mwelimishaji
Member
- Oct 5, 2010
- 51
- 10
Mzee Mwinyi nakupa Hongera kwa sababu unaonyesha Njia, unaonyesha njia ambayo wengine wanashindwa kuiona; Njia ambayo Mwalimu Nyerere na waasisi wengine kama kina karume wameitengeneza ili Watanzania wote waipite bila kupata misukosuko ya ajabu. Mzee Mwinyi ulipokuwa unaongea na waandishi wa habari nilikuona kama Nabii aliyebaki katika Dunia hii ili kuionyesha Tanzania nyia impasayo Kwenda. Njia inayowaelekeza Watanzania kuwa wao ni ndugu wasiopaswa kugombana kwa kuwa wanaipigania dini zao. Na Kimsingi nakukubali Mzee kwa sababu ni wewe peke yako uliyethubutu kulisemea swala la kuchinja vitoweo. Wengine wote wamekwepa ukweli ulipo. Mungu akubariki Mzee ili tuendelee kuwa nawe kwani wewe ni hazina ya nchi hii, wewe ni chemi chemi ya busara ambayo tunahitajika kuendelea kuteka maji ya busara.
Nawasilisha
Olowarukerikeri
Ni kweli Bwana Olawaru kerikeri pongezi zako kwa mzee Mwinyi ni sawa. Suala la imani ni la watu wanaohusika na imani hiyo na wasiohusika nayo hawalazimiki kuifuata wala kuwazuia wahusika kuifuata imani yao. tukisema mifugo yote ichinjwe na wenye imani fulani italazimu hao wachijnaji wawe na kazi hiyo tu kwani ng'ombe wa kuchinjwa ni wengi, kuku ni wengi, nguruwe ni wengi, bata, mbuzi,....Kwa kweli kipato watakachopata kutokana na kazi hiyo hakitatosha kukidhi mahitaji yao, watahitaji kufanya kazi zingine. Msisahau kazi ya kuchinja pia yahitaji ujasiri wa aina yake.