Rais mteule wa Gambia kuwaachilia wafungwa wa kisiasa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Rais mteule wa Gambia kuwaachilia wafungwa wa kisiasa

_92824518_barrow.jpg

Rais Mteule wa Gambia amekuwa akiongea juu ya anavyotazamia kubadilisha taifa tangu ashinde bila kutarajia juma lililopita.

Adama Barrow, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mfanyabiashara wa kujenga nyumba na kuuza, alimshinda Yahya Jammeh, aliyenyakua madaraka kwa mtutu wa bunduki na kutawala kwa miaka 22.

Makundi ya haki za binadamu yamemlaumu Bw Jammeh kwa ukiukaji wa haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja, waandishi wa habari na wanasiasa wa upinzani.

Rais Mteule wa Gambia amewahimiza watu waliotoroka Gambia kwa sababu ya hali ngumu ya maisha ya mtangulizi wake kurudi nyumbani ili kusaidia kujenga taifa lao.

Bwana Barrow aliambia shirika la habari la Associated Press kuwa atawaachilia kutoka gerezani wanasiasa wote wa upinzani walio gerezani.

Yeye pia alisisitiza kuwa atabadili msimamo wa awali wa Bw Jammeh wa kutaka kuondoa Gambia katika mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, na Jumuiya ya Madola.

Raia wengi wa Gambia walikesha usiku wote wakisherehekea kuondoka kwa Bw Jammeh, ambaye amesema kuwa ataendelea na shughuli zake za kilimo.

Lakini changamoto nyingi zipo.

Taifa hilo ni maskini sana, na wananchi wengi wachanga wametorokea mataifa ya ng'ambo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Nakumbuka huyu bwana jameh alisema atatawala milele sijui miaka 22 ndo milele???
 
Ngoja aonje madaraka utamu wa madaraka, hayo yote anayoyaahidi yatageuka ndoto
 
Nakumbuka huyu bwana jameh alisema atatawala milele sijui miaka 22 ndo milele???
Wakiingia madarakani wanafikiri wameinunua nchi kama hawa wa ccm! Wataota na kufanya kila kitu kama nchi ni mali yao binafsi kumbe Mungu muumba asivyo na hiana anawaangalia kwa makini na punde anapiga shoka la Inkoskazi wanagaragazwa kama Saddam, Idd Amin na Gadafi! Ole wao!
 
Back
Top Bottom