Rais Magufuli: Waliouziwa Viwanda wakashindwa kuviendeleza, Wakamatwe wawekwe Korokoroni

Heshima kwenu wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli, amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Mwijage kuhakikisha Wote waliouziwa Viwanda halafu wakashindwa kuviendeleza, wakamatwe na wawekwe ndani.

Anasisitiza kwamba Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya Viwanda, anataka kuona Viwanda kama ambavyo pwani wamefanya. Sasa hivi pwani ina viwanda zaidi ya 371.

=====
Pwani. Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa kuviendeleza.

Ameyazungumza hayo leo (Alhamisi) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.

“Kipindi cha nyuma tulipofanya makosa ni pale tulipouza viwanda kwa watu binafsi, sasa kuna viwanda 197 vimeshakufa waliouziwa hawajishughulishi na vingine vipo kama magofu,” amesema.

Kutokana na hilo, Rais amesema; "natoa wito kwa wote waliouziwa viwanda kipindi cha nyuma na sasa wameshindwa kuviendeleza , naagiza sasa basi mrudishe na wewe Waziri Mwijage tumia hata nguvu kama kuwaweka ndani weka tu siku akitoka huko atakuta kiwanda kimeanza kazi."

Chanzo: Mwananchi
Nataka kuamini kwamba huyu bwana hayuko sawa sawa wapi aliambiwa korokoroni inasaidia kuleta utengamano ni mambo ya ajabu sana
 
mnajua hata kama kumchukia Magu isifikie huku...hv mnajua viwanda vingi vilivyobinafsishwa vimegezwa maghala tu mi nampa big up sana atunyoshe tu aisee
Aiseee kumbe kwa serikali ipi ccm ya Zaman au mpya ya kesho after upinzani
 
Ndani kwanza, uchunguzi baadae. Huna hatia unaachiliwa, Tatizo liko wapi?

Unajua kesi wanazowafungulia siku hizi ! Uhujumu uchumi.......sasa hadi kesi iishe 3yrs baba unasota kwa kosa la kipuuzi!!! Ulinunua hukupewa bure.....wakurudishie pesa wachukue magofu yao macine za miaka 70 itaweza kuzalisha kwa ushindani miaka 45 baadae
 
Ukiwapanga wanasiasa wote walio hai hapa nchini.
Magufuli is second to none.
hilo halihitaji kuandamana wala elimu ya juu mkuu.
hata wewe unajua sema kiburi tu...
Huyo jamaa hapo juu kaleta kipande cha habari badala ya habari utadhani alikuwa anakimbizwa...
naona umechelewa umekuta ameshafanya editing.
Kama umemikili kiwanda kwa makubaliano ya kukiendeleza na umevunja kwa sababu zisizoeleweka lazima uchukuliwe hatua hakuna namna...
Kulikuwa na makubaliano yoyote? tuanzie hapo
 
mimi naishi kibiti mkuu.

kumbe rais ndiyo mtunga sheria za nchi??
Hahahahahahaha shauri yako. Reformation na overhaul ya mfumo wa kisekta hasa sekta za uchumi na ukizingatia hali iliyokuwa imefika ni lazima mkuu wa nchi awe hivi. Baadae mwishoni tukikaa sawa ananogesha na kakatiba basi maisha yanakuwa mswano kabisa. Lakini kwenye hii transitional period tutake tusikate kama tunataka kujinasua ni lazima taratibu hizi zifuatwe. Lazima zitakuwa chungu kwa baadhi ya wadau but hatuna jinsi. "The hard way The only Way"
 
Haya na alienunua meli mbovu ikashindwa kufanya safari japo moja na ikageuzwa faru Joni wa geshi
 
Hili li nchi ndio maana wazungu hawakuliendeleza kipindi cha ukoloni,

Nadhani walipima IQ,wakakuta tanzania ni ya chini kuliko Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi na Congo
 
Ukiwapanga wanasiasa wote walio hai hapa nchini.
Magufuli is second to none.
hilo halihitaji kuandamana wala elimu ya juu mkuu.
hata wewe unajua sema kiburi tu...
Huyo jamaa hapo juu kaleta kipande cha habari badala ya habari utadhani alikuwa anakimbizwa...
naona umechelewa umekuta ameshafanya editing.
Kama umemikili kiwanda kwa makubaliano ya kukiendeleza na umevunja kwa sababu zisizoeleweka lazima uchukuliwe hatua hakuna namna...
Hao watu walipewa hivyo viwanda kwa utaratibu gani? Kulikuwa na mikataba au walipewa sandakalawe? Kwenye uzi uliouadhisha ukaukimbia, umejidai wewe ni muumini wa sheria lakini nimekueleza ukweli kuwa wewe si muumini wa sheria bali ni mshangiliaji tu kama unavyoshangilia hapa. Hii nchi imejaa washangiliaji na haitofika kokote!
 
Back
Top Bottom