Rais mstaafu Kikwete: BRN iliniwezesha kuongeza ufanisi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Masuala ya Afya wa Mawaziri unaoandaliwa na Chuo Kikuu cha Harvard ujulikanao kama Harvard Health Leaders' Ministerial Roundtable uliofanyika Geneva leo. Mkutano huo wenye lengo la kujenga uwezo wa Mawaziri wa Afya na Wataalam kwa njia ya kubadilishana uzoefu umehudhuriwa na mawaziri wa Afya kutoka nchi zaidi ya 40 wakiwemo Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo.

Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu alialikwa kushiriki na kuelezea uzoefu wake katika mjadala kuhusu 'Mafanikio ya Kukumbukwa kwa Kuwezesha Utekelezaji wenye Matokeo' (Achieving a Legacy in Goverment by Getting Things Done). Katika mjadala huo, Rais Mstaafu Kikwete alielezea uzoefu wake kuhusu changamoto za utekelezaji wa programu na miradi ya Serikali na chimbuko la kuanzishwa kwa 'Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa' (BRN) ikiwemo mafanikio na changamoto zake. Katika jopo hilo, walishiriki pia Mhe. Baroness Tessa Jowel, Waziri wa Zamani wa Uingereza wa Masuala ya Olimpiki na Waziri wa Utamaduni, Michezo na Habari, na Mheshimiwa Idris Jala, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia anayeshughulikia Mpango wa Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Programu na Matokeo Malaysia ujulikanao kama PEMANDU.

Mheshimiwa Rais Mstaafu ameelezea changamoto aliyoipata kabla ya kuansishwa kwa BRN ambapo ilikuwa vigumu kujua na kufuatilia kwa uhakika hatua inayopigwa katika utekelezaji wa miradi na shughuli za Serikali. Kiu yake ilipata jawabu alipofanya ziara nchini Malaysia na kujifunza namna Mpango wao wa PEMANDU ulivyokuwa ukifanya kazi. Aliamua kujifunza kuwaalika wataalamu wa PEMANDU kuja kusaidia wataalam wa Tanzania kubuni mpango wa BRN.

Ameusifia mpango wa BRN kuwa umewezesha ufanisi kwa kuwezesha kupata 'matokeo makubwa kwa rasilimali zile zile'. Aidha mpango umewaleta pamoja wadau wote wa ndani na nje ya Serikali kushirikiana pamoja na kuainisha changamoto, kukubaliana vipaumbele, ufumbuzi, kugawana majukumu na kuhimizana katika kutimiza wajibu wa kila mdau. Aidha imewezesha kuwepo kwa takwimu na uwazi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uwajibikaji wa Serikali katika kutekeleza ahadi zake. Pamoja na uzuri wa mpango huo na mafanikio yaliyopatikana, changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa rasilimali katika kutekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Katika mjadala huo, Mawaziri wa nchi za Afrika wamevutiwa na uzoefu wa Tanzania na Mpango wa BRN na wameonyesha shauku ya kutaka kujifunza zaidi juu ya mpango wa BRN. Wamempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuonyesha uongozi kwa kuwezesha ubunifu katika utekelezaji wa programu za Serikali ambao umekuwa na matokeo mazuri yenye kupimika.
c7ad2acff5d327f2cefe92572a506428.jpg
 
Kikwete atabaki ktk kurasa za kumbukumbu njema ktk Taifa hili na Dunia kwa ujumla. Aliyepandishwa na Mungu mwanadamu hawezi kumshusha.
 
Kweli na Mimi ndo nagundua pamoja na mapungufu ya ufisadi kukithiri wakati wa utawala wake Mzee Kikwete lakini alikuwa mpenda Demokrasia ya kweli hakuwa na chembe ya Udikteta ...tutamkumbuka sana
 
Huyu mzee wetu bado hajarudi tu msoga kupumzika?, jamani viongozi wetu hebu boresheni Huduma za kijamii kijiji cha msoga ili huyu mzee arudi kijijini kupumzika mweeee
 
Huyu mzee wa msoga amesahau kama alikuwa rais. Ataenda mpaka kwenye mikutano ya wakulima wa iliki. Kwa hadhi aliyokuwa nayo huu mkutano ulikuwa wa kupiga chini.
 
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Masuala ya Afya wa Mawaziri unaoandaliwa na Chuo Kikuu cha Harvard ujulikanao kama Harvard Health Leaders' Ministerial Roundtable uliofanyika Geneva leo. Mkutano huo wenye lengo la kujenga uwezo wa Mawaziri wa Afya na Wataalam kwa njia ya kubadilishana uzoefu umehudhuriwa na mawaziri wa Afya kutoka nchi zaidi ya 40 wakiwemo Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo.

Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu alialikwa kushiriki na kuelezea uzoefu wake katika mjadala kuhusu 'Mafanikio ya Kukumbukwa kwa Kuwezesha Utekelezaji wenye Matokeo' (Achieving a Legacy in Goverment by Getting Things Done). Katika mjadala huo, Rais Mstaafu Kikwete alielezea uzoefu wake kuhusu changamoto za utekelezaji wa programu na miradi ya Serikali na chimbuko la kuanzishwa kwa 'Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa' (BRN) ikiwemo mafanikio na changamoto zake. Katika jopo hilo, walishiriki pia Mhe. Baroness Tessa Jowel, Waziri wa Zamani wa Uingereza wa Masuala ya Olimpiki na Waziri wa Utamaduni, Michezo na Habari, na Mheshimiwa Idris Jala, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia anayeshughulikia Mpango wa Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Programu na Matokeo Malaysia ujulikanao kama PEMANDU.

Mheshimiwa Rais Mstaafu ameelezea changamoto aliyoipata kabla ya kuansishwa kwa BRN ambapo ilikuwa vigumu kujua na kufuatilia kwa uhakika hatua inayopigwa katika utekelezaji wa miradi na shughuli za Serikali. Kiu yake ilipata jawabu alipofanya ziara nchini Malaysia na kujifunza namna Mpango wao wa PEMANDU ulivyokuwa ukifanya kazi. Aliamua kujifunza kuwaalika wataalamu wa PEMANDU kuja kusaidia wataalam wa Tanzania kubuni mpango wa BRN.

Ameusifia mpango wa BRN kuwa umewezesha ufanisi kwa kuwezesha kupata 'matokeo makubwa kwa rasilimali zile zile'. Aidha mpango umewaleta pamoja wadau wote wa ndani na nje ya Serikali kushirikiana pamoja na kuainisha changamoto, kukubaliana vipaumbele, ufumbuzi, kugawana majukumu na kuhimizana katika kutimiza wajibu wa kila mdau. Aidha imewezesha kuwepo kwa takwimu na uwazi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uwajibikaji wa Serikali katika kutekeleza ahadi zake. Pamoja na uzuri wa mpango huo na mafanikio yaliyopatikana, changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa rasilimali katika kutekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Katika mjadala huo, Mawaziri wa nchi za Afrika wamevutiwa na uzoefu wa Tanzania na Mpango wa BRN na wameonyesha shauku ya kutaka kujifunza zaidi juu ya mpango wa BRN. Wamempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuonyesha uongozi kwa kuwezesha ubunifu katika utekelezaji wa programu za Serikali ambao umekuwa na matokeo mazuri yenye kupimika.
c7ad2acff5d327f2cefe92572a506428.jpg

Naoma kama majirani zake wanamshangaa hadi wanachungulia kuona desa lake. Ufanisi aliojiongezea ni wakutengeneza majuha mengi ili afanikishe manipulations huku akitawisha migawanyiko na ufisadi nchini. Huyu jamaa angelikuwa na aibu za kibinadamu, bila shaka angejifungia sehemu mbali kabais na binadamu hata mikusanyiko na mitandao kwa sababu hajui anapoonekana akiropoka watu wanamfananisha na kiumbe gani.
 
Mkuu kwani JK alimfanya nini mama ako, mbona una hasira naye hivi. Dont u know JK ni kipenzi cha watanzania
 
Katika hii Dunia Dr. Kikwete ni miongoni mwa wachache waliopata Neema kubwa kubwa na ndogondogo !
 
32f718e1-599d-453a-bdea-a25d0c7d9e81.jpe

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Masuala ya Afya wa Mawaziri unaoandaliwa na Chuo Kikuu cha Harvard ujulikanao kama Harvard Health Leaders' Ministerial Roundtable uliofanyika Geneva leo.

Mkutano huo wenye lengo la kujenga uwezo wa Mawaziri wa Afya na Wataalam kwa njia ya kubadilishana uzoefu umehudhuriwa na mawaziri wa Afya kutoka nchi zaidi ya 40 wakiwemo Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo.

Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu alialikwa kushiriki na kuelezea uzoefu wake katika mjadala kuhusu 'Mafanikio ya Kukumbukwa kwa Kuwezesha Utekelezaji wenye Matokeo' (Achieving a Legacy in Goverment by Getting Things Done). Katika mjadala huo,

Rais Mstaafu Kikwete alielezea uzoefu wake kuhusu changamoto za utekelezaji wa programu na miradi ya Serikali na chimbuko la kuanzishwa kwa 'Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa' (BRN) ikiwemo mafanikio na changamoto zake. Katika jopo hilo, walishiriki pia Mhe. Baroness Tessa Jowel, Waziri wa Zamani wa Uingereza wa Masuala ya Olimpiki na Waziri wa Utamaduni, Michezo na Habari, na Mheshimiwa Idris Jala, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia anayeshughulikia Mpango wa Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Programu na Matokeo Malaysia ujulikanao kama PEMANDU.

Mheshimiwa Rais Mstaafu ameelezea changamoto aliyoipata kabla ya kuansishwa kwa BRN ambapo ilikuwa vigumu kujua na kufuatilia kwa uhakika hatua inayopigwa katika utekelezaji wa miradi na shughuli za Serikali. Kiu yake ilipata jawabu alipofanya ziara nchini Malaysia na kujifunza namna Mpango wao wa PEMANDU ulivyokuwa ukifanya kazi.

Aliamua kujifunza kuwaalika wataalamu wa PEMANDU kuja kusaidia wataalam wa Tanzania kubuni mpango wa BRN. Ameusifia mpango wa BRN kuwa umewezesha ufanisi kwa kuwezesha kupata 'matokeo makubwa kwa rasilimali zile zile'.

Aidha mpango umewaleta pamoja wadau wote wa ndani na nje ya Serikali kushirikiana pamoja na kuainisha changamoto, kukubaliana vipaumbele, ufumbuzi, kugawana majukumu na kuhimizana katika kutimiza wajibu wa kila mdau. Aidha imewezesha kuwepo kwa takwimu na uwazi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uwajibikaji wa Serikali katika kutekeleza ahadi zake. Pamoja na uzuri wa mpango huo na mafanikio yaliyopatikana, changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa rasilimali katika kutekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Katika mjadala huo, Mawaziri wa nchi za Afrika wamevutiwa na uzoefu wa Tanzania na Mpango wa BRN na wameonyesha shauku ya kutaka kujifunza zaidi juu ya mpango wa BRN. Wamempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuonyesha uongozi kwa kuwezesha ubunifu katika utekelezaji wa programu za Serikali ambao umekuwa na matokeo mazuri yenye kupimika.
 
Hivi BRN ilikuwa felt zaidi nje kuliko kwetu tulioliwa nayo
 
Nikiona hivi nafikiri- "you can fool some people ALL the time" It is true!
 
Yaani hapo hawa wazungu naona mambo ya plagiarism yamewapita kando...originator ni PEMANDU ya Malaysia sasa aliyedesa anatafuta nini huko? Au ndio applied researcher? Lakini hata Malaysia walishatumia..halafu naona kaarufu cha kumjenga upya huyu jamaa hapa JF baada ya wimbi la Magu kumshusha vichwani mwa watz. Lengo ni nini? Think big!
 
Anaitetea kijanja maana JPM ameshawatimua watendaji wa juu woote na mikataba yao hataki ku renew......Omary Issa Peniel Lyimo Maharage na wengineo wengi tu hawana la kufanya BRN JPM haitaki na haiamini kama ina ulazima!......hapo JK anapigia debe watu wake wa BRN kina Omary Issa!
 
Back
Top Bottom