Rais Museveni atembelea kituo cha reli ya kisasa SGR Dar es salaam, ammwagia sifa Rais Samia na hayati Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,932
141,894
Rais Yoweri Museveni leo ametembelea kituo cha reli ya kisasa ( SGR) jijini Dar es salaam na kuwamwagia sifa Rais Magufuli na mrithi wake mh Samia kwa ujasiri mkubwa wa kubuni mradi huo.

SGR itaendeshwa na umeme wa bwawa la Nyerere ambalo ni baraka za kipekee kutoka kwa Mungu wa mbinguni.

Tukio liko mubashara TBC na Channel ten.
 
Rais Yoweri Museveni leo ametembelea kituo cha reli ya kisasa ( SGR) jijini Dar es salaam na kuwamwagia sifa Rais Magufuli na mrithi wake mh Samia kwa ujasiri mkubwa wa kubuni mradi huo...
Mleta mada weka sawa maelezo yako, SGR haijulikani ni lini itakamilika au kuanza kazi (tuliambia ingeanza kufanya kazi 2019 kwa kipande cha Dar-Moro wakati huo Bwawa la Nyerere ndio lilikuwa linaanza kujengwa) na bwawa la Nyerere halijulikani kama litakamilika au kukamilika lini.

Ni vyema kuitofautisha hii miradi kuliko kuichanganya ili kuwa na focus.
 
Mtoa mada labda unaishi zama za kale,pls tembelea wewe mwenyewe huu mradi wa SGR halafu ndio ulete mada zenye FACTS ndani yake!na lile bomba la mafuta mpaka bandaribya tanga umeishia wapi ule mradi?President M7 anashangaa why mizigo ya Uganda kupitia bandari ya Dar ni tani chache mno na hajui mizigo mingine ya nchi yake inapitia bandari gani!!!
 
Yoweri!
 
Kwa kweli mimi Yoweri simuelewi hata kidogo, mara nyingi amekua akimtaja Nyerere binafsi nachukulia kama role model wake, ana muheshimu sana lakini anachofanya nchini mwake ni tofauti na mitazamo ya Nyerere kama kuendelea kushikilia madaraka kwa muda mrefu wkt umri umemtupa mkono na sometimes kua na kauli tata. Kwamba yeye ni kota pini inaingia kwa nyundo na itatoka kwa nyundo kama ilivyoingia.
 
Back
Top Bottom