Yuko mubashara Star Tv Anahutubia. Ameongeza kuwa huu ndiyo muda wa wakulima waliotunza mazao yao kutajirika.
"Asitokee kiongozi akawapangia bei ya mazao yenu", alisisitiza rais.
"Ikibidi mbadilishe debe moja la mahindi kwa ng'ombe 3", vicheko vikasikika.
=========
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka wakulima nchini kupandisha bei ya mazao kadri watakavyo kutokana na nguvu kubwa wanayoitumia katika uzalishaji wa mazao hayo.
Amesema hayo mara baada ya kuwepo malalamiko ya kupanda kwa bei za mazao mbalimbali hasa mahindi na mchele kutokana na upatikanaji wake kuwa mdogo.
"Wakulima pandisheni bei ya mazao kwa kiwango mnachotaka bila kuzuiliwa na mtu wala kiongozi yeyote wa serikali, mmekuwa mkipata shida nyingi kuhangaika hadi kuzalisha mazao hayo, huu ni mwaka wa neema kwa wakulima, tumieni fursa hii pandisheni bei za mazao kadri mnavyotaka,"amesema Rais Magufuli.
CHANZO: JPM: Wakulima pandisheni bei mtakavyo