Rais "mteule" John J.P Magufuli, rudisha Umoja wa Taifa

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,598
1,539
Wasalaam wakuu.

Nianze kutoa pole kwa wafuasi/wanachama na waumini wa Upinzani wa kweli nchini bila kujali itikadi za vyama vyao. Pole zaidi zikiwa kwa wanaUKAWA lakini pia wanaCCM walioshindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Pongezi zisizo za dhati kwa Rais John JP Magufuli kwa "ushindi" wa 'kuteuliwa' kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia kwa wafuasi/waumini, wanachama na mashabiki wa CCM.

Sasa ni wazi tunawaza maisha baada ya Uchaguzi mkuu.

Siku chache mara baada ya Uchaguzi kuwekuwepo na simanzi, lakini furaha kwa watu wengine. Katika sehemu mbalimbali Tanzania nzima(kazi zimesita).

Mwaka 1998, baada ya Ufaransa kushinda Kombe la Dunia la mpira wa miguu, ilikuwa patashika katika miji mikubwa Ufaransa hasa Paris(Kitovu cha Kivutio). Hii ilipelekea kuwa na shamra shamra, matamasha kwa takribani miezi miwili huku kazi zikisitishwa kwa ushindi waliokuwa nao(kuwashinda mabingwa wa Dunia). Hii ilifuatiwa na Uchumi kuporomoka kwa kiasi kikubwa na Taifa kuwa katika hali isiyo nzuri kiuchumi lakini hata watu binafsi.

Hii ndiyo ninaiona Tanzania leo, kundi kubwa likishindwa kufanya kazi kutokana na Majonzi, na kundi lingine kushindwa kufanya kazi likijisherehesha.

Nchi yetu tumekuwa 'wamoja ingawa si wamoja wala pamoja' kwa muda mrefu. Binafsi kwa hali ninayoiona katika ofisi(za serikali na binafsi), sehemu za mikusanyiko(sokoni, nyumba za ibada/swala, vituo vya usafiri) ni ya majonzi na kukatisha tamaa.(Hapa nikimaanisha mikoa mitatu niliyobahatika kutembelea baada ya uchaguzi).


Ninaona Tanzania ngumu kuwahi kutokea toka enzi za Mwl.(pengine wakati wa ukoloni tu) kwa maana ya;



UAMINIFU.
Hakuna suala gumu katika uongozi kama kuongoza watu wasiokuamini. Wengi wa wananchi(tukiamua kuweka 'ushabiki' pembeni ni kutazama kwa mustakabali wa Nchi hawaiamini CCM. Pengine imani iko kwa Magufuli(lakini ni nani aliye nyuma yake, ndilo swali la msingi).

Lakini pia watu hawaaminiani tena, wakinyoosheana vidole, 'hawa ndiyo wanaotukwamisha' lakini wengine wakitamba, 'Mtaisoma namba".

'A house that is divided against itself can not stand'

Ingawa utendaji wa Rais 'mteule' unajulikana na ni uhakika (ukilinganisha na baadhi ya mawaziri waliokuwa nae ngazi moja ya uongozi). Lakini si yeye mwenye kuiendesha Serikali pekee. Watu waliochini yake(Watendaji) kwa maana ya Mawaziri(Baraza la mawaziri) ni watu wa kutegemewa, Usalama wa Taifa, Jeshi na Wananchi anatakiwa ku_side nao.


Hatua tulipofika sasa ni mbaya ya kuwahi kutokea katika nchi hii, watu kubaguana. Hoja, Mradi, Mpango kazi, n.k makazini vinaweza kukataliwa tu kwa sababu ya tofauti. Watu kutoshiriki shughuli za kijamii mf. Harusi, Misiba n.k kutokana na tofauti za kiitikadi tu.


MISAADA.
Kwa Nchi ya Tanzania("tuliyoridhika" kuwa bila misaada bajeti yetu haitufikishi popote) ninaona ni jambo la siku za usoni kwa maisha magumu. Utofauti kati wa UN na EU katika uchaguzi mkuu 2015 Lakini utalitesa taifa.

Lakini pia Sabotage kufanyika Serikalini katika misaada mingi kutolewa(kwa Donors) watakaokuwa wamebaki bado) kutofika mahali kusudiwa.

Maamuzi ya "haraka haraka" ya Rais: Japokuwa Rais 'mteule ni mchapakazi' lakini tabia ya 'kukurupuka' haifichiki, katika kampeni tumeona maamuzi mengi na kauli nyingi ambazo ni dhahiri kuna shida kwa 'mteule' . Hapa ninapata wasiwasi kwa jambo moja. Ingawa Mheshimiwa 'mteule' ana washauri lakini ninamfahamu kama mtu wa msimamo binafsi(ambalo ni jambo zuri) lakini zaidi ya yote kuwa unpredictable. Maamuzi haya yanaweza kumtesa na hili litakuwa gumu kwake kwani si kila la kuambiwa ni lazima kulifanyia kazi hasa katika 'atmosphere' hii isiyoeleweka). Na hapa ndipo pengine anaweza kupoteza kundi dogo lililobaki(Patriot) na ambao so far wao wana neutral interest katika siasa, ila hotuba yake ya kwanza na pengine siku 90 za utawala wake zinaweza kufanya wao pia ku_pick side.


VIPAUMBELE.
Ni dhahiri kuwa kulikuwa na vipaumbele kadhaa vilivyotajwa wakati wa kampeni, na pengine kwa sasa baada ya kuingia madarakani re_shuffle ya vipaumbele hivi kutokea. Lakini hivi vikitegemea nguvu kazi isiyomuamini. Lakini kwa wale wanaomuamini bado kupata ukinzani mkubwa kutoka upande wa pili na hivyo mwisho wa siku kurudi pale pale.

Si Jeshi(Polisi na JKT), si usalama wa Taifa, Wananchii walio wamoja kwa sasa.

Hata hivyo 'mteule' alisema anaitwa tinga tinga na kwake yeye ni Kazi tu. Hebu na mtihani huu wa kuliunganisha tena Taifa uushinde.
 
Back
Top Bottom