Rais Mugufuli atakumbukwa na vizazi vingi wa Watanzania

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Waswahili husema, "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni".
Ni ukweli ulio wazi Sasa kuwa Rais Magufuli atakumbukwa na watanzania katika vizazi vingi vijanyo.
Kipindi chake cha uongozi kimekuwa na mambo mengi makubwa ambayo kiukweli yalihitaji ujasiri mkubwa kuyafanya.

Hakika Magufuli ni mtu mwenye uthubutu hata Kama akifeli baadhi ya mambo lakini watanzania wataiona nia yake njema.

Huu mkataba wa madini kusainiwa kwa mara ya kwanza Tanzania itanufaika na raslimali yake ya madini, hii inamfanya Magufuli kuingie kwenye vitabu vya kumbukumbu vya taifa hili hasa mtu atakapogusa nyanja ya madini. Huu ni ukweli ulio wazi japo Wana siasa wengi watapinga hili.
Vitosho na maneno mengi ya kukatisha tamaa mara kushitakiwa Miga n.k , laikini alisimamia msimamo wake hadi leo matokeo tumeyaona.

Itakapo tajwa kampuni mpya ya TWIGA moja kwa moja utamtaja Magufuli, ukitaja mabadiliko ya sheria za madini hapo lazima utamtaja Magufuli, chimbuko la mawazo ya kuanzishwa vitu hivi vyote ni yeye.

Hebu tuseme ukweli.
1; Wana Mwanza itawachukua miaka mingapi kumsahau Magufuli kwa uwepo la daraja la BUSISI? Waliwahi kuota kuwa wangekuwa na kitu Kama hiki?
Ujenzi wa Meli tano ziwa Victoria itawachukua miaka mingapi hadi kusahau.

2; Itatuchukua miaka mingapi hadi kusahau Tren ya Umeme SGR!!
Kila atakae iona hata Kama ni miaka 70 baadae jina la Magufuli litamjia kichwani.

3; Wananchi wa kigoma watamsahau vipi Magufuli kwa ujenzi wa mabarabara yanayounganisha mkoa wa kigoma na mikoa jirani, mkoa ambao Kama vile ulikuwa umesahaulika kabisa.

4; Tutakapoanza kutumia Umeme kutoka Bwawa la Nyerere tutamsahau vipi Magufuli watanzania.?

5; Utakapoona ndege za ATCL zikipasua anga atamsahau vipi Magufuli?

Hakika huyu ni shujaa wa taifa hili, wanasiasa watakataa kwasababu nawao pia wanahitaji kushika dola hivyo usitegemee kuwa watamuunga mkono Magufuli hata mara moja.
Lakini vitu anavyo vifanya vinajieleza.

Prof Lumumba hakuwa mnafiki aliposema " the Magufulification of Africa."

Licha ya mapungufu yake kiuongozi lakini hakika huyu ni kiongozi wa mfano wa kuingwa barani Africa.
 
Mods naomba mnirekebishie heading hapo "ATAKUMBUKWA" badala ya Atakumbwa, "VYA" badala ya WA.
 
Tumeliwa trilion 495 hivi hivi na zimezikwa rasmi leo!Pia mchanga wameambiwa wakauze!Shamba la bibi ni shamba la bibi tu!
Kama si uthubutu wake hiyo tril 495 ungeijulia wapi? Ni wewe ndio ulitoa wazo la uchunguzi kufanyika??

Amesema mchanga uliopo bandarini utauzwa Sasa chini ya usimamizi wa TWIGA acha kukurupuka mkuu.
 
Kweli "ATAKUMBWA" sana.
Waswahili husema, "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni".
Ni ukweli ulio wazi Sasa kuwa Rais Magufuli atakumbukwa na watanzania katika vizazi vingi vijanyo.
Kipindi chake cha uongozi kimekuwa na mambo mengi makubwa ambayo kiukweli yalihitaji ujasiri mkubwa kuyafanya.

Hakika Magufuli ni mtu mwenye uthubutu hata Kama akifeli baadhi ya mambo lakini watanzania wataiona nia yake njema.

Huu mkataba wa madini kusainiwa kwa mara ya kwanza Tanzania itanufaika na raslimali yake ya madini, hii inamfanya Magufuli kuingie kwenye vitabu vya kumbukumbu vya taifa hili hasa mtu atakapogusa nyanja ya madini. Huu ni ukweli ulio wazi japo Wana siasa wengi watapinga hili.
Vitosho na maneno mengi ya kukatisha tamaa mara kushitakiwa Miga n.k , laikini alisimamia msimamo wake hadi leo matokeo tumeyaona.

Itakapo tajwa kampuni mpya ya TWIGA moja kwa moja utamtaja Magufuli, ukitaja mabadiliko ya sheria za madini hapo lazima utamtaja Magufuli, chimbuko la mawazo ya kuanzishwa vitu hivi vyote ni yeye.

Hebu tuseme ukweli.
1; Wana Mwanza itawachukua miaka mingapi kumsahau Magufuli kwa uwepo la daraja la BUSISI? Waliwahi kuota kuwa wangekuwa na kitu Kama hiki?
Ujenzi wa Meli tano ziwa Victoria itawachukua miaka mingapi hadi kusahau.

2; Itatuchukua miaka mingapi hadi kusahau Tren ya Umeme SGR!!
Kila atakae iona hata Kama ni miaka 70 baadae jina la Magufuli litamjia kichwani.

3; Wananchi wa kigoma watamsahau vipi Magufuli kwa ujenzi wa mabarabara yanayounganisha mkoa wa kigoma na mikoa jirani, mkoa ambao Kama vile ulikuwa umesahaulika kabisa.

4; Tutakapoanza kutumia Umeme kutoka Bwawa la Nyerere tutamsahau vipi Magufuli watanzania.?

5; Utakapoona ndege za ATCL zikipasua anga atamsahau vipi Magufuli?

Hakika huyu ni shujaa wa taifa hili, wanasiasa watakataa kwasababu nawao pia wanahitaji kushika dola hivyo usitegemee kuwa watamuunga mkono Magufuli hata mara moja.
Lakini vitu anavyo vifanya vinajieleza.

Prof Lumumba hakuwa mnafiki aliposema " the Magufulification of Africa."

Licha ya mapungufu yake kiuongozi lakini hakika huyu ni kiongozi wa mfano wa kuingwa barani Africa.
 
Hatuongei ovyo mkuu, lete ushahidi wa unacho kisema.
Hiiiiiiiiiiiiii.
tapatalk_1496084922915-1.jpeg

dodge
 
Wewe ushahidi wa kuwa atakumbukwa uko wapi? Faida ya hivyo vitu haijaonekana,miradi mingine hata haijaanza,halafu wewe unasema atakumbukwa!! Kwa lipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ovyoo!! Haya atakumbukwa kwa ndege au nazo huzioni?? haya na wewe weka ushadi hapa kuwa ni yeye ndo alimpiga Tundu marisasi.
Huoni faida si ni kwasababu unajitoa ufahamu Kama huoni faida ya ujenzi wa miundombinu huoni Kama unatatizo kichwani.?
 
Back
Top Bottom