Chuo Kikuu cha Iringa chamtunuku Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Nishani ya Heshima kwa kuanzisha Vyuo Vikuu binafsi nchini wakati wa utawala wake

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
mkapa.jpg

Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini – Iringa) kinatarajia kumtunuku Nishani ya Heshima Rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kuanzisha vyuo vikuu binafsi, hivyo kukifanya Chuo Kikuu cha Iringa kuwa chuo cha kwanza binafsi nchini Tanzania wakati wa utawala wake. Nishani ya Heshima itatolewa pia kwa Mama Anna Mkapa katika mahafali chuoni hapo tarehe 07-12-2019.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Chuo hicho pia kitatoa Shahada ya Juu ya Heshima ya Sheria (Honoris Causa Juris) kwa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho, pamoja na Shahada ya Juu ya Heshima ya Usimamiaji na Utawala wa Biashara na Sayansi ya Uchumi (Honoris Causa Business Administration and Economic Science – Dr. BAESc) kwa Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland, Dr Vesa V. Viitamieni.

Wadau wengine watakaotunukiwa Nishani ya Heshima ni pamoja na Ndg. Salim Abri (ASAS) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela.

Chuo Kikuu Cha Iringa kilisajiliwa na kuwa Chuo Kikuu binafsi cha kwanza nchini Tanzania mamo tarehe 30 Desemba mwaka 1997.

Chuo hicho kilianzishwa mwaka 1993 wakati huo kikijulikana kama Chuo cha Kilutheri Iringa, huku kikitoa Stashahada ya Theolojia na Stashahada ya Juu ya Utawala wa Biashara.

Screenshot_20191204-095553.png

======

UPDATES: MATUKIO YA Desemba 7, 2019.

gradu-201913.jpg

Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa (kulia) wakifanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Prof. Ndelilio Urio (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho Jaji MKuu Mstaafu Agustino Ramadhani (wapili kushoto), baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ajili ya sherehe ya mahafali ambapo Mzee Mkapa alitunukiwa Nishani ya Heshima.

gradu-20194.jpg

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin W. Mkapa (wapili toka kulia, waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi, wafanyakazi wa chuo na wageni waalikwa waliohudhuria mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu cha Iringa yaliyofanyika tarehe 7-12-2019 katika viwanja vya chuo hicho. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani. Kulia kwa Mhe. Mkapa ni Balozi wa Heshima wa Ufini (Finland) nchini Tanzania, Dkt. Vesa Viitamieni; Mke wa Rais Mkapa, Mama Anna Mkapa; (mmoja tunamruka), Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela; na mwisho ni Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella.

gradu-20191.jpg

Rais Benjamin W. Mkapa akikabidhi nakala ya kitabu chake cha "My Life, My Purpose -- A Tanzanian President Remembers" kwa mmoja wa wahudhuriaji wa mahafali ya 22 ya chuo Kikuu cha Iringa.

gradu-201933.jpg

Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa akisoma kitabu cha mwongozo wa Mahafali
 
  • Thanks
Reactions: ank
Pia jamaa hakupenda misifa. Kama sio yeye kuanzisha, ungekuta pesa zote leo zina picha ya Magufuli halafu wapambe wakiwakejeli Wapinzani kama hawamtaki wasitumie pesa ya Magufuli.
 
Mipango mizuri, udahili utapanda na chuo kitatanuka, wigo was utoaji was taaluma mbalimbali utaongezeka, wabia watapatikana. Bodi ya wadhamini iendelee kufanya hivi, vinginevyo vyuo binafsi vitakufa kwani ushindani na vyuo vya unma ni mkali see baada ya maboresho tunayoyaona!
 
Back
Top Bottom