Rais Magufuli wa Tanganyika 2015-2020

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
622
1,000
Ni wazi uchaguzi umeshavurugwa, hili halina shaka kitakachojiri anakijua Mwenyezi Mungu. Tunavyoona na inavyoonekana CCM inachuchukua ushindi kwa kuengua wagombea ikiwa ni zoezi la mwanzo, zoezi la pili ni kuengua wapiga kura, zoezi la tatu ni kubadili matokeo ya kura ikifuatiwa na zoezi la mwisho la kumtangaza mtu ambaye au watu ambao hawakuchaguliwa kwa ridhaa za wananchi.

CCM inatumia kila hila kumfanya awepo kwenye madaraka kwani visa na vitendo vya watendaji vimewafanya raia wauchukie utawala wa Mheshimiwa Magufuli na kutaka mabadiliko, leo CCM inalazimika kutumia na kuwakumba wasanii wote wa Tanzania.

Inatumia mchezo huo kuwalaghai watanzania walio wengi ambao elimu yao kuyafahamu yaliopo duniani ni mdogo sana.

Na huu mchezo uliofanywa na Tume ya Bashiru na Polepole itamharibia Dkt. Magufuli, mimi naamini bila ya vurumai hizi za Tume Magufuli angelishinda japo kwa asilimia ya kiasi na ingekubalika wala isingetia ila ushindi wake.
 

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
3,565
2,000
CHADEMA mnajiona mnaakili kwelikweli.

Wakati Lissu anaweka pingamizi kwa Magufuli na Lipumba kwamba hawajaweka picha kwenye form huko sio kutaka abaki peke yake?

Acheni kulialia kama watoto wa mwisho.

Mnajua uchaguzi hamshindi imebaki kiki ya bajaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom