Rais Museveni asema hana haraka ya kustaafu

Hearten

Hearten

Member
Joined
May 17, 2016
Messages
45
Points
125
Hearten

Hearten

Member
Joined May 17, 2016
45 125
proxy-duckduckgo-com-jpg.1191700

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hana haraka ya kustaafu, na wala hana mpango wa kumwandaa mtu yeyote kurithi nafasi yake na badala yake anazingatia kuimarisha ukuaji wa Uganda na bara la Afrika kwa jumla.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hana haraka ya kustaafu, na wala hana mpango wa kumwandaa mtu yeyote kurithi nafasi yake na badala yake anazingatia kuimarisha ukuaji wa Uganda na bara la Afrika kwa jumla.

Katika mawasiliano ya moja kwa moja na wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii wa facebook, Museveni amesema viongozi walio madarakani katika bara la Afrika, hawajaonyesha nia ya dhati kusuluhisha matatizo yanayolikumba bara hilo, na hivyo hawezi kuwa mwenye amani endapo atastaafu hii leo.

Museveni awasiliano na wafuasi wake kwa facebook akiwa katika ndege

Wakati alikuwa safarini kutoka Uganda hadi Yokohama, Japan, rais wa Uganda Yowweri Museveni alitumia mda huo kuwasiliana na wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii, anaowaita kuwa wajukuu wake.

Wajukuu walimuuliza Museveni maswali mengi kuhusu hali ya Uganda, yanayowakera na yanayowafurahisha, wakiangazia maswala ya demokrasia, uchumi, na hali yao ya maisha.

Vijana waahidi Museveni kumfanya baba wa taifa

Lakini lililoangaziwa Zaidi ni kuhusu utawala wa miaka 33 wa Museveni ambao wajukuu wake wanasema, umetosha, na anastahili kustaafu ili kuwaachia vijana kuongoza nchi.

Wafuasi wa museveni kwenye mtandao wa kijamii wa facebook, wanamtaka astaafu na awe mshauri, wakipendekeza kwamba mbunge Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, awe mrithi wake, wakiahidi kumtambua Museveni kama baba wa taifa na kumpa heshima za kitaifa.

Lakini Museveni, amechukua mda mrefu kujibu hoja hiyo akisema hana mipango ya kustaafu kwa sasa wala kumwandaa mrithi wake.

Museveni amesema ana kazi nyingi sana iliyosalia kwake kutimiza kwa manufaa ya Uganda, jumuiya ya Afrika mashariki, Maziwa makuu na bara la Afrika kwa jumla.

Maoni ya wachambuzi

Wachambuzi kama Francis Babu, wanasema Museveni ametuma ujumbe kwamba si wakuondoka madarakani kwa sasa.

“kitu kimoja nimeona Uganda ni kwamba kila mtu anataka awe rais, jambo ambalo haliwezikani. Museveni naye anataka aendelee kuwa pale. Sasa, inategemea na chama chake. Kama chama kinataka aendelee kuwa rais, sasa ni jukumu la wapiga kura kuamua” amesema Francis Babu.

Vile vile, Museveni mwenye umri wa miaka 75, anataka vijana, akiwemo Bobi Wine, kumuunga mkono katika ndoto yake kubwa ya kuhakikisha bara la Afrika lililoendelea kabisa kiuchumi katika siku za usoni.

Museveni amesisitiza kwamba Uganda na bara la Afrika kwa jumla, halina mtu mwenye uwezo wa kutimiza ndoto kubwa aliyo nayo, ya kuimarisha maendeleo ya uchumi, demokrasia na maisha bora kwa kila mtu. Lakini Samuel Kisitu, mchambuzi wa siasa za Uganda, ana mtazamo tofauti.

“Rais Museveni ni mtu ambaye hamwamini mtu yeyote kabisa hata ukiangalia wale ambao amefanya nao kazi, kuna jinsi anawashusha heshima na kuwadhalilisha waonekana kama watu ambao hawana uwezo wa kuongoza nchi na kila kinachofanyika ni juhudi zake pekee yake. Hii ndio sababu anasema kwamba ni yeye pekee ana maono ya nchi, jumuiya ya Afrika mashariki na hata Afrika nzima” ameeleza Kisitu.

Kitendawili cha Museveni kustaafu

Museveni, ameahirisha ahadi yake ya kustaafu mara kadhaa katika kipindi cha miaka 33 iliyopita ambayo amekuwa madarakani.
Katika chaguzi za 1995, 2001 na 2006, Museveni aliahidi kwamba angestaafu, lakini kila mara baada ya kuchaguliwa, huanza mchakato mpya kuondoa vizuizi vinaweza kumzuia kugombea mhula mwingine tena.

Kizuizi kilichokuwa kimesalia ni cha umri kwa wagombea wa urais, ambapo katiba ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2017 na kuondoa kifungo hicho.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.
 
Thad

Thad

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Messages
11,903
Points
2,000
Thad

Thad

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2017
11,903 2,000
Walau huyu mzee hajaminya uhuru wa kuongea, watu wako huru kutoa maoni yao tofauti na kwa bwana mkubwa ambako ukiinua mdomo tu unafunguliwa kesi ya uchochezi!
 
mtu chake

mtu chake

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
15,696
Points
2,000
mtu chake

mtu chake

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
15,696 2,000
Walau huyu mzee hajaminya uhuru wa kuongea, watu wako huru kutoa maoni yao tofauti na kwa bwana mkubwa ambako ukiinua mdomo tu unafunguliwa kesi ya uchochezi!
Ni kweli Uganda wako huru kiasi ,nilikuwepo kule kipindi mjukuu anamsumbua babu , tatizo Babu hataki MTU aguse kiti chake
 
Ulimbo

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Messages
2,067
Points
2,000
Ulimbo

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2009
2,067 2,000
Huyo anataka kufia Ikulu. Mugabe mwenyewe walipoona wameshamnyojya vya kutosha, walimsogeza pembeni itakuwa yeye?
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
453
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
453 500
Miaka 33bado hajafanya wala kuona afrika haijakua,anawaponda wezake kwamba hawataki kujishughulisha ili afrik nauganda ikue.du
 
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
17,636
Points
2,000
Kennedy

Kennedy

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
17,636 2,000
Akistaafu Atafanya Kazi Gani? Atamani Tu Raha
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
33,786
Points
2,000
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
33,786 2,000
Kota pini kwenye baiskeli inaingizwa kwa nyundo na kutolewa kwa nyundo
Hii kota pin ikisuguka itaanza kupwaya yenyewe na kuchomoka.

Ili kuepuka usumbufu pindi itakapoponyoka ni vizuri itolewe kwa nyundo ili iwekwe nyingine mpya na imara zaidi.
 
King_mwanamalundi

King_mwanamalundi

Member
Joined
Mar 27, 2019
Messages
13
Points
45
King_mwanamalundi

King_mwanamalundi

Member
Joined Mar 27, 2019
13 45
Ndio maana huwa namwelewa saana Mtukutu Trump,
Huko kwao wakianza kuijadili namna ya kuisaidia Africa yeye hutoka nje kunywa kahawa mpaka wamalize.
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
4,964
Points
2,000
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
4,964 2,000
Huyu mwamba unaweza kumwita Jasusi Kachecho mbobezi Yower Kaguta Museveni....... Hawa dawa yao ni Drone tu...
 
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
8,511
Points
2,000
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
8,511 2,000
Muacheni jamani mzee wetu, tunamuhitaji sana EAC. He is now a symbol of unity. Akiondoka inawezekana EAC isiwe kama ilivyo sasa.
 

Forum statistics

Threads 1,334,886
Members 512,157
Posts 32,489,890
Top