Carter na Clinton walisaidiaje dunia, Afrika, na Tanzania?
Correction...
He is not pro abortion but pro-choice.
Sikubaliani na wewe pale unapomlinganisha Obama na Kikwete.
...ilikuwa haina hata haja ya kumjibu!! Obama ni baaaaaab'kubwa kuliko Nyerere mara million!!!
Uchambuzi wako Mwanakijiji sidhani kama ni sahihi.
Kwanza kama wewe unadhani sera za Bush ni nzuri...Then ni wazi sitoshangazwa unapomfagilia Mc Cain.
Jambo moja uelewe...Sera za Bush na Obama ni tofauti so as vs Mc Cain.
MKJJ huo utajiri unaodai utasambazwa ni upi huo? Mbona ndani ya miaka nane ya Bush walishushiwa kodi lakini bado makampuni yaka outsource biashara zao? Republican hawataweza kushusha kodi kiwango cha kupambana na lets say Mexico, China na hata India.
Uchaguzi huu Mc Cain naye anaweza kushinda, hilo la washabiki kufanya hayo si jambo la ajabu....Hata hivyo umenishangaza sana kwasababu hujatilia maanani historia ya Taifa hili...Kwao uchaguzi huu ni wa tofauti sana na wanautilia maanani sana na matokeo yataonyesha ni kwa jinsi gani wananchi wa marekani wamejihusisha na siasa kwa kiwango kisicho cha kawaida.
Watu wameshapiga kura na bado wanapiga kura kwa viwango vya kuvunja rekodi....Yani kila mtu ni simulizi. Ukizungumza na wamarekani hata ambao si weusi kama unavyodai na wao pia ni jambo la kihistoria kutokana na historia ya Taifa hili.
Kwamba imetokea kuwa ni mweusi hilo ni jambo la kihistoria hilo halina ubishi....Kwamba ana sera nzuri inategemea na kama wewe ni tajiri mkubwa mwenye uchu na asiyewajali masikini ambao uwezo wao wa kuspend ndio unausukuma uchumi.
Hao matajiri wanaotaka kuwekeza hapa marekani na kupata faida ya kuwatosha huku taifa likineemeka ndio matajiri wazuri ambao wako nyuma ya Obama...Matajiri ambao wanasema kama marekani iliweza kuutokomeza ugonjwa wa malaria hapa marekani ni kwanini isiwezekane Afrika?
Uchaguzi wa kesho ni wa kihistoria na yeyote kati ya Mc Cain na Obama anaweza kushinda...Lakini yeyote kati yao atakayechaguliwa atafanya tofauti kabisa na atakalofanya mpinzani wake kama angechaguliwa.
Naomba usubiri 3 years ndio useme hivyoo. Kuna mambo kayafanya kwenye short career yake, tofauti na Kikwete.Wanalingana sana:
Wote ni populists
Wote wanatumia ahadi ya pepo na mambo mazuri bila kuwaambia watu ukweli wa hali halisi.
Wote wawili wamekampeni kwa kutumia ahadi tupu bila rekodi yoyote.
Wote wawili wamebebwa na vyombo vya habari to the expense of any other
Wote wawili wanatumia mvuto wa sura kama inspiration
Wote wawili wanaahidi kuwafanyia watu mengi zaidi kuliko yanayowezekana kibinadamu ikiwemo "lets go and change US, lets go and change the world - Obama" na "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" - Kikwete.
Wote wawili wanadaiwa kuwa na mahusiano na watu wenye mashaka; Obama na kina Ayers, Kikwete na kina Patel
Of course wanatofautiana pia; mmoja ni Mmarekani mwingine ni Mtanzania.
Wanalingana sana:
Wote ni populists
Wote wanatumia ahadi ya pepo na mambo mazuri bila kuwaambia watu ukweli wa hali halisi.
Wote wawili wamekampeni kwa kutumia ahadi tupu bila rekodi yoyote.
Wote wawili wamebebwa na vyombo vya habari to the expense of any other
Wote wawili wanatumia mvuto wa sura kama inspiration
Wote wawili wanaahidi kuwafanyia watu mengi zaidi kuliko yanayowezekana kibinadamu ikiwemo "lets go and change US, lets go and change the world - Obama" na "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" - Kikwete.
Wote wawili wanadaiwa kuwa na mahusiano na watu wenye mashaka; Obama na kina Ayers, Kikwete na kina Patel
Of course wanatofautiana pia; mmoja ni Mmarekani mwingine ni Mtanzania.
Watanzania hatumuungi mkono mgombea Urais wa Marekani kwa kutegemea kwamba ataisadia dunia, Afrika na Tanzania. Kuwa na Rais wa US ambaye hatatumia majeshi ya Marekani kuanzisha vita visivyokuwa na kichwa wala miguu ni sababu tosha kabisa ya kumuunga mkono Rais kama huyo maana vita hivyo vinaathiri dunia nzima kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na athari nyingine mbali mbali.
Bush hizo pesa zake zote alizoahidi kuisadia Afrika ikiwemo Tanzania hazitatoka kwanza kutokana na hali ya uchumi wa US na pili Rais anayeingia kipaumbele chake kitakuwa siyo kuisaidia dunia, Afrika au Tanzania bali kuwasaidia Wamarekani kwanza ili kuujenga tena uchumi wa Marekani ambao umegubikwa na unemployment inayokuwa kwa kasi kubwa sana, budget deficit ya $500 billion and counting na deni la nje la $10.4 trillioni. Mpaka hapo uchumi wa Marekani utakapotengamaa nchi yeyote duniani isitegemee msaada toka US hata baadhi ya wananchi wameanza kuhoji umuhimu wa kuwapa Israel $3 billioni kwa mwaka wakati nchi yao iko katika hali mbaya ya kiuchumi.
Kuna mamilioni ya watu katika bara letu ambalo wanasubiri kwa hamu ushindi unaotarajiwa wa Obama kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huko Marekani. Kuna tafrija na sherehe zilizoandaliiwa sehemu mbalimbali ambapo watu weusi watasimama kufurahia ushindi wa Obama.
Sitoshangaa wengi wanaosubiri huo ushindi wa Obama wanafanya hivyo si kwa sababu wanakubaliana na sera zake zote (kuongeza kodi, kugawanya utajiri n.k) au misimamo yake ya kijamii (kuunga mkono utoaji mimba au haki za mashoga n.k) bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".
Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".
Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!
hapa najikumbusha maneno ya Mwalimu "Sisi bwana hatutukuzi rangi, tunatukuza mtu bwana"!
Yawezekana ulimwengu ukakosea katika ushabiki wake wa Obama kama Watanzania asilimia 80 ya wapiga kura walivyokosea walipomshabikia Kikwete. Kweli Obama ataweza kutimiza ahadi yake ya "kuibadili Marekani, na kuibadili dunia"?
Yawezekana kiongozi ambaye watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu zilipaswa kumshabikia ni McCain na siyo Obama kama wangeamua tu kuweka rangi pembeni? Well, masaa 24 yajayo will give us a clue.
...ilikuwa haina hata haja ya kumjibu!! Obama ni baaaaaab'kubwa kuliko Nyerere mara million!!!
kama watu wangetaka kumlinganisha Obama na Nyerere wangefanya hivyo mwaka 1961!
........bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".
Obama akiwa mweusi wewe utakuwa nani?
Obama is as white as any kid in america.
From a white a mom and a mzungu upbringing, calling him mweusi is like his mom and his up bringing dont exist.
Trust me there is a big reason behind this....thing BIG.
Miafrika 100% ndivyo tulivyo hata weupe 50% tunavutia kwetu.