Rais Mbadilishe Waziri wa Katiba na Sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Mbadilishe Waziri wa Katiba na Sheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwikumwiku, Mar 1, 2012.

 1. m

  mwikumwiku Senior Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Bodi wenzangu, labda nianze kwa kusema sina wasiwasi na utendaji wa Celina Kombani hata kidogo kwa kuwa sote tumemuona akiwa naibu Waziri na baadae Waziri kamili kwenye wizara nyingine.

  Hata hivyo Kama kuna makosa makubwa ya uteuzi Wa mawaziri rais aliwahi kufana ni hili la kumteua Kombani kuwa Waziri Wa Katiba na sheria kwa kuwa ameshindwa kabisa kuiongoza na kuratibu shughuli za wizara hiyo na badala yake kumfanya AG afanye Kazi mbili, mtu ambaye hata Kazi yake tu ya u- AG inamahinda.

  Nasema hivyo kwa sababu, katika nyakati zote hakuna wakati mgumu kwa Wizara ya Katiba na Sheria kama kipindi hiki! Wizara inatarajiwa kuratibu mchakato Wa kutunga katiba mpya jukumu amabalo linahitaji siyo tu uzoefu Wa kisiasa bali taaluma na uelewa mkubwa Wa maswala ya sheria na katiba! Hivyo, ni wazi kabisa kwamba Kama kuna wakati ambao wizara hii inahitaji Waziri mwenye taaluma ya sheria kuliko wakati mwingine wowote basi ni sasa!

  Kunabaadhi ya hoja au majibu yanayotolewa na huyu mama ni hopeless mpaka yanakatisha tamaa! Kwamfano nimemfuatilia kwenye kipindi Cha baragumu asubuhi hii akiongea kwa njia ya simu unaona kabisa kwamba ni mbabaishaji! Ni mtu anayefanya mambo ili naye aonekane anafanya kitu fulani!

  Anailizwa mnawezaje kuwataka wadau walete majina kwaajili ya uteuzi Wa Tume bila kuwepo na kanuni zinazofafanua mchakato wa upatikanaji Wa hayo majina?! Anasema hilo lipo chini ya Ofs yangu nalishughulikia!!!!!

  Sasa mchakato utaendaje mama!!!! Teyari kuna mkanganyi juu ya jumuiya za kidini endapo kila jumuiya inatakiwa kuleta majina matatu au jumuiya zote zikae kwa pamoja na kuwasilisha majina matatu!!!! Mambo kama haya yanahita kanuni!

  Ushauri wangu kwa Rais ambadilishe huyu mama na alete mtu mwenye taaluma ya sheria! Wakati huu ni mgumu sana unahitaji Waziri mwanasheria! Huyu mama atakanganya sana huu mchakato!
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  ukiona jk katoa cheo kwa mtu,huyo mtu atakuwa;1.hawala.2.rafiki.3.adui(analazimika kutokana na upepo),kwa kesi ya kombani nafikiri namba 1 inafit the description.
   
 3. D

  DOMA JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Najua unamuona anapwaya ukimlinganisha na waziri mbadala Lissu
   
 4. S

  Sam Upendo Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu mwanzo Kombaini na Werema walipinga wazo la Katiba mpya, lakini Rais akawapuuza kutokana na nguvu za wimbi la mabadiliko. Hivyo watu hawa wataendelea kumshauri vibaya Rais ili mchakato wa Katiba ushindikane.

  Haiingi kichwani kwamba mpaka sasa hata Kanuni za Sheria ya uchaguzi bado kuandaliwa, hivyo hata Tangazo la kuwasilisha majina lilipashwa kusubiri mpaka Kanuni ziwe zimetayarishwa. Lengo lao zoezi likwame kabisa.

  Hivi Rais bado hajajiuiza kwa nini Sheria hiyo ina mushkeli kana kwamba haikuandaliwa na Ofisi Mwanasheria Mkuu? Hata Kanuni zikitoka nazo zitakuwa na Mushkeli.
   
 5. m

  mwikumwiku Senior Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna dhamira ya dhati hata kidogo!
   
Loading...