Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai, akosea matumizi ya serikali, ayaita ni mabaya hayana tija

Mzee wa Code

Member
Sep 23, 2024
58
89
Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai, amekosoa matumizi ya serikali, akiyaita ni mabaya na yasiyo na tija. Akichangia Bungeni mwelekeo wa bajeti ya 2025/26 na mpango wa maendeleo wa Taifa, alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa miradi yenye manufaa kwa wananchi.

Amesema kuwa kuanzishwa kwa miradi isiyo na msingi, kama vile chuo cha umahili wa teknolojia ya habari, wakati chuo Kikuu cha Dodoma kinatoa masomo ya tehama na kina miundombinu iliyopo, ni mfano wa matumizi mabaya ya rasilimali.

Katika maoni yake, Vuai alionyesha wasiwasi kuhusu ufanisi wa mipango ya serikali, akiongeza kuwa ni lazima kuwe na mwelekeo wa kisera unaozingatia mahitaji halisi ya jamii. Hali hii inadhihirisha kwamba, licha ya kuwa mstaafu, anaendelea kuwa na mawazo ya busara kuhusu usimamizi wa fedha za umma.
 
Huyu mzee ni mjinga sn, badala aongelee matumizi mabaya na makubwa ya serikali kama misafara pamoja wizi wa mali za umma yeye anaongelea chuo ambacho ni muhimu kwa watanzania!
 
Back
Top Bottom