OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,073
- 114,572
Kama kuna watu waliopata thawabu na baraka nyingi wiki hii ni Prof.Musa Assad (Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali - CAG). Ripoti yake haijaacha kitu. Imegusa kila penye uchafu.
Kama ni dawa ya Mbu basi ni "Heat". Inaua mbu, nzi, sisimizi, mende, vipepeo na kila kitaambacho au kirukacho.
Kwa wananchi hii ni ripoti iliyoleta matumaini na kuwawezesha kujua nchi yao ikoje, lakini kwa baadhi ya watumishi wa umma na wanasiasa ripoti hii ni kirusi..Wanatamani wasiione.Kama wewe ni mwanasiasa au mtendaji mkubwa serikalini unahitaji kutafuna kwanza"pilipili kichaa" kwa wingi ndio upate ujasiri wa kusoma ripoti hii.
Imegusa kuanzia wizara ya ujenzi ambayo Rais Magufuli alikuwemo, Halmashauri, vyama vya siasa, watumishi wa umma, taasisi, mashirika ya umma, hadi Intergrity za wabunge wetu.Lakini napenda kuuliza kwa yeyote mwenye taarifa anijuze.Hivi Mhe.Rais si alikua Mbunge kwa miaka 20? Je anaingia kundi lipi kwenye saga ya mafuta kwa wabunge?
Alikua anatembelea jimboni kila mwezi au alikua hapokei fedha ya mafuta kabisa? Kuna yeyote mwenye taarifa? Pia vipi ile wizara iliyotumia mara 4 zaidi ya bajeti waliyoidhinishiwa? Kuna hatua zozote zitachukuliwa kwa watendaji wa wizara hiyo?Anyway mwambieni ripoti ya CAG imemuongezea idadi ya"majipu" ya kutumbua na amekupa mtihani wa kujitumbua mwenyewe kwa issue ya wizara ya ujenzi.
Lakini chondechonde usijaribu KUMPANGIA KAZI NYINGINE mteule wetu Prof.Assad. Kwasasa ndiye mtu pekee anayeaminika zaidi nchini.Baada ya taarifa ya jana nimegundua wananchi wanamuamini zaidi Prof.Assad kuliko hata wabunge waliowachagua. Wanamuamini kuliko wanavyowaamini Maimamu na maaskofu wao.Kimsingi wanamuamini CAG kuliko Ikulu. Mungu azidi kumpa heri na maisha marefu.