dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483

Rais Mteule wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuapishwa alhamisi asubuhi ambapo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Othman Makungu atamuapisha katika sherehe zitakazofanyika uwanja wa Amani.
Kwa mujibu wa Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya sherehe ya kitaifa amesema maandalizi yanaendelea vizuri ambapo ametembelea uwanja wa Amani na kushuhudia harakati za sherehe hizo ambazo zitashirikisha vikosi vya ulinzi na usalama huku Balozi akiwataka Wazanzibar kujitokeza kwa wingi kushuhudia kuapishwa kwa Dkt.Shein.
Balozi Seif Ali Iddi akizungumzia uchaguzi mkuu uliomalizika juzi amesema Serikali imeridhika na jinsi uchaguzi huo ulivyosimamiwa,kwa vile ulikuwa wa amani na amewataka wananchi kuacha fikra na mazungumzo yasiyo na tija na sasa kushughulika na kazi za maendeleo kwa vile uchaguzi umekwisha na Rais ameshapatikana pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Dkt.Shein ambaye ni Rais Mteule wa awamu ya saba anaapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kushinda uchaguzi wamarudio wa jumapili kwa ushindi wa asilimia 91.4 na kuwaacha wapinzani wake kwa kiwango kikubwa.
Chanzo: ITV