Endeleeni kujadiliana kuhusu kuchinja.sie huku twapanga jinsi ya kuanza wapatia standard 1 laptop.Mkihamia pande hii sisi tutaenda mbali zaidi.

Halafu watachomeka waya matakon.ni kuchaji, na wakirudi nyumbani wataikatakata vipande vipande hiyo laptop na kuila ili waweze kupata nguvu ya kufanya homework maanake njaa nyao, duh!
 
Mimi natoka kijijini. Kwet huku uislamu haupo na wala sijaona msikiti hata mmoja. Waislami walionekana kwa wingiu mwambao wa pwani, Tabora, Bukoba, Kigoma. Ni katika miaka hii ya karibuni baada ya Uislamu kuingia katika maeneo mengi nchini. Je huko nyuma kabla ya kelele hizi za kuchinja, tulikuwa tunakula nyama gani.. na nani ana chinja. Tatizo lingine ambalo nadhani vionghozi wetu hawalioni kuwa ukichinja kwa kufanya baiashara yaani kuuza hiyo nyama basi lazima ifanywe na mwislamu. kwa mana hiyo unamfanya mwislamu ndie afanye biashara ya bucha na mkristo au mpagani au mhindu wasiwe wafanyabiasha hiyo. Mgogo wa Dodoma ambae si muislamu asiuze nyama aliyochinja!! MMasai au ------ asiuze nyama hadharani. Hiyo si sawa. Viongozi wetu watafakari hili jambo kabla hawajajibu au kiuzungumza. Kuchinja kwa lengo la kuuza isiwe prerogative ya dini. Nbona miaka ya nyuma hatukusikia haya.. sasa kuna nini hata kelele hizi zipigwe!!
 
Kama ilivyo ngumu kutokana na imani yake Muislam kuweza kuingia Kanisani na kufanyia Ibada yake humo na kama ilivyo ngumu kwa Mkristo kuingia Msikitini na kuweza kufanyia ibada yake humo IKIZINGATIWA NI SUALA LA IMANI basi na kuchinja kuheshimiwe kama suala la imani kwa kila dini kati ya hizi dini mbili. Muislam kwa kuwa achinjapo sharti awe amemuelekeza mnyama yule huko KIBLA basi achinje na ALE kwa IMANI YAKE. Na Mkristo naye na ACHINJE KWA MKONO WAKE NA ALE KULINGANA NA IMANI YAKE. Mkristo kulazimishwa kula alichochinja Muislam kulingana na imani yake ni sawa na kumlazimisha Mkristo yule kuingia Msikitini kufanyia ibada za Kikristo kitu ambacho hakiwezekani, vivyo hivyo kwa Muislam.

Kama Muislam asivyoweza kumchinjia Mkristo nguruwe akala na iwe pia kwa wanyama wengine.
Tanzania bila UDINI inawezekana, tekeleza wajibu wake kulinda amani yetu na dumisha mapendo.
 
Halafu watachomeka waya matakon.ni kuchaji, na wakirudi nyumbani wataikatakata vipande vipande hiyo laptop na kuila ili waweze kupata nguvu ya kufanya homework maanake njaa nyao, duh!
I guess you had severe birth asphyxia, which was later complicated by Kernicterus.Endelea kugombania kuchinja.This is the only way you can survive in east african federation
 
Hii nchi ina laana si bure. Haiwezekani watu woooote wanaoamka kuzungumza wazunguuuke halafu warudi pale pale kwenye 'TOKEA ZAMANI'. Hivi ni mambo mangapi yanafanywa leo lakini hapo zamani hayakukuwepo?

1. Hapo zamani wanawake walikuwa wakikeketwa, je turudie zamani ili tusilete migogoro na wale wanaoamini kwenye ukeketaji wa wanawake?
2. Hapo zamani huduma za usafiri zilitolewa na UDA na KAMATA tu, je turudie zamani kwa kuwa daladala hazikuwepo?
3. Hapo zamani polisi hawakuwa wakifanya doria na silaha za moto mitaani, walikuwapo mgambo na virungu vyao na ukikamatwa nao unapelekwa ZONE. Je turudie zamani kwa kuwa bunduki zinaogofya?

Tuache huu ujinga wa 'tangu zamani'. Ni watu PRIMITIVE ndio huishi kwa mazoea badala ya fikra pevu zinazoendana na wakati. Hapo zamani, hakukuwa na nchi iliyokuwa na katiba. Watu wote waliishi primitive life na social conduct ilikuwa inasimamiwa na mazoea ya jamii ya watu husika.

Ongezeko la watu na scarcity ya resources ndio iliyoleta katiba miongoni mwa jamii mbali mbali. Katiba imekuja ili kuondoa mikwaruzano kama hii. Sasa linapokuja suala kama hili halafu ananyanyuka mtu mzima na akili zake na kusema 'kwani tangu zamani ilikuwa vipi' huyo mtu anakwenda mbele au anarudi nyuma? Tena mbaya kiongozi wa nchi ambaye anapaswa kuwa wa mbele kuelezea umuhimu wa utawala wa sheria, badala yake analeta MAZOEA.

Kila mtu ana imani yake na sioni sababu ya watu wa imani mojawapo kuwa na kiherehere cha kujifanya wao ndio wana haki ya kuwaamulia wengine wale kitu cha namna gani. Na kwa nini Waislam wawe wenye kuleta mitafaruku kila kukicha, kwani nchi hii ina Waislam na Wakristo tu?

Wahindu traditionally hawali NG'OMBE, je na wao waingie mitaani kupinga ng'ombe kuchinjwa?

Watanzania tutumie akili zetu. Kila kitu kina turning point. Mtoto mdogo wa kiume hulala na mama yake kwa umri fulani, lkn anapokuwa mkubwa, hilo hukoma. Je, mama mtoto akiomba nafasi zaidi kwa mtoto huyo kulala tutamwambia 'kwani siku zote alikuwa analala wapi?'

Kiherehere kiachwe. Naamini hata hiyo dini yenu imewaamuru kutokula 'mnachoita kibudu', lkn haikuwaambia muhakikishe watu wote hawali. Mimi hata sielewi haki hiyo mnaipata kwa wajibu upi.
 
Mzee Mwinyi nakupa Hongera kwa sababu unaonyesha Njia, unaonyesha njia ambayo wengine wanashindwa kuiona; Njia ambayo Mwalimu Nyerere na waasisi wengine kama kina karume wameitengeneza ili Watanzania wote waipite bila kupata misukosuko ya ajabu. Mzee Mwinyi ulipokuwa unaongea na waandishi wa habari nilikuona kama Nabii aliyebaki katika Dunia hii ili kuionyesha Tanzania nyia impasayo Kwenda. Njia inayowaelekeza Watanzania kuwa wao ni ndugu wasiopaswa kugombana kwa kuwa wanaipigania dini zao. Na Kimsingi nakukubali Mzee kwa sababu ni wewe peke yako uliyethubutu kulisemea swala la kuchinja vitoweo. Wengine wote wamekwepa ukweli ulipo. Mungu akubariki Mzee ili tuendelee kuwa nawe kwani wewe ni hazina ya nchi hii, wewe ni chemi chemi ya busara ambayo tunahitajika kuendelea kuteka maji ya busara.

Nawasilisha


Olowarukerikeri
 
Unajua hata hawa viongozi wetu hawaelewi chanzo cha matatizo yote na kuchinja kwa waislam na wakristo ni nini!
Shida inaanzia pale ambapo waislam wanasema kuchinja kwao ni ibada!!!!!!! that means wanapochinja wanaendesha ibada ya kiislam!!!! sasa ni mkristo gani yupo tayari kushirikishwa kwenye ibada ya kiislam asiyo iamini???!!!! hapa ndipo wakristo walipoanza kudai haki ya kuchinja wanyama wao wenyewe na hata kuwa na mabucha yao wenyewe. ukimuuliza kweli muislam yeyote atakuambia kuchinja ni ibada kwao

Hili suala linahitaji busara ya hali ya juu sana kulitatua na sio kukurupuka tuu usingizini na kuropoka hovyo otherwise muafaka hauwezi kufikiwa kirahisi rahisi tu kwamba kwa vile waislamu walizoeleka kwamba ndio wanachinja basi waachwe na wachinje!!!!!!! je kwa wenzetu wenye mchanganyiko wa dini kama sisi wanafanya hivyo??!!!!
 
Unajua hata hawa viongozi wetu hawaelewi chanzo cha matatizo yote na kuchinja kwa waislam na wakristo ni nini!
Shida inaanzia pale ambapo waislam wanasema kuchinja kwao ni ibada!!!!!!! that means wanapochinja wanaendesha ibada ya kiislam!!!! sasa ni mkristo gani yupo tayari kushirikishwa kwenye ibada ya kiislam asiyo iamini???!!!! hapa ndipo wakristo walipoanza kudai haki ya kuchinja wanyama wao wenyewe na hata kuwa na mabucha yao wenyewe. ukimuuliza kweli muislam yeyote atakuambia kuchinja ni ibada kwao

Hili suala linahitaji busara ya hali ya juu sana kulitatua na sio kukurupuka tuu usingizini na kuropoka hovyo otherwise muafaka hauwezi kufikiwa kirahisi rahisi tu kwamba kwa vile waislamu walizoeleka kwamba ndio wanachinja basi waachwe na wachinje!!!!!!! je kwa wenzetu wenye mchanganyiko wa dini kama sisi wanafanya hivyo??!!!!
 
Back
Top Bottom