toroka uje mjini
JF-Expert Member
- Mar 29, 2017
- 1,584
- 2,108
Mbona hujaifafanua vizuri hio hotuba ulimsikia????Jana nimemsikia JPM akilalamika kwamba uzalishaji ni mdogo hivyo hawezi kuongeza mishahara ya watumishi wake
Nakumbuka awamu ya tano ilikuja na mkwara mkubwa wa kuondoa fedha zote za serikali katika mzunguko kwa mara moja,wataalamu walionya kwamba kutatokea athari kubwa sana kiuchumi kwa kuwa kimsingi,serikali ndio mwanahisa mkuu wa uchumi wa nchi na kwa vyovyote vile akijiondoa lazima kampuni iyumbe na kisha ife
Serikali ilipoondoa fedha katika mabenki na kuzipeleka Benki Kuu,ni wazi kuwa kule zimelala tu na kuozeana,haziingizi faida kwa serikali wala katika uchumi wa mtaani,hii ni tofauti na pale zilipokuwa katika mabenki ya kibiashara ambapo zilikuwa zinakopeshwa kwa wenye viwanda na wajasiliamali ambao walizizungusha na zikaleta faida kubwa,mjasiliamali alikopa,akafungua biashara,akalipa leseni ,kodi,tozo,zote zinaenda serikalini,hapa maana yake pesa hiyo imezaa kwa serikali kupata kodi,na maana yake uzalishaji umeongezeka,watumishi wataongezewa mishahara kutokana na fedha hiyo kuzunguka
Pia serikali kama imeweka fedha hiyo katika fixed deposit,nako fedha hii ingezaa riba,kwa hiyo kotekote serikali ingekula,kuna taarifa kwamba yale mashirika yaliyolazimishwa kupeleka fedha benki kuu yameomba kibali cha kutumia fedha ya mtaji ili kulipana mishahara,wakati zamani ile faida ya fixed deposit ilitosha kulipa mishahara bila kugusa mtaji,taarifa zilizopo zinaonyesha yameruhusiwa kutumia si zaidi ya asilimia 15 ya mapato kulipana mishahara
Nakumbuka Beno Ndulu,Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya wana uchumi sugu waliokuwa TRA walikwazana naye mpaka akaivunja Bodi
Natoa wito kwa JPM,rudisha mzunguko wa fedha ili zizaane na uzalishaji wa kiuchumi uongezeke ulipe watumishi wako,vinginevyo utapaona ofisini pachungu kwa kukosa hela
Naifananisha amri yako ya kuweka fedha Benki Kuu na ile habari ya talanta kwenye Biblia,kuna mmoja alipewa hakuizalisha bali aliifukia chini ,wenzie wawili wakazalisha na wakapongezwa,yule aliyeifukia alifokewa na kutimuliwa na bosi wake
Taratibu naona waajiri wako wananchi wanaanza kufoka na kunun'gunika,wamekupa talanta,wanaona haizai
Mwisho kabisa,serikali na wananchi has a sekta binafsi,tunajenga Nyumba moja,acha kugombea fito,toa fito zako benki kuu,lete uraiani tuendelee na ujenzi
BENKI ILIWEZA KUJIENDESHA KWA PESA ZETU WENYEWE..
YAANI IMETOLEWA MIL600 IPELEKWE HALMASHAURI YA MKOA FLANI.
HIO PESA IKAZUILIWA NA MTU MMOJA NA AKAIWEKA BANKI KWA MIEZI 6. HAPO ATAVUTA RIBA(intres)HAJALI UCHELEWESHAJI WA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI.
AKISHAVUTA RIBA YAKE BAADA YA MIEZ 6 HIO PESA ANAIREJESHA HALMASHAURI .
HAPO HATA MFANYA MAHESABU WASERIKALI HATOGUNDUA KAMA KUNA SHOTI.ISIPOKUA NI UCHELEWESHWAJI WA HIZO PESA
KWA MANTIKI HIO HIZI BANKI ZILIKUA ZIKIFANYA BIASHARA NA HELA ZA SERIKALI(ambazo ni.Pesa zetu sisi walipa kodi)
KWA AWAMU HII HAIPO.HIO DILI.
NDIO MAANA WANAJILIZA LIZA KUA WANAFILISIKA..
Mleta mada fafanua ki hivi Mkuu