figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,852

=========================
MOROGORO NI MFANO WA MIKOA AMBAYO WALIONUNUA VIWANDA WAMEKUWA MAATAPELI NA WAONGO ..UKIANZA NA HUYO..
MOHAMED ABOOD
Alinunua viwanda zaidi ya vitatu , MOROGORO CANVAS ,MOROGORO OIL etc
Hakuna kiwanda kinachofanya kazi zaidi tu amevikopea bank ,kiwanda cha Morogoro canvas kilikuwa kiwanda cha mfano duniani na hadi leo mali zake zinauliziwa sokoni ...lakini amekifilisi na kuna hatari ameondoa baadhi ya mitambo
Huyu amefanya tumuamini magufuli kwa kuwa alikuwa ametumia pesa zake kuwafanya wana Morogoro misukule , kwa kutumia radio yake na misaada ya kiswahili kiswahili isiyo na tija kwenye dunia ya sasa ..
Mohamed Enterprises alipewa kiwanda kikubwa kuliko vyote afrika enzi hizo cha POLYTEX ...kinafanya kazi lakini kwa asilimia 30% na bado kinampatia faida kubwa , kiwanda hiki kina changamoto ya kuhamia technology ya makaa ya mawe ili kiweze kuwasha boiler zake na kuongeza uzalishaji .
MOROGORO SHOES COMPANY
Hiki kilipata bahati mbaya kwa kupaata mmiliki tapeli wa kimataida , mwenye sifa ya magendo aina zote , huyo pia ni yule ambaye amepata kuichoma hoteli yake Bagamoyo ili apate pesa ya bima ...na wakati huo hoteli yake ndio ilikuwa nzuri Bagamoyo ya kutegemewa na watalii na serikali kwa mikutano
Alipopewa kiwanda hiki maarufu kwa kutengeneza boot za jeshi ,rabber za shule na matumizi mbali mbali , kiwanda hiki kilikuwa kinapakana kabisa na Morogoro canvas kwa kuwa baadhi ya malighafi zake ni canvas ..kwa hiyo value addition inaendelea mlango wa pili tu ..
Huyu bwana kwa kushirikiana na watu wasiokuwa waaminifu alianza kuhamisha mashine za kiwanda kwa kuzifungua wakati wa usiku na kupeleka kigamboni dar es salaam ambapo alikuwa amejenga gododwn , baada ya kuwa amehamisha mali zote muhimu .....alikiwasha kiwanda kile moto .....kikaungua kabisa ......na kwakuwa alikuwa na bima Alilipwa kiwanda kizima ...akatajirika .........na kuja kufungua kiwanda Kigamboni kwa kutumia mashiine zile kwa jina la ITAL SHOE .
KIWANDA CHA MAN'GULA MOROGORO
Hiki kilikuwa backbone heavy-duty industry cha aina take afrika ...kilikuwa kinauwezo wa kumimina chuma au metal ya aina yeyote hata kama ni engine block ya treni ...ikitegemewa kuwa viwanda vyote vikubwa vingehudumiwa na MAN'GULA ...Kilikuwa kikishirikiana na kiwanda cha KILIMANJARO MASHINE TOOLS ambacho hiki kilikuwa na kazi ya kuchonga spares ndogo ndogo za viwandani .....ikiwa na maana kuwa Tanzania ilikuwa ikijitegemea kwa spares nyepesi na nzito za viwanda vyake ....
Aliyenunua kiwanda cha Mangula ni MCHUNGAJI RWAKATARE ambaye yeye nae kama huyo wa viatu ...amengoa mitambo yake yote ambayo ni world class na kuuza kama scrapper nje ..inasadikiwa kuwa wazungu walioinunua hawakaenda kuyeyusha bali wameikarabati na kuuaza kama complete line kwenye nchi nyingine ...
Karibuni wachina wanaowekeza mradi wa chuma LIGANGA waliomba kwenda kukiona wakitegemea wangeweza kuingia ubia ili kuanza nacho kwenye kutengeneza baadhi ya vitu kwa kutumia chuma yetu ...walishikwa na bumbuwazi kukuta kiwanda kimengolewa ....kwenye directory ya viwanda vizuri vya chuma kipo ndio maana ilikuwa rahisi kushauriwa na washauri wao ambao ni wachina wenzao wakitafute ..walishangaa sana sana ..
Kulikuwa na tawi la kiwanda hiki hapa DAR ..Hapo mwenge kanunua MCHUNGAJI MWINGIRA ..YEYE kabadili matumizi kinyume kabisa na masharti ya PSRC ...Na kufungua kanisa ...
MASHAMBA
Mashamba mengi tena ambayo yana viwanda nayo hayafanyi kazi au wana kawaida ya kulima karibu na lami ili wakubwa wakipita waone kinafanya kazi wakati sio kweli na hii ndio tabia nchi nzima
HITIMISHO
Nchi hii ilikuwa na viwanda vya kila kitu kuanzia sindano ,wembe ,radio ,nguo, ,nyama,matrekta ,malori etc ..hata waagizaji wa magari kama Landrover ,Layland etc walilazimishwa kama wanataka kuuaza magari tanzania wafungue ASSEMBLY HOUSES na ndio ilikuwa hivyo ikiwa na maana angalau asilimia 20% ya kazi ilifanyika hapa na kutengeneza ajira na kuacha ujuzi ...
Kulikuwa na mtandao wa viwanda karibu 500 vya serikali ambavyo viliuzwa na PSRC ....LAKINI ni vichache sana vipo , tuliwaamini watanzania wenzetu wenye asili ya nje lakini wengi walijitajirisha na kukimbia na kuacha magofu ....kuna viwanda kama KILTEX gongolamboto ambavyo kilikuwa kati ya viwanda bora ,hiki vibaka walifungua kila kitu hadi mabati na kuuaza baada ya kuwa kimtelekezwa .....
Watu wazima wanakumbuka those glory days ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa mijini walikuwa wameajiriwa viwandani , wanakaa kwenye nyumba za viwanda, wanasafiri kwenda na kurudi kazini kwenye mabasi ya viwanda , ilikuwa saa kumi wakati tunatoka shule idadi ya mabasi yaliyojaa barabarani kwa viwango vya enzi zile yalikuwa ya viwanda yakirudisha wafanyakazi kwenye quaters zao
Hii iilikuwa welfare ambayo ilikuwa lazima hata kwa viwanda binafsi kufanya huwezi kuruhusiwa kuwa na wafanyakazi 50 kwenda juu bila kuwa na basi la wafanyakazi ....na ikibidi pia kuwa na nyumba za wafanyakazi ....
Kwa viwanda vikubwa ilikuwa lazima kuwa na mpango wa matibabu ....kama hospitali ya wafanyakazi , kwa na mpango wa burudani kwenye makazi yao kama kuwawekea SOCIAL CENTRE , BAND , NA TIMU ZA MAKAZINI ..mpira wa miguu ,pete etc na wachezaji wanakuwa waajiriwa pia ..Viwanda vya pembezoni vilienda hatua moja mbele ya kujenga shule za awali na msingi kwenye nyumba za wafanyakazi .
Mishahara haikuwa mikubwa lakini watu walikuwa na furaha kwa ajili walihudumiwa kwa mambo mengi ....na ukizingatia na elimu ilikuwa bure kweli na matibabu kwa raia wengine bure ..kwa hiyo hutegemei kuombwa pesa na ndugu zako za shule au matibabu ...HUO NDIO ULIKUWA UJAMAA .
Kama mwalimu aliacha viwanda 500 ...kwa miaka 23 ya utawala wake ..ambapo hakuwa akichimba madini zaidi ya Almasi [AMBAYO nayo ilikuwa hauzi ghafi bali iliuzwa baada ya kuchongwa vizuri na kiwanda chetu wenyewe TANCUT ALMASI ] ...leo hatuna TANCUT GOLD ,TANCUT TANZNITE ,TANCUT ,RUBBY etc .., pamoja na kukabiliana na vita vya kagera na vita vya ukombozi kusini mwa afrika , na sera kandamizi za IMF na WORDBANK ....pengine bila vikwazo hivi leo Tanzania ingekuwa taifa linalojitegemea kwa kila kitu ...maana uchumi wetu uliharibiwa na sababu ambazo ziko valid na sio hizi za sasa za ufisadi
Kama kila rais aliyemfuatia Mwalimu angejenga nusu ya viwanda vya Mwalimu kwa kuwa wao wanakaa miaka 10 basi ni wazi leo tungekuwa tunakimbilia viwanda vikubwa 2000 ambavyo vingeweza kuajiri watu moja kwa moja milioni 2 ...na ukijumlisha na huduma mtambuka vingeweza kutengeneza shughuli za kiuchumi[ajira] milioni 8 [ratio 1:4]....watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi wapo milioni 15 ...hao waliobakiwa wangeweza kujiajiri kwa kilimo na biashara au sekta nyingine za ajira kama jeshi,uwalimu etc .....TANZANIA INGEKUWA INATAFUTA WAFANYAKAZI HASA WA MASHAMBANI KAMA ZAMANI TOKA NCHI JIRANI .....
VITA YA KURUDISHA VIWANDA NI VITA TAKATIFU NA MAGUFULI ASIRUDI NYUMA ...BORA KUFUATA MFUMO WA MAGEUZI YA VIWANDA VYA UMMA WA BORIS YELTSIN