Rais Mstaafu Mkapa alia na sera ya utumishi wa umma katika kavazi la Mwalimu Nyerere

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,512
2,730
mkapa%20zungumza.jpg

Mkapa alieleza kusikitishwa kwake na jinsi mfumo wa utumishi wa umma ulivyoparaganyika nchini,ambapo sasa mtu yeyote anaweza kupata nafasi yeyote bila kujali historia yake ktk utumishi.

Sera ya utumishi wa umma imeparaganyika kabisa.Lakini zamani,muulizeni mzee Msuya waziri mkuu mstaafu,ukilazimika kupitia hatua nyingi na ngazi toka chini mpaka juu,lakini sasa hivi unaweza ukawa yeyote wakati wowote alisema Mkapa huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mdahalo huo.

Aidha alizionya nchi za Africa kuwa makini na unaoitwa ushirikiano na nchi za magharibi kwasababu hauna nia njema na mustakabali wa Africa.alisema watu wa magharibi wanafanya kila ghiliba kuwafanya waafrica wawaone kama wenzao na rafiki zao lakini hawana dhamira ya dhati kutaka kuliendeleza bara hili.

Aliongeza kuwa ushirika wa kibiashara unaopigiwa chapuo na mataifa ya magharibi kwa Africa una malengo ya kuwanufaisha wao zaidi kuliko waafrica wenyewe na hata masharti ya kibiashara wanayosema ni nafuu,unafuu huo ni mtego wenye hatari kwa viwanda vya Africa.

Wanasema wanalegeza masharti ya biashara,hiyo ni kutaka kuingia kwenye soko lenu,wanaposema wanataka uwanja sawa wa biashara hiyo ni kutaka kujaza soko letu na bidhaa zao,tukikubali hilo ndani ya miaka 10 tu hatutakuwa na viwanda.

Mkapa aliendelea kusema ktk vitu anavyojutia ktk uongozi wake ni kutotimiza ndoto yake ya kuhusu wakulima na kilimo cha Tanzania kwa ujumla,anajutia kushindwa kuanzisha benki ya kilimo ambayo ingewahudumia kulingana na mahitaji na haki zao.

Alisema umasikini wetu ni kielelezo cha kushindwa kwa sera za umma na kwamba ili kuondokana na umasikini ni lazima kufanya mapinduzi ya wakulima na wafugaji ili waweze kujiletea maendeleo.Mwisho wa kumnukuu.

WAKATI Bruce Holland, Seneta wa zamani wa Arkansas, aliposema "Watu wanapozungumzia viongozi mahiri, wanafanya hivyo kwa bashasha na upendo wa dhati toka moyoni na kwenye sauti zao, hata kama viongozi husika wamefarika dunia miaka mingi, wanaongea kwa hamasa na unaona jinsi wanavyovutiwa na viongozi wanaowazungumzia, kwa sababu viongozi mahiri hawafi', hakujua kama alikuwa anamzungumzia Mwalimu Nyerere.

Kwa yeyote aliyekuwa ndani ya Ukumbi wa Tume ya Sayansi (COSTEC) kwa siku mbili kushuhudia uzinduzi wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, atakuwa shuhuda wa ukweli kwamba viongozi mahiri hawafi, wanaishi milele kupitia fikra zao na maisha yao.

Umilele wa fikra za Mwalimu ulijidhihirisha kwenye uzinduzi wa Kavazi la Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Archive) kupitia mjadala uliohusisha vijana, wazee, wanazuoni na watu wa kada zote kuhusu dira na mwelekeo wa Tanzania ya sasa ukilinganisha na wakati wa Mwalimu.

Kavazi hilo la Mwalimu ambalo lilizinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ni zao la utafiti wa wanazuoni watatu walioufanya kuhusu fikra za Mwalimu. Professa Issa Shivji, ambaye ni Mkurugenzi wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, Profesa Saida Yahya-Othman na Dk. Ng'wanza Kamata, ambao hatimaye utahitimishwa na kuandika bayografia ya Mwalimu.

Kama alivyowahi kusema mwenyewe, wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi Mjini Mbeya mwaka 1995, kuhusu azimio la Arusha kwamba "Leo narudia kusoma Azimio la Arusha hata kama hamlitaki. Kama kuna watu Tanzania hawajali, wachukue waanze kulisoma ili waone na waniambie wanachokiona mle kibaya ni nini hasa. Asome tu kwa dhati tu na kisha aseme hiki ni kibaya". Ndivyo iluvyojitokeza katika ukumbi huo.

Usahihi na uhai wa misingi ya Azimio, ulibainishwa na watu waliohudhuria kongamano hilo wakiwemo vijana, ambao hawakuwahi kuliishi lakini wanalisoma na kuona amtunda yake. Msisitizob ulikuwa katikia kutafuta dira ya taifa, ambayo itakuwa msingi wa rejea wa mambo ya kitaifa yanayoaswa kufanyika nchini kama mitaala ya elimu, aina ya siasa na viongozi tunaowahitaji kuliongoza taifa letu.

Shairi la Nyerere laibua hisia kali.

Moja ya mambo ya kusisimua yaliyotokea ukumbini humo, lilikuwa ni shairi lililotungwa na Malenga wa Kavazi, Mwalimu Bashiru Ally, likimkaribisha Mwalimu Nyerere katika uzinduzi wa Kavazi lake ili kujadiliana mambo muhimu ya taifa yanayokwenda mrama.

Wakati shairi hilo linasomwa hali ya utulivu iliongezeka huku nyuso za waliohudhuria kongamano hilo zikionyesha hisia za kuguswa na tungo zake kiasi cha kuwafanya wengine kulia. Huku ukweli wa fikra za kizalendo za Mwalimu ukituama sawia kwenye akili za waasikilizaji.

Ubeti mmoja wa shairi hilo ulisema.

Afrika bara letu, sasa halina amani,
Uhuru na utu wetu, kwa sasa viko rehani,
Fikra na mila zetu, havina tena thamani,
Karibu Baba Nyerere, Tutafakari pamoja.
Mkapa alia na Sera ya Utumishi.

Katika Kavazi hilo, Rais wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alieleza kusikitishwa kwake na jinsi mfumo wa utumishi wa umma ulivyoparaganyika nchini, ambapo sasa mtu yeyote anaweza kupata nafasi yeyote bila kujali historia yake katika utumishi.
Mkapa ambaye pia alikuwa mwanamjadala mkuu pamoja na Professa Adebayor Olukoshi kutoka taasisi ya UN – African Insititute of Economic and Development Planning, alisema.

"Sera ya Utumishi wa Umma imeparaganyika kabisa. Lakini zamani, muulizeni Mzee Msuya (Cleopa, Waziri Mkuu Mstaafu) ulilazimika kupitia hatua nyingi na ngazi toka chini mpaka juu, lakini sasa hivi unaweza ukawa yeyote wakati wowote," alisema Mkapa huku akishangiliwa na wananachi waliohudhuria mdahalo huo.

Alisema hilo ni moja ya mambo yanayochangia kufifisha moyo wa uchapa kazi na uzalendo miongoni mwa watumishi wa umma hali inayozorotesha harakati za maendeleo.

Aidha alizionya nchi za Afrika kuwa makini na unaoitwa ushirikiano na nchi za Magharibi kwa sababu hauna nia njema na mustakabali wa Afrika. Alisema watu wa Magharibi wanafanya kila ghiliba kuwafanya Waafrika wawaone kama wenzao na rafiki zao lakini hawana dhamira ya dhati kutaka kuliendeleza bara hili.

Aliongeza kuwa ushirika wa kibiashara unaopigiwa chapuo na mataifa ya Magharibi kwa Afrika una malengo ya kuwanufaisha wao zaidi kuliko waafrika wenyewe na hata masharti ya kibiashara wanayosema ni nafuu, unafuu huo ni mtego wenye hatari kwa viwanda vya Afrika.

"Wanasema wanalegeza masharti ya biashara, hiyo ni kutaka kuingia kwenye soko lenu, wanaposema wanataka uwanja sawa wa biashara hiyo ni kutaka kujaza soko letu na bidhaa zao, tukikubali hilo ndani ya miaka 10 tu hatutakuwa na viwanda," alisema.
Ajutia kutowajali wakulima.

Awali akijadili mada iliyotolewa na Professa Olukoshi kuhusu kurejesha taifa la kimaendeleo (The return of the Developmental state), Mkapa alisema miongoni mwa vitu anavyojutia katika uongozi wake ni kutotimiza ndoto yake kuhusu wakulima na kilimo cha Tanzana kwa ujumla.

"Majuto yangu makubwa kama kiongozi ni kutoweza kuanzisha benki ya kilimo, ambayo ingewahudumia kulingana na mahitaji na haki zao" alisema Rais Mstaafu Mkapa.

Alisema umaskini ni kielelezo cha kushindwa kwa sera za umma na kwamba ili kuondokana na umaskini ni lazima kufanya mapinduzi ya wakulima na wafugaji ili waweze kujiletea maendeleo.

Prof. Adebayor: Nyerere ni Baba wa Afrika.

Akizungumza katika mdahalo huo Professa Adebayor Olukoshi, alielezea heshima aliyopata ya kufanya kazi na Mwalimu Nyerere katika miaka miwili ya mwisho ya uhai wake.

"Mwalimu amekuwa ni mtoto shujaa wa Afrika, nilikuwa nafanya kazi nae wakati mwingine nilikuwa nachukua notes Mama Wickens asipokuwepo, ni heshima kubwa kwamba mnamuita Baba wa taifa lakini kwa uhakaki ni Baba wa Afrika," alisema.

Akizungumzia mustakabali wa Afrika na kurejeshwa kwa taifa la kimaendeleo, alisema Afrika lazima ijifunze kujisimamia na kutekeleza malengo na ndoto zake na kwamba katika kufanya hivyo inapaswa itambue kuwa jambo hilo halitawafurahisha watu wa Magharibi.
"Tisitarajie kupigiwa makofi na mataifa ya nje kwa kutekeleza na kusimamia sera ya kujitegemea, " alisema.

Aliwataka Waafrika kurejea kwenye misingi ya awali ambayo ilijengwa juu ya kanuni za kujitegemea na kuachana na falsafa zinazopuuza mambo yenye manufaa kwa Afrika.

"Badala ya kupeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi kwa gharama kubwa, kwanini hatujengi Vyuo Vikuu vyenye hadhi ya namna hiyo hapa barani Afrika kuondokana na gharama hizo za kila mwaka, viongozi wetu wanatibiwa Ujerumani kwenye hospitali bora, kwanini kwanini tusijenge Hospitali hizo baora hapa kwa manufaa ya watu wetu?" alisema Prof. Olukoshi.

Alisisitiza kuwa ujenzi wa taifa la kimaendeleo lazima ujikite kwenye kujenga taifa lenye umoja na mshikamano dhidi ya unyonyaji wa aina yeyote.

Aidha alishangaa unyonge unaoonyeshwa na Waafrika mbele ya mataifa ya Magharibi ambayo yanafanya juhudi za wazi wazi kutaka kulitawala tena bara la Afrika, lakini waafrika na viongozi wao ama hawafanyi chochote wanatazama tu au wanafanya kama hawaelewi wakati wanauona ukweli huo.

"Wale wana dhamira ya dhati kabisa na wanatamka wazi wazi kwamba, ‘tunataka kuwatawala tena' sisi tupo tunasikia na hatufanyi kitu, lazima tuamke," alisema.

Usuli wa kavazi la Mwalimu Nyerere

Hotuba kamili ya Mkurugenzi wa Kavazi la Mwalimu kwenye uzinduzi inachapwa hapo chini kwa ajili ya rekodi na faida kwa Watazania.

"Napenda kuungana na Dk. Mshinda (Hassan, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH) kuwakaribisha kwenye shughuli hii adhimu. Ni kilele cha kazi yetu ya utafiti wa miaka mitatu wa kuandika bayografia ya Mwalimu Nyerere. Tumefarijika sana kwamba mmekubali mwaliko wetu na kujumuika nasi.

Miaka mitatu iliyopita, pamoja na wenzangu wawili, Profesa Saida Yahya-Othman na Dk. Ng'wanza Kamata, tuliamua kuandika bayografia ya Mwalimu. Ulikuwa uamuzi wa kijasiri kweli kweli lakini mara nyingine lazima uamue kufanya linalotakiwa kufanywa. Bahati nzuri, Dk. Mshinda alikubali kugharamia mradi wetu.

Wakati wa utafiti wetu, tuliweza kukusanya nyaraka katika makavazi mbalimbali ndani na nje ya nchi pamoja na kuwahoji watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wastaafu wa ndani na nje ya nchi. Tunashukuru kwamba, bila kusita, wengi wenu mlitupokea na kuzungumza nasi kuhusu Mwalimu.

Ni kweli kwamba kuna mengi katika urithi aliotuachia Mwalimu, ambayo tumeyasahau au kuyapuuza. Lakini kuna jambo moja lililojengeka katika hulka ya viongozi wetu, hasa viongozi wa kizazi cha kwanza baada ya uhuru, ambalo bado lipo, ingawa limeanza kufifia. Hulka hii ni upole na unyeyekevu, bila kuwa na kiburi, jambo ambalo sio kawaida kwa viongozi wengi.

Marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, viongozi waandamizi serikalini, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa mashirika ya umma, na zaidi, familia ya Mwalimu - wote hao walikaa nasi kwa masaa mengi ya mazungumzo. Wachache walitukatalia, na wachache zaidi waliamua kusema yale tu waliotaka kuyakumbuka; ingawa hao walikuwa wachache sana.

Baadhi ya wale tuliowahoji walituruhusu hata kuchambua nyaraka zao binafsi. Hii inanipa ujasiri wa kuwaomba viongozi na wananchi wengine walifikirie Kavazi kama mahali pa kuhifadhi nyaraka zao.

Wote tunawashukuru kwa moyo mkunjufu.

Tulitarajia kwamba utafiti wetu utazaa matokeo mawili. La kwanza, ambalo ni wazi, ni kitabu ambacho tunaendelea kukiandika. La pili, ambalo sio wazi sana, ni KAVAZI LA MWALIMU NYERERE ambalo tunalizindua leo. Lengo kuu la KAVAZI lilikuwa wazi tangu mwanzo, ambalo ni kukusanya na kuhifadhi nyaraka na taarifa tulizopata wakati wa utafiti wetu. Hii ndio sifa kuu ya makavazi.

Tukiwa tunaendelea na utafiti lengo la pili lilijitokeza. Tulipokuwa tunasoma na kujadili nyaraka mbalimbali – madokezo ya Mwalimu katika mafaili, barua na makala zake, n.k. – tulifikiri kwamba haitoshi kuhifadhi nyaraka kana kwamba fikra za Mwalimu ni mfu. Fikra zinastahili kuwa hai. Uhai wa fikra ni kuzijadili, kuzidadisi, kuzichambua na kuzikosoa. Mijadala ndio utambulisho wa fikra. Migongano ya fikra ndio huzaa ufahamu na uelewa mpya.

Ndipo tukaamua kwamba Kavazi liwe na shughuli nyingine muhimu. Kupitia njia mbalimbali – kama mihadhara, makomgamano, mazungumzo n.k. – Kavazi liandae malumbano juu ya fikra za Mwalimu pamoja na masuala mengine muhimu ambayo yalikuwa yanamtatiza. Na bila shaka Tume ya Sayansi ni mahali mwafaka pa kuendeleza mijadala ya aina hii.

Kadhalika, tuligundua jambo jingine wakati wa mahojiano yetu na viongozi. Wengi wao, hususan wale wa kizazi cha kwanza na cha pili baada ya uhuru, na ambao wamestaafu, wanakereketwa na mengi, wangependa kujadili, kubadilishana mawazo na kushiriki katika mijadala ya kitaifa bila vikwazo vya kiprotokali.

Kwa hiyo, tukaona Kavazi linaweza kuwa mahali pa wao kukutana na wenzao, na wasomi na watafiti, na kujadili nao, kuzungumza nao, kubadilishana taarifa na mawazo na kutoa mchango wao. Fikra kama hizi ndizo zimechangia, kwa kiasi fulani, katika kuandaa ratiba ya sherehe hizi za uzinduzi. Huu ni mwanzo; fikra zetu zinakua. Tunawategemea nyinyi kutuuunga mkono.

Bila shaka kutakuwa na mawazo mengi katika mijadala yetu. Kutakuwa na migongano ya mawazo. Tunatarajia kujadili na kudadisi mawazo na fikra pana – fikra za kimaendeleo, sio fikra mgando. Tunakusudia kuendeleza fikra-mkakati katika mijadala na masomo yetu. Tunataka kuangalia mbele, sio tu ya kesho au keshokutwa au uchaguzi ujao.

Mijadala yetu itakuwa inaangalia mbali na wakati wake utakuwa wa masafa marefu – zaidi ya malumbano ya vyama vya siasa, zaidi ya mifumo iliyopo ya demokrasia na kiuchumi. Tunataka kufikiri na kuwafikirisha wanazuoni wetu kuhusu mifumo mbadala. Binadamu hajafilisika kifikra kiasi cha kukubali kuwa demokrasia ni mchezo wakubadili sura za watawala kila baada ya miaka mitano.

Binadamu hajafika kilele chake cha ubunifu kiasi cha kudhani kuwa soko ni mfumo pekee wa uchumi. Tunataka kuvuka mipaka ya ufahamu iliyowekwa na mifumo tawala.

Napenda kuhitimisha kwa kugusia mambo mawili, moja ni la msingi, na jingine ni la kawaida. La kawaida linahusu fedha. Tungependa KAVAZI lijitegemee.

Ndio maana tumeunda mfuko maalum (Endowment Fund) ambao utazalisha fedha za kujiendesha. Tunamshukuru sana Dk. Ramadhani Dau, Mkuu wa NSSF, kwa kuchangia fedha za awali za kuanzisha mfuko huu. Tunawakaribisha wengine wachangie kuukuza Mfuko wa Kavazi.

Tunashukuru shirika la Rosa Luxemburg waliotupa fedha za kuendesha shughuli za Kavazi kwa mwaka wa kwanza. Jina la Rosa Luxemburg lina umuhimu wa kipekee katika historia ya ujamaa. Rosa alipambana dhidi ya unyonyaji na udhalilishaji wa wavujajasho. Na alijitoa mhanga katika mapambano hayo. Aliwahi kusema kwamba: "Wasiosogea hawatambui kuwa wana minyororo."

Naam!. Tumeitambua minyoyoro ya utumwa; tumesogea na tumeivunja. Tumeitambua minyororo ya ukoloni; tumesogea chini ya uongozi wa Mwalimu, na tumeivunja. Sasa tunapaswa kubaini minyororo ya kiitikadi na kizuoni tuliyofungwa na wababe wa mitazamo ya uliberali mambo-leo; tunapaswa kusogea ili tuivunje. Ni matarajio yetu kwamba KAVAZI litachangia, ingawa kwa kiwango kidogo, kuchochea kusonga mbele.

Jambo la pili, ni kuhusu jina la KAVAZI LA MWALIMU NYERERE. Jina hili linatakiwa kufafanuliwa, japo kwa ufupi, kwa sababu limezuwa mjadala. Tafsiri ya Kiswahili ya neno la Kiingereza ‘Archives' ni Makavazi, kwa maana ya mahali pa kuhifadhi nyaraka za kale na za kihistoria.

Kama ilivyo kwa neno la Kiingereza (archives), neno Makavazi halina umoja. Hata hivyo, kwa hisia na dhamira zetu, makavazi yanayotunza nyaraka zinazomhusu Mwalimu yana umuhimu na hadhi maalum. Na sisi tulitaka jambo hili lijitokeze waziwazi katika jina la chombo hiki. Ndio maana tumediriki kubuni neno KAVAZI ambalo ni mzizi wa neno au dhana ya makavazi.

Ili kusisitiza upekee wake, tunaliita ‘Kavazi LA' Mwalimu Nyerere, na sio Kavazi ‘ya' au Kavazi ‘ka-'. Kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza ‘Kavazi la' ni sawa na kusema ‘The Archive'; huwezi ukasema ‘The Archives' katika wingi.

Karibuni Kavazini."

Chanzo: Raia Mwema
 
Mkapa siku zote alikuwa mtu wa kuongea mambo ya msingi sana na kazi yake ilionekana. Ninachelea kuona kwamba kuna kitu kimebadilika kwa huyu mzee. Ameanza kukosa confidence za kulenga matatizo kinyume na slogan yake ya ukwlei na uwazi.

Ninategemea angeenda zaidi ya kutaja tu kuparanganyika kwa mfumo wa utumishi wa umma. Ingeleta maana na uhai zaidi kama angeweka bayana sababu za kupranganyika huko, kwa sababu watumishi wa umma hawajipi utumishi bali wanapewa. Mifumo kama ni mibovu si suala la bahati mbaya au kwamba halifahamiki.

Ingeonyesha uzalendo na kujali taifa kama angemsema Kikwete kwamb ameharibu mifumo yote na uharibifu huo umeathiri taifa na athari zake haziishi leo. Kwa uharibifu huo kila sector ya umma imekaa ovyo ikiendeshwa na ufisadi, rushwa, favoritism, ubabe, udanganyifu na u dictator abavyo vimekwenda hadi ngazi za chini sana na hakuna akemeaye wala anayeonyesha nia ya kuzuia ama kukomesha.

Nilitegemea angeonya pia ukiukiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora na namna inavyokwenda kuangamiza taifa letu.

Nilitamani azungumzie suala la mahusiano miongoni mwa watawala, watawaliwa na wageni. Kwamba watawala kuwabagua watawaliwa na kujiungamanisha na wageni ni hatari, kwa nchi, ndipo aje kwenye sera za mahusiano ya kimataifa whether ni ya magharibi ama ya mashariki.

MKAPA ANAOGOPA NINI KUKEMEA UOVU KWA WAZI? KIKWETE AKILI ZAKE ZIKO CHINI YA KIWANGO. BILA KUTAMKA BAYANA HANA UWEZO WA KU INTERPRET NA KUELEWA. ATAJUA TU WANASEMWA VINOGZI WA AFIRCA.

Hata kama audience yake haikutampa nafasi ya kwenda kwenye details kama zile, lakini kama anaufahamu huo, nilitegemea kwa hapa nyumbani angeshafanya juhudi za makusudi kunusuru nchi na majanga ambayo ccm inayatengeneza.
 
Kwa jinsi ninavyojua mzungu yupo kwa ajili ya kulinyonya bara la afrika, mbaya zaidi hakuna kiongozi hata mmoja WA kiafrika ambaye anaongoza kwa maslahi ya wananchi wake, wote mafisadi Tu, anatengeneza kitu cha shilingi kumi huku kahonga kitu cha milioni.
 
Amesema ukweli, na hili likiendelea, tutegemee maamuzi ya ajabu zaidi kwenye utumishi wa umma. Kwa maana wenye sifa hawapewi nafasi, wasio nazo wanapewa na matokeo yanaonekana!
 
Mkapa siku zote alikuwa mtu wa kuongea mambo ya msingi sana na kazi yake ilionekana. Ninachelea kuona kwamba kuna kitu kimebadilika kwa huyu mzee. Ameanza kukosa confidence za kulenga matatizo kinyume na slogan yake ya ukwlei na uwazi.

Ninategemea angeenda zaidi ya kutaja tu kuparanganyika kwa mfumo wa utumishi wa umma. Ingeleta maana na uhai zaidi kama angeweka bayana sababu za kupranganyika huko, kwa sababu watumishi wa umma hawajipi utumishi bali wanapewa. Mifumo kama ni mibovu si suala la bahati mbaya au kwamba halifahamiki.

Ingeonyesha uzalendo na kujali taifa kama angemsema Kikwete kwamb ameharibu mifumo yote na uharibifu huo umeathiri taifa na athari zake haziishi leo. Kwa uharibifu huo kila sector ya umma imekaa ovyo ikiendeshwa na ufisadi, rushwa, favoritism, ubabe, udanganyifu na u dictator abavyo vimekwenda hadi ngazi za chini sana na hakuna akemeaye wala anayeonyesha nia ya kuzuia ama kukomesha.

Nilitegemea angeonya pia ukiukiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora na namna inavyokwenda kuangamiza taifa letu.

Nilitamani azungumzie suala la mahusiano miongoni mwa watawala, watawaliwa na wageni. Kwamba watawala kuwabagua watawaliwa na kujiungamanisha na wageni ni hatari, kwa nchi, ndipo aje kwenye sera za mahusiano ya kimataifa whether ni ya magharibi ama ya mashariki.

MKAPA ANAOGOPA NINI KUKEMEA UOVU KWA WAZI? KIKWETE AKILI ZAKE ZIKO CHINI YA KIWANGO. BILA KUTAMKA BAYANA HANA UWEZO WA KU INTERPRET NA KUELEWA. ATAJUA TU WANASEMWA VINOGZI WA AFIRCA.

Hata kama audience yake haikutampa nafasi ya kwenda kwenye details kama zile, lakini kama anaufahamu huo, nilitegemea kwa hapa nyumbani angeshafanya juhudi za makusudi kunusuru nchi na majanga ambayo ccm inayatengeneza.

mkuu nipenda sana uchambuzi wako,katiba yetu ina madhifu fulani fulani ambayo inapopata viongozi wasio waadilifu km hawa tulionao sasa hivi ni matatizo makubwa,nafikiri ni katiba hii hii mwalimu alisema imempa madaraka makubwa kiasi ambacho alikuwa anaweza kuwa dictator,haya ya udhaifu huo mkubwa yanapopata viongozi wa hovyo hovyo ndio tunaanza kushuhudia haya tunayoshuhudia sasa.
 
Amesema ukweli, na hili likiendelea, tutegemee maamuzi ya ajabu zaidi kwenye utumishi wa umma. Kwa maana wenye sifa hawapewi nafasi, wasio nazo wanapewa na matokeo yanaonekana!

mkuu chimbuko la haya yote lipo ktk katiba yetu,the president as the head of state is vested with a lot of power ambayo wakati mwingine kwa maslahi binafsi anatumia vibaya mamlaka yake vibaya.
 
mkuu chimbuko la haya yote lipo ktk katiba yetu,the president as the head of state is vested with a lot of power ambayo wakati mwingine kwa maslahi binafsi anatumia vibaya mamlaka yake vibaya.

Kweli katiba ndio tatizo ila Mkapa ni kiongoz pamoja na hayo mapungufu yake na katiba hii inawapa viongozi dhaif kufanya kama hayo wafanyayo Mungu tubariki tanzania
 
Kweli katiba ndio tatizo ila Mkapa ni kiongoz pamoja na hayo mapungufu yake na katiba hii inawapa viongozi dhaif kufanya kama hayo wafanyayo Mungu tubariki tanzania

mkuu ukiondoa makando kando ya Mkapa kufanya biashara akiwa ikulu,nafikiri ni rais bora kabisa tuliyewahi kumpata ukimuondoa baba wa taifa,wakati wa mzee Mkapa hatukuwahi kushuhudia teuzi za hovyo hovyo na zenye harufu ya ukengeufu wa maadili kama ktk awamu hii ya nne.
 
Teuzi za kiutendaji kwenye utumishi wa umma zinapogeuzwa kuwa kama teuzi za kisiasa na kirafk ndo matokeo yake. Angalia teuzi zilizofanyika kwenye Agency n Authority kwa kipindi cha miaka 7 iliyopita kama imezingatia huo mtiririko wa utumishi wa umma
 
mkuu ukiondoa makando kando ya Mkapa kufanya biashara akiwa ikulu,nafikiri ni rais bora kabisa tuliyewahi kumpata ukimuondoa baba wa taifa,wakati wa mzee Mkapa hatukuwahi kushuhudia teuzi za hovyo hovyo na zenye harufu ya ukengeufu wa maadili kama ktk awamu hii ya nne.

Tupo pamoja sana baada ya mwalim ni Ben hata akiongea unajua kweli rais anaongea na kipindi chake wazir alikua akiitwa ikuluanajiuliza mara 2 hadi anauuliza dereva wake nimefanya nn maana kulikua hakuendeki hovyo kama saizi kupiga story fresh tu Mkapa alituachia hela na dhahabu Benki kuu pamoja na yake ila leo hii tumekuo ambaomba Tanzania hii yenye kila kitu inauma sana
 
Ndiyo maana ccm hawataki kuwa na katiba nyingine ili waendeleze ubwanyenye huu. Sasa kinachohitajika ni kuipiga chini katiba waliyotengenza ambayo inawapa madaraka na uwezo wa kuabuse vile watakavyo. Tuambizane katiba ya ccm hapana bila kujali mikoromo ya mafisadi, li tuwe na katiba bora itakayosimamia maslahi ya umma bila kutegemea discretion ya raisi. Nyerere na Mkapa kwa sehemu waliweza, lakini Kikwete ameproove failure na amedhihirisha madhara ya katiba yetu kwa mtu asiye na aibu wala uadilifu kama yeye.

mkuu nipenda sana uchambuzi wako,katiba yetu ina madhifu fulani fulani ambayo inapopata viongozi wasio waadilifu km hawa tulionao sasa hivi ni matatizo makubwa,nafikiri ni katiba hii hii mwalimu alisema imempa madaraka makubwa kiasi ambacho alikuwa anaweza kuwa dictator,haya ya udhaifu huo mkubwa yanapopata viongozi wa hovyo hovyo ndio tunaanza kushuhudia haya tunayoshuhudia sasa.
 
​Mzee wetu Mkapa ameongea ukweli kabisa, pamoja na matatizo yake mengine lakini alitutoa mbali, profesa kaja kutuzamisha
 
Kweli mkapa umenena.viongozi wataasisi kama za muhimbili na moi ni urafiki umefanyika bila kuangalia vigezo hadi taasisi zinakufa
 
Kweli katiba ndio tatizo ila Mkapa ni kiongoz pamoja na hayo mapungufu yake na katiba hii inawapa viongozi dhaif kufanya kama hayo wafanyayo Mungu tubariki tanzania

Unajua mkapa alipendekezwa na MTU mmoja(nyerere),ndomana alikua huru katika utendaji,JK aliingizwa na kundi la watu,ndomana hayupo huru,tutegemee kuwa hivyo,labda Lowasa atakua tofauti,sababu ametumia gharama zake
 
Unajuwa kuwa Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha aliongeza ada. Alipohojiwa akasema "kila mtu ataubeba msalaba wake"

Hivi unajuwa kuwa Ben ndo alimfuata Nyerere kwake akanshawishi aende kutibiwa ulaya.? Yeriko Nyerere njoo huku.
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo maana ccm hawataki kuwa na katiba nyingine ili waendeleze ubwanyenye huu. Sasa kinachohitajika ni kuipiga chini katiba waliyotengenza ambayo inawapa madaraka na uwezo wa kuabuse vile watakavyo. Tuambizane katiba ya ccm hapana bila kujali mikoromo ya mafisadi, li tuwe na katiba bora itakayosimamia maslahi ya umma bila kutegemea discretion ya raisi. Nyerere na Mkapa kwa sehemu waliweza, lakini Kikwete ameproove failure na amedhihirisha madhara ya katiba yetu kwa mtu asiye na aibu wala uadilifu kama yeye.

tunacho mshukuru Mungu nikwa Jk kutuonesha madhaifu makubwa ya katiba yetu kupitia teuzi zake zisizokidhi haja au wakati mwingine zisizokuwa na tija kabisa kwa taifa,rejea uteuzi wa wabunge wawili march 20 2015..
 
Unajua mkapa alipendekezwa na MTU mmoja(nyerere),ndomana alikua huru katika utendaji,JK aliingizwa na kundi la watu,ndomana hayupo huru,tutegemee kuwa hivyo,labda Lowasa atakua tofauti,sababu ametumia gharama zake

kauli yako inaweza kuwa na ukweli mwingi ndani yake,haya yanayoitwa makundi ya urais ndio yanatumaliza nowdays,wote wanaokusupport wakati unausaka urais lazima uje urudishe fadhila kwa kuwaweka kwenye nafasi mbali mbali za ulaji.
 
Ndiyo maana ccm hawataki kuwa na katiba nyingine ili waendeleze ubwanyenye huu. Sasa kinachohitajika ni kuipiga chini katiba waliyotengenza ambayo inawapa madaraka na uwezo wa kuabuse vile watakavyo. Tuambizane katiba ya ccm hapana bila kujali mikoromo ya mafisadi, li tuwe na katiba bora itakayosimamia maslahi ya umma bila kutegemea discretion ya raisi. Nyerere na Mkapa kwa sehemu waliweza, lakini Kikwete ameproove failure na amedhihirisha madhara ya katiba yetu kwa mtu asiye na aibu wala uadilifu kama yeye.

mkuu ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa wameahirisha kura ya maoni leo hvy ni faraja kwetu kwasababu tutapata muda wa kuwaelimisha wananchi kuhusu hii katiba bambikizi ya ccm,katiba hii sio mpya bali ni marekebisho ya katiba ya 1977.
 
Unajuwa kuwa Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha aliongeza ada. Alipohojiwa akasema "kila mtu ataubeba msalaba wake"

Hivi unajuwa kuwa Ben ndo alimfuata Nyerere kwake akanshawishi aende kutibiwa ulaya.? Yeriko Nyerere njoo huku.

mkuu embu funguka zaidi kuhusu huyu waziri mkuu mstaafu kwasababu nimeshamsikia wakimtaja taja ktk mystery iliyopo nyuma ya kifo cha Sokoine.
 
Last edited by a moderator:
Unajuwa kuwa Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha aliongeza ada. Alipohojiwa akasema "kila mtu ataubeba msalaba wake"

Hivi unajuwa kuwa Ben ndo alimfuata Nyerere kwake akanshawishi aende kutibiwa ulaya.? Yeriko Nyerere njoo huku.

cc Yericko Nyerere
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom