Rais Mugabe asema anarogwa

Rais Mugabe asema anarogwa

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
QAZ.jpg
​

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.

Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400- walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa "inayofaa" kufanya hivyo.

Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake.

Malumbano ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana kuendelea kudhoofika zaidi.

Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka.

Mwaka 2006 alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008. Licha ya hayo aligombea na kushinda katika uchaguzi uliokuwa na ghasia ambao matokeo yake yalibishaniwa.

Kwa hivyo haijawa wazi ni lini , kama kweli Rais Mugabe ataondoka madarakani. Mnamo mwioshoni mwa juma kamati za kikanda za chama tawala cha, Zanu-PF provincial zilimuidhinisha kama mgombea wake katika uchaguzi wa 2018 , ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.

Chama hicho kitaidhinisha uamuzi huo katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi ujao. Kwa hiyo kwa sasa haionekani kama kweli anaangalia uwezekano wa kustaafu.

Chanzo: BBC
 
Miaka 92 anarogwa au anajiroga .....

Only in Black Continent .....
 
Du inaonekana uzee tu huo hata Seifu Sharifu nae umri umekwenda anasema anataka kuuliwa ama kweli wazee hawataki wafe vijana wao wanataka wafe kwani kutwa viroba na t 1 na mambo kadhaa ambayo vijana vinawaondoa dunia
 
Akiongea kwenye halaiki ya watu 400 Rais Mugabe amesema ndani ya chama chake Cha Zanu Pf kuna watu wanamloga na wengine wakimwombewa kifo.

Asema hayo yote yanafanyika ili asiweze kugombea Nafasi ya Urais 2018 ambapo atakua na Jumla ya Miaka 94 hata hivyo chama chake tiyari kimempitisha kama mgombea wa chaguzi huo ujao.

Je kuna haja ya kiongozi Mkubwa kama Rais Mugabe kuamini vitu kama Ivyo?
 
Hakuna haja. Lakini inategemea hulka za watu wa Zimbabwe kama wamebobea kwenye ushirikina.

Mugabe amefika mwisho ktk kufikiri na wala nchi yake haiwezi ku gain chochote kutoka kwake kwa hali ya sasa.
 
Kuna audio na video ya yeye akisema hivyo?

Manake huyo mzee amekuwa akizushiwa maneno mengi mno.
 
Lumumba fc muda siyo mrefu watafika hapa, na kusema kuwa huyo ni Lema
 
Hakuna haja. Lakini inategemea hulka za watu wa Zimbabwe kama wamebobea kwenye ushirikina.

Mugabe amefika mwisho ktk kufikiri na wala nchi yake haiwezi ku gain chochote kutoka kwake kwa hali ya sasa.
Kama Morgani Tsangirai alishindwa kuingia madarakani wamwache tu mzee Mpaka amue mwenyewe sasa

Na sidhani kama kuna haja ya uchaguzi wamwache tuu
 
... Asema hayo yote yanafanyika ili asiweze kugombea Nafasi ya Urais 2018 ambapo atakua na Jumla ya Miaka 94 hata hivyo chama chake tiyari kimempitisha kama mgombea wa chaguzi huo ujao ...
US-Zim Presidents.jpg
 
Akiongea kwenye halaiki ya watu 400 Rais Mugabe amesema ndani ya chama chake Cha Zanu Pf kuna watu wanamloga na wengine wakimwombewa kifo.

Asema hayo yote yanafanyika ili asiweze kugombea Nafasi ya Urais 2018 ambapo atakua na Jumla ya Miaka 94 hata hivyo chama chake tiyari kimempitisha kama mgombea wa chaguzi huo ujao.

Je kuna haja ya kiongozi Mkubwa kama Rais Mugabe kuamini vitu kama Ivyo?
Mbona kufuli anasema tumwombee??
 
Back
Top Bottom